Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akikabidhi cheti cha shukrani kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas, Bi. Angelica Pesha, kutambua mchango wa Kampuni ya Mawasiliano ya Yas katika kushirikiana na Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC). Hafla hiyo ilifanyika Zanzibar wakati wa uzinduzi wa ZHC Connect App pamoja na Mwinyi Housing Scheme, miradi miwili ya kidijitali inayolenga kurahisisha huduma za makazi. Kushoto ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali na kulia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas - Angelica Pesha akisoma hotuba yake wakati wa hafla hiyo.