mdesi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 1,367
- 2,220
Naomba niende direct kwenye point;-
Huwa nachukizwa na kupata uchungu sana kuona raia wanaharibu miundombinu ya umma kwa maksudi bila sababu yeyote ya msingi. Yaani si kwa bahati mbaya wala sababu fulani justifiable iliyo sababisha uharibifu huo.
Pamoja na sehemu nyingine hapa ubungo chini ya daraja pamejengwa uzio mzuri tu kuzuia watu wasitumie eneo chini ya daraja ambapo kabla hapajawekwa uzio paligeuka sehemu ya malazi kwa vijana wadogowadogo.
Kilichonisukuma kuandika hapa; ni hali ambayo nilikuwa naiona siku kwa siku ule uzio unakatwa/chanwa sehemu mbalimbali, kidogokidogo kuanzia kwa juu kushuka chini, nikajua mamlaka husika labda wameona baadae ikaenda mbali zaidi wakakata na kung'oa kipande kizima cha fence na kutokomea nacho walikokujua wao na kuacha pakiwa wazi. Watu wanaweza ingia na kutoka bila kizuizi kutupa uchafu nk.
Hivi mamlaka za ulinzi wa watu na mali zao wameshindwa kudhibiti kitu kama hicho cha uharifu wa miundombinu?
Kinacho ni choma zaidi miundombinu hiyo imejengwa kwa kukatwa 30% ya monthly salary yangu na mamlaka za ulinzi zinakula salary kutoka kwenye 30% yangu.
Inashindikanaje kuwadhibiti vijana wa mtaani??