KERO Miundombinu ya mabomba kwenye Vyoo vya 'Magufuli Bus Terminal' imeharibika, maji yanatoka ovyo na hakuna anayejali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kituo kikuu cha Mabasi Dar es Salaam 'Magufuli Bus Terminal' ni miongoni mwa maeneo ambayo Serikali imekuwa ikikusanya mapato, kutokana na hilo inatarajiwa Miundombinu na huduma za kituo hicho ziende sambamba na kodi na tozo wanazotozwa Wananchi ambao wamekuwa wakifika eneo hilo.

Kwa sasa licha ya changamoto ambazo tumekuwa tukilalamikia ikiwemo stendi kukosa maji nyakati tofauti, tozo za vyoo ndani ya stendi, lakini kwa sasa kuna changamoto nyingine ambayo sio ya kukalia kimya kungojea jahazi lizame.
photo_2024-09-29_14-43-40.jpg

photo_2024-09-29_14-43-39.jpg

photo_2024-09-29_14-43-38.jpg
Licha ya kutozwa tozo za huduma za vyoo, ambapo kila Mtu anayeingia kwenye maeneo kwenye choo vilivyopo ndani ya stendi kutozwa Tsh.200, lakini inashangaza miundombinu ya mabomba ya vyoo imeharibika inatoa maji kiholela na hakuna jitihada zinaonekana kuboresha.

Kwa kuwa kuna waliopewa mamlaka ya usimamizi ambao wamekuwa wakikusanya hela ya huduma ya vyoo tofauti na tozo nyingine ambayo utozwa kwa abiria wakati wa kuingia ndani ya stendi wakaboresha miundombinu hiyo wasingojee ichakae zaidi na kupelekea kero zaidi kwa watumiaji.

Pia soma:
~
Stendi ya Mbezi Magufuli hakuna maji siku ya pili leo
~ Watoza ushuru stendi ya mabasi Magufuli hawatoi risiti hivyo kuikosesha mapato manispaa
 
Wajanja walipiga pesa huku wakimhadaa Shujaa 😁😁
 
Si Kuna meneja wa hicho kituo?
Au huyo meneja Ni muha?
Hapo anatakiwa meneja mnyasa, wakati mwingine msiangalie vyeti tu wakati wa kuajiri. Angalieni na asili ya mtu alikitokea.
 
Hakuna anayejali ...... wapo wanaojali ushahidi wa kwanza ni wewe mwenyewe uliyeamua kuposti humu.

Sasa mpo wengi tu mnaojali na matokeo yataonekana usijali ndugu 🤝
 
Back
Top Bottom