Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati mwingine mtu unatamani kusema sisi watanzania ni majuha lakini unaheshimu uumbaji wa Mungu wetu.
Jinsi mambo ya hovyo yanayofanywa na baadhi ya watu tuliowapa madaraka yanavyotia kinyaa, mtu unatamani kusonya lakini ukweli ulio mbele yetu unakutia aibu.
Wakati mwingine unaposikia mtu anasema "Kuna watu ni mazuzu" unaanza kudhani anatusema sisi, hasira zinakupanda lakini unatulia unapokumbuka uhovyo hovyo tulio nao.
Ni lini watanzania tutajua kwamba Hawa wanaofuja, kutapanya na kuiba mali za Umma/serikali huwa wanatuibia sisi!??
Kifanyike nini kwetu hadi tuone kwamba tunatakiwa kuasi dhidi ya mafisadi na wezi wanaotuibia kupitia nafasi za kimadaraka walizo nazo!?
Ni lini tutajitofautisha kiakili na utashi kati ya sisi tulioumbwa binadamu na Ng'ombe!?
Kuvumilia kwetu mambo ya hovyo hakuoneshi kuwa sisi hatukustahili kujitawala!!??