Mizaha tunayofanya kwenye mambo ya maana inaonesha jinsi watanzania tusivyojiheshimu!!

Viongozi wetu wanatumia fursa ya ujinga wa wananchi kufanya mipango yao michafu. Wanajua kabisa watanzania wengi kichwani hamna kitu.
Jamiiforums kuna wasomi wengi nadhani ila nini wanafanya nje ya jamiiforums? Utagundua shida sio ujinga maana hata huo ujinga unaweza kutumika kufanya mapinduzi. Waarabu wametuzidi elimu kiasi gani ila hakuna mambo kama yetu huku.
 
Hili jambo ndiyo hatari yenyewe...
Hio ndio tabia ya Nyumbu, mmoja wao akiwa attacked wengine wanakaa pembeni wanamshangaa anavyolia kwa uchungu huku akitolewa roho na kundi dogo la simba.

Wakati kwa wingi wao wanaweza kuwafurusha hao simba watatu na kumuokoa mwenzao. Huo umoja haupo kwa Watanzania.
 
Jamiiforums kuna wasomi wengi nadhani ila nini wanafanya nje ya jamiiforums? Utagundua shida sio ujinga maana hata huo ujinga unaweza kutumika kufanya mapinduzi. Waarabu wametuzidi elimu kiasi gani ila hakuna mambo kama yetu huku.
Waarab wana uthubutu sisi hatuna...
 
Wakati mwingine mtu unatamani kusema sisi watanzania ni majuha lakini unaheshimu uumbaji wa Mungu wetu.

Jinsi mambo ya hovyo yanayofanywa na baadhi ya watu tuliowapa madaraka yanavyotia kinyaa, mtu unatamani kusonya lakini ukweli ulio mbele yetu unakutia aibu.

Wakati mwingine unaposikia mtu anasema "Kuna watu ni mazuzu" unaanza kudhani anatusema sisi, hasira zinakupanda lakini unatulia unapokumbuka uhovyo hovyo tulio nao.

Ni lini watanzania tutajua kwamba Hawa wanaofuja, kutapanya na kuiba mali za Umma/serikali huwa wanatuibia sisi!??

Kifanyike nini kwetu hadi tuone kwamba tunatakiwa kuasi dhidi ya mafisadi na wezi wanaotuibia kupitia nafasi za kimadaraka walizo nazo!?

Ni lini tutajitofautisha kiakili na utashi kati ya sisi tulioumbwa binadamu na Ng'ombe!?

Kuvumilia kwetu mambo ya hovyo hakuoneshi kuwa sisi hatukustahili kujitawala!!??
Tatizo tunaogopa wanapotumia gobore kuuwa mbu hapo ndio tatizo linapoanzia kila mtu anatamani kuongea ila nani atamlinda baada ya kuongea vanessa mdee alipokuwa Tanzania alikuwa mtiifu ila sasa hivi yupo marekani anapaza sauti kwa hyo lazima uangalie mara mbili mbili kabla hujachangia.
 
Kwa ivo tunataka nani aongee Kwa niaba yetu... Au tumezoea maumivu!??
 
Jamiiforums kuna wasomi wengi nadhani ila nini wanafanya nje ya jamiiforums? Utagundua shida sio ujinga maana hata huo ujinga unaweza kutumika kufanya mapinduzi. Waarabu wametuzidi elimu kiasi gani ila hakuna mambo kama yetu huku.
Ni kweli kabisa, ujinga plus njaa matokeo yake ndyo haya. Hata wasomi wananunulika na kukosa uadilifu kutokana na njaa zao
 
Wakati mwingine mtu unatamani kusema sisi watanzania ni majuha lakini unaheshimu uumbaji wa Mungu wetu.

Jinsi mambo ya hovyo yanayofanywa na baadhi ya watu tuliowapa madaraka yanavyotia kinyaa, mtu unatamani kusonya lakini ukweli ulio mbele yetu unakutia aibu.

Wakati mwingine unaposikia mtu anasema "Kuna watu ni mazuzu" unaanza kudhani anatusema sisi, hasira zinakupanda lakini unatulia unapokumbuka uhovyo hovyo tulio nao.

Ni lini watanzania tutajua kwamba Hawa wanaofuja, kutapanya na kuiba mali za Umma/serikali huwa wanatuibia sisi!??

Kifanyike nini kwetu hadi tuone kwamba tunatakiwa kuasi dhidi ya mafisadi na wezi wanaotuibia kupitia nafasi za kimadaraka walizo nazo!?

Ni lini tutajitofautisha kiakili na utashi kati ya sisi tulioumbwa binadamu na Ng'ombe!?

Kuvumilia kwetu mambo ya hovyo hakuoneshi kuwa sisi hatukustahili kujitawala!!??
Hawatakuelewa hata kidogo!
 
Back
Top Bottom