KERO Miundombinu ya vyoo Mnada wa Mbuzi - Kibamba ni kichefuchefu! Mamlaka za Afya Wilaya ya Ubungo mpo wapi?

KERO Miundombinu ya vyoo Mnada wa Mbuzi - Kibamba ni kichefuchefu! Mamlaka za Afya Wilaya ya Ubungo mpo wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Salamu Wakuu,

Kwa waliowahi kufika Kibamba kwenye mnada maarufu wa nyama tamu ya mbuzi, bila shaka mtakuwa mmekutana na changamoto kubwa ya miundombinu duni – hasa vyoo.

Hali ni ya kusikitisha. Vyoo havina maji tiririka, vinyesi vinaonekana waziwazi, na mazingira ni machafu kupindukia. Vibanda vya biashara vimefunikwa kwa turubai zilizochakaa, hali inayoashiria kutotiliwa maanani kwa usalama wa wateja.

Cha kushangaza, wafanyabiashara wa mnada huu wanalipa Tsh 15,000/- kila mwezi, kwakuwa ni mnada wa mara mbili tu kwa wiki (Jumatano na Jumapili). Ukiangalia idadi yao – zaidi ya 100 – mapato haya yanatosha kabisa kuboresha miundombinu ya vyoo, hata kama vitakuwa vya kulipia kama ilivyo kule Loliondo, Mailimoja, Kibaha.

Je, viongozi wa afya wa Wilaya ya Ubungo wapo wapi? Hakuna viwango vya usalama wa afya vinavyopaswa kuzingatiwa kabla ya eneo kuruhusiwa kutoa huduma za chakula? Inawezekana vipi sehemu inayohusisha afya za watu kuachwa katika hali mbaya kiasi hiki?

Natoa wito kwa mmiliki wa eneo na wafanyabiashara kuhakikisha miundombinu ya vyoo inaboreshwa haraka. Kwa sasa, watu wanalazimika kujisaidia vichakani kwa kuhofia hali mbaya ya vyoo, jambo linaloongeza hatari ya magonjwa.

Mamlaka za afya na usafi wa mazingira za Wilaya ya Ubungo zinapaswa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha mazingira ya eneo hili yanakidhi viwango vya afya na usafi.

Kumbukeni, hii si tu sehemu ya biashara jamani – ni eneo la burudani kwa watu wengi sana kutoka maeneo mbalimbali ya Dar na Pwani.

Mnasubiri mlipuko wa magonjwa ndipo mchukue hatua?

1000385786.jpg
1000385790.jpg
1000385788.jpg

1000385794.jpg

1000385784.jpg
 
Back
Top Bottom