Mizani ya maisha, kila mtu ana umuhimu

Mizani ya maisha, kila mtu ana umuhimu

Joined
Jul 21, 2022
Posts
29
Reaction score
163
Habari zenu wapendwa! Nachukua wasaha huu kuwashirikisha mtazamo wangu nakupenda kusikia kutoka kwenu Kuhusu Maisha.

Nimekuwa najiuliza hivi kama ningejikuta duniani Niko peke yangu tu. Ningeishije, je ningetamani kuendelea kuishi hivyo mpweke?

Hili swali ni gumu sana lkn maisha yanakuwa na Radha kwa sababu ya utofauti tulionao sisi binadanu. Mfano mzuri ni huu; Leo hii tusingewatambua matajiri kama wasingekuwepo maskini , kumbe heshima ya tajiri inaletwa na maskini. lkn pia kwenye upande wa elimu tunamtambua mtu wa kwanza kama asingekuwepo na yule mwanafunzi wa mwisho. kwa hiyo mabest student wote heshima yao inatokana na wale wanafunzi wa mwisho.

Mfano mwingine ni wa viongozi ambao wanapata heshima kutokana na wafuasi wao. Na hao wafuasi wanaweza kuwa ( wananchi, waumini n.k) kwa hiyo haya maisha yana MIZANI mingi sana. Ili tuishi vyema lazima tutambue "KILA MTU NI MUHIMU KWENYE NAFASI YAKE" na sote pia tunategemeana na ndio maana tunaishi kama jumuiya. Kila mtu akizingatia hili tutakuwa watu wema , wenye utu na tusiokuwa na matabaka.
 
Neno zuri Head Girl. Kikubwa tuheshimiane tu na tuishi kwa amani na upendo.
 
Back
Top Bottom