KERO Miundombinu ya Stendi ya Urambo ni duni, inatia aibu, Vyoo navyo ni hatari kwa Afya za Watumiaji

KERO Miundombinu ya Stendi ya Urambo ni duni, inatia aibu, Vyoo navyo ni hatari kwa Afya za Watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
WhatsApp Image 2025-03-27 at 10.43.27_4734a394.jpg
Juzi nikiwa katika safari zangu nilipita Urambo, nilipofika katika Stendi ya Wilaya ambapo basi letu lilipita hapo, nilishangazwa na muonekano wa Kituo hicho, kilikuwa ‘too local’, mazingira yake sio mazuri na ukweli hali hiyo inasikitisha.

Tulishuka na wenzangu kadhaa na kwenda kwenye vyoo vya Wanaume, tulilipa ili kuingia kupata huduma, huko nako tukakuta hali siyo nzuri, usafi hauzingatiwi na inavyoonekana hapafanyiwi usafi vizuri jambo ambalo ni hatari kwa afya.
WhatsApp Image 2025-03-27 at 10.43.42_a2356af5.jpg

WhatsApp Image 2025-03-27 at 10.43.37_e9873479.jpg

WhatsApp Image 2025-03-27 at 10.43.31_5af01981.jpg

WhatsApp Image 2025-03-27 at 10.43.34_32cf92e1.jpg

​
Nilipouliza kuhusu Stendi hiyo nilijulishwa kuwa lazima mabasi yapite hapo na yanalipia, yale ambayo hayapiti yanakutana na adhabu kali.

Nilichobaini ni kuwa miundombinu ipo duni na usalama wa Vyoo pia nao mzuri, nashauri Mamlaka zinazohusika zichukue hatua.
WhatsApp Image 2025-04-07 at 19.33.36_a250f582.jpg
 
Back
Top Bottom