Mizani mpya ya kupimia wanyama - Ugunduzi wa Kitanzania

Mizani mpya ya kupimia wanyama - Ugunduzi wa Kitanzania

hukumundo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2011
Posts
850
Reaction score
438
Kuna habari za kuaminika kutoka vyanzo vilivyo serikalini inayoelezea mabadiliko mazuri ambayo yako mbioni kufanyika mintarafu mizani na vipimo vya kupimia wanyama hapa nchini.
Kufuatia mafanikio makubwa ya kufaulisha watahiniwa wa kidato cha sita kwa kubadilisha viwango vya ufaulu, serikali imeagiza mizani mpya zitengenezwe ili kile kinachosomeka kama kilo moja sasa kianze kusomeka kilo mbili. Kwa njia hiyo, ng'ombe wetu atakayekuwa na uzito wa kilo 200 atasomeka ana kilo 400. Na itakuwa ni mafanikio katika ile kaulimbiu ya BIG RESULTS NOW. Halafu tutafanya sherehe kubwa nchi nzima kujipongeza kwa ugunduzi huu.
 
Weka picha mkuu. Pia bandika ushahidi wa huo mpango. Bango lake lipo pale magogoni.
 
ila kwel,ndo BRN kizazi cha maboya kila kitu ni mwendo wa ku duplicate tu ,na kama imeweza kuwapa wa kidato cha nne na sita makisi za bure itashindwa huo mzani!
 
Huku kwetu kuna msemo "nyani wanaucheka msitu ukiungua" jioni wanajikuta hawana pa kulala! Wewe jichekeshe tu na mwakani wapigie kura watawale tena kwa miaka mitano na siku ukiumwa ukawakuta hao "waliopimwa kwa mizani ya kisasa" ndio wanatibu hapo ndio utacheka "practically!"
 
Back
Top Bottom