Mivutano na kukosoana visisababishe utengano wa kidini. Tunahitajiana sote

Mivutano na kukosoana visisababishe utengano wa kidini. Tunahitajiana sote

TrulyP

Senior Member
Joined
May 25, 2024
Posts
195
Reaction score
417
Umuofia kwenu wanabodi!

Kutokana na uhuru wa kikatiba tulionao wa kutoa mani, siku za hivi karibuni kumekuwa na watu binafsi au makundi mbalimbali ya kijamii yanayojitokeza kusajili (register) hisia zao mbele ya umma - Jambo jema kabisa kwa jamii inayoheshimu na kustawisha fikra mbadala miongoni mwa watu wake.

Moja ya makundi yaliyotoa maoni na mitazamo yao kuhusu yanayoendelea nchini, ni Taasisi za dini za kikikristu na kiislamu. Matamko hayo yametolewa hadharani kwa lengo la kufikisha ujumbe kadiri wanavyoona inafaa.

Kinachosikitisha ni pale ambapo kundi lingine linapoacha kuandaa na kutoa kauli zao wenyewe, badala yake kujikita katika kushambulia (attack) waliotumia uhuru wao kutoa tamko kabla ya wao.

Hii imetokea ndani ya dini zenyewe (wakristu kwa wakristu, waislamu kwa waislamu n.k) lakini pia dini moja kwenda nyingine. Mashambulio hayo yana lugha za kuudhi na huenda yanatolewa ili kuanzisha vuguvugu kwamba kundi fulani sio bora kama wao n.k

Jambo hili sio afya kwa umoja wa taifa hili ambao kamwe haukujengwa juu ya misingi ya kiimani. Bila shaka wapo wanaoshabikia au kuhamasisha matendo haya ya hatari kwa kudhani yanasaidia kuhamasisha wanachokiamini na kufifisha kile wanachokipinga.
LAKINI

Tujihadhari, historia inaonesha chuki za kidini ni mbaya sana, huanza kidogo kidogo kama hivi baadae zinageuka hata mauaji.
USHAURI:

Makundi na taasisi mbalimbali zenye mitazamo tofauti zijiepushe kushambuliana kwa maneno ya kukera, badala yake kama wana la kusema, uhuru upo, na wao watoe tamko kuelezea hisia zao bila kulenga kukanusha au kushambulia kundi jingine.
HITIMISHO

Kwa wale tunaoamini Mungu, tumuombe Mungu atuvushe salama
 
Waambie wale Mashekhe watulie wanasemaje yaliopita sio ndwele wanataka kutusahaulisha na hapo bado hatujazika na matanga bado hatujaanua....?
 
Umechelewa sana ndugu yangu maji yameshamwagika ungetakiwa kusema haya mwezi wa tisa!!! watoto wamekufa unataka ustaarabu sasa baada ya kupuuza na kudharau watu ni ngumu sana. Sasa tumeamsha hasira kubwa kwa watu na kutuliza ni lazima tupate katiba mpya
 
Mwenyewe nliondoka humu JF mwaka huu mwanzoni baada ya cm kupotea na nimekuwa nikifuatilia tu wadau na madini wanayotema na niseme ni bora zaidi kusikiliza kuliko kuongea au kukomenti .Sijapanga kusign in humu Ili nichangie kitu ila baada ya post yako nami nimeona niseme pia ndoto nlizoota a year after Jiwe passed,nliota ndoto tatu zinazofanana za jeshi(sijui ni jeshi Gani)ila wamevaa full black with masks killing without remorse,hali ilikuwa inatisha sana and according to the dreams these three waves each bigger than the first,iliniacha very desperate na ukiwa ukaikumba nchi,Baada ya ndoto hizo ambazo nakumbuka Kila nukta kama muvi zilinisumbua sana na kumfuata mchungaji ambaye hata hivyo alisema ni Mungu anajaribu kusema Kuwa maisha yangu yatakuwa magumu jihadhari.Ila baada ya mo29 tarehe 01 nimeota the same dream vividly ndio nikajua hasa nini kinaendelea,kwa kweli sikupenda kuja humu kucoment maana naona utamu zaidi kusoma comments ila kama The most high gave me these dreams as gave other righteous nikaona ni lazima na Mimi nitoe neno japo litamsaidia hata Mtu mmoja aliye wa haki basi hakikisha unaombea wenye haki wengine wa Mungu,aweze kutupa ulinzi kwa yale yasiyo budi kutokea

Sijasema after those dreadfull dreams hakuna bright future,nliota pia ndoto za mwanga mpya na uonevu wa wenye haki ukipungua sana katika nchi yangu.

Pia naamini Farao Bado una nafasi ya kuuma Ego zako na kumrudia Mungu kwa Toba ya kweli na majuto maana niliona kundi kubwa la watu (na pale ilikuwa msibani) vividly nakumbuka rangi za mkutano ule zilizotawala ikiwemo njano pamoja na picha za Farao yule.

Aliye na maskio na asikie...Ntarudi Mungu akipenda maybe next year kama atatuweka.Godspeed
 
Back
Top Bottom