Miundombinu ni ya thamani kuliko uhai wa watanzania

Miundombinu ni ya thamani kuliko uhai wa watanzania

Mtanzania2020

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
1,033
Reaction score
2,307
Waliotekwa, waliouawa hatuoni wala hatuumi. Ila tumeona miondombinu ikiharibiwa na imetuuma.

Hii haikubali.

-Yaani hotuba zote za wenye mamlaka ya juu katika nchi hazigusii uharibifu wa uhai wa watu. Ila uharibifu wa mali na miundombinu.

-Hotuba hazionyeshi kukubali kuwa wapo waliotekwa, au kuuawa bila kosa linalostahili adhabu hiyo.

-Hotuba hazionyeshi uwezo wa kuwajua watekaji na wauaji wa watu ila wanaoharibu miondombinu.

-Hotuba hazionyeshi kutambua uwepo wa kubambikiwa kesi kwa wakosoaji wa makosa mbalimbali katika jamii.

-Hotuba zinazoamini kuwa kuuawa, kutekwa, kuteswa, kuonewa, kubambikiwa kesi kwa watu wasio na hatia ni kulinda amani. Ila maandamano ya amani yakiharibu miondombinu sio maandamano ya amani. Yaani miondombinu ina thamani, ni ya maana kuliko uhai wa watu. Yaani hatukubali kuwa hiyo ni njia ya watu kuonyesha kuwa wanaouawa wana thamani kuliko miundombinu.

Hii haikubaliki na inaonyesha kubariki vitendo vyote viovu. Hotuba za aina hii zisipopata mbadala kifuatacho ni mauaji, utekaji na utesaji watu kwa kiwango cha kutisha. Na kama hali itakuwa ni hivi, basi wengi wetu mfano wa mwandishi wa posti hii hatutaishi siku nyingi kutoka tar ya kuandika post hii. Kwani nitaonyesha namna zote kupinga hali hii. Ni mawili tu eidha kufa mapema au sauti yangu ihusike kukomesha haya. Ukweli njia hii haitafanikiwa kuinyamazisha sauti ya haki Tanzania. Haki itashinda hata kwa kuuawa maelfu katika sisi tunaopinga dhuluma hii ambao baadhi tumepata madhara mengi ya kuuawa ndugu zetu kwa sababu hii.

Ushindi unatakiwa kutokea mapema iwezekanavyo. Hii haikubaliki.

1001323527.jpg
 
Back
Top Bottom