Miundombinu ya Shule ya Msingi Kamama yaboreshwa, Vyoo na madarasa vyajengwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


Hali ilivyo sasa


Hali ilivyokuwa

Miundombinu ya Shule ya Msingi Kamama ikiwemo Vyoo na Madarasa imefanyiwa maboresho ikiwa ni miezi kadhaa yangu kuripotiwa kuwa imechakaa na inahatarisha usalama wa afya wa Wanafunzi na wahusika wengine.

Inadaiwa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui imechukua hatua ya kuboresha majengo hayo.



===============V==================

Julai 31, 2024
Mdau alielezea maoni yake kuwa Shule ya Msingi Kamama iliyopo, Kijiji cha Kamama, Kata ya Goweko kuwa haina miundombinu mizuri hasa ya Vyoo na madarasa ambapo alieleza Shule hiyo ina jengo moja la vyoo ambalo lina matundu kati ya 6 au 8 na yote yakiwa katika hali isiyofaa kiafya, hivyo kusababisha baadhi ya Wanafunzi kujisaidia porini.

Kusoma zaidi bofya hapa ~ Hali ilivyo Shule ya Msingi Kamama (Tabora) inasikitisha, vyoo ni chakavu na vichafu, madarasa ndio usiseme

Agosti 25, 2024
Mdau akaripoti kuwa amepita Shuleni hapo na kubaini ujenzi umeanza wa maboresho umeanza ambapo ulihusisha Vyoo na madarasa ambayo ni chakavu.

Kusoma zaidi, bofya ~ Baada ya picha za vyoo vya Shule ya Kamama (Uyui - Tabora) kuziweka hapa JF, nimeona wanajenga vyoo vipya
 
Big up mkuu waikumbuke na shule ya msingi Simbo wilaya ya Kigoma vijijini..shule hyo ni kongwe kati ya shule kongwe ila imechakaa kweli kweli utadhani viongozi wa kule hawaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…