Kuna habari za kuaminika kutoka vyanzo vilivyo serikalini inayoelezea mabadiliko mazuri ambayo yako mbioni kufanyika mintarafu mizani na vipimo vya kupimia wanyama hapa nchini.
Kufuatia mafanikio makubwa ya kufaulisha watahiniwa wa kidato cha sita kwa kubadilisha viwango vya ufaulu, serikali imeagiza mizani mpya zitengenezwe ili kile kinachosomeka kama kilo moja sasa kianze kusomeka kilo mbili. Kwa njia hiyo, ng'ombe wetu atakayekuwa na uzito wa kilo 200 atasomeka ana kilo 400. Na itakuwa ni mafanikio katika ile kaulimbiu ya BIG RESULTS NOW. Halafu tutafanya sherehe kubwa nchi nzima kujipongeza kwa ugunduzi huu.