Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hali ilivyo sasa
Hali ilivyokuwa
Miundombinu ya Shule ya Msingi Kamama ikiwemo Vyoo na Madarasa imefanyiwa maboresho ikiwa ni miezi kadhaa yangu kuripotiwa kuwa imechakaa na inahatarisha usalama wa afya wa Wanafunzi na wahusika wengine.
Inadaiwa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui imechukua hatua ya kuboresha majengo hayo.
===============V==================
Julai 31, 2024
Mdau alielezea maoni yake kuwa Shule ya Msingi Kamama iliyopo, Kijiji cha Kamama, Kata ya Goweko kuwa haina miundombinu mizuri hasa ya Vyoo na madarasa ambapo alieleza Shule hiyo ina jengo moja la vyoo ambalo lina matundu kati ya 6 au 8 na yote yakiwa katika hali isiyofaa kiafya, hivyo kusababisha baadhi ya Wanafunzi kujisaidia porini.
Kusoma zaidi bofya hapa ~ Hali ilivyo Shule ya Msingi Kamama (Tabora) inasikitisha, vyoo ni chakavu na vichafu, madarasa ndio usiseme
Agosti 25, 2024
Mdau akaripoti kuwa amepita Shuleni hapo na kubaini ujenzi umeanza wa maboresho umeanza ambapo ulihusisha Vyoo na madarasa ambayo ni chakavu.
Kusoma zaidi, bofya ~ Baada ya picha za vyoo vya Shule ya Kamama (Uyui - Tabora) kuziweka hapa JF, nimeona wanajenga vyoo vipya