Takwimu nyingi sana zimefanyika kuonesha idadi ya wasomi wenye sifa za kupata ajira zimeongezeka kwa kasi kubwa sana mwaka hadi mwaka na hii imepelekea awsomi kuwa wengi sana mitaani huku idadi ya wanaopata ajira za kudumu au za muda mfupi katika serikali kuwa ni chache kulingana na idadi ya wasomi walioko mtaani bila ajira au wengine wenye nafasi wamejiajili wenyewe kwa kufanya ujasiriamali, na wengine wamepata nafasi katika kampuni na mashirika tofauti tofauti yasiyokua ya kiserikali.
Serikali inajitahidi kutoa ajira mbalimbali kwa awamu tofauti kama ajira za afya, elimu, sayansi na teknolojia, ugavi na manunuzi, utalii, uhandisi na nyininezo nyingi ili kupunguza idadi kubwa ya wasomi wenye sifa za taalumu husika kukaa mtaani tu bila kua na ajira, lakini pia serikali inatoa nafasi hizo ili kuongoze tija na ufanisi katika upatikanaji bora wa huduma kwa kiwango cha hali ya utoshelezi, na kwa wakati maalumu.
Katika ajira zote zitolewazo katika vipindi vyote kumekua na vitengo viwili vya kitaaluma abavyo serikali imeviweka kua ni kipaumbele zaidi , vitengo hivyo ni afya pamoja na elimu ndio maana kila serikali inapofikilia kutoa nafasi za ajira vitengo hivi vimekua kinara sana kupewa vipaumbele kwa wanataaluma wake ukilinganisha na vitengo vingine kama utalii, uhandisi n.k.
Lakini katika mgawanyiko wa utoaji wa ajira katika vitengo hivi viwili vya afya na elimu kumekua na sintofahamu kubwa sana kwa kua kumekua na utoaji wa nafasi hizi za ajira bila kuwa na mizani ya usawa kwa wanataaluma wote, mfano serikali i nasisitiza kuwa wale wanataaluma waliojitolea ndio wapewe vipaumbele katika ajira hizi je? nafasi hizo za kujitolea zinapatikana wapi? ilihali wanataaluma wengi sana maombi yao ya kujitolea yamejaa katika taasisi za uma kama hospitali na shule ikiwa hawajui nini muafaka kwa kua majibu wanayopewa ni kwamba "kwa sasa nafasi zimejaa hatupokei wanaojitolea labda jaribu wakati mwingine".
Pale ambapo serikali itatoa nafasi za ajira katika vitengo mbalimbali ni mapendekezo yangu kua ilio kuleta usawa na haki na ili kurudisha imani katika ajira hizi mpya zinazotolewea na serikali mambo yafuatayo yapuuzwe kabsa na yasipewe nafasi kwani yanawapa kundi la watu wachache nafasi na kuwanyima kundi kubwa la wanataaluma nafasi ya kupata ajira ambazo wanastahili kabisa, mambo hayo ni kama

- kutolewa kipengele cha recommendation letter(barua ya mapenekezo), kipengele hiki kinamtaka muombaji wa ajira aliyejitolea katika kitengo flani apendekezwe na kiongozi msimamizi wa eneo lile ili kupewa ajira. kipengele hiki ni cha kibaguzi sana kwani kinachochea utoaji wa rushwa na kinachochea kuwakandamizi watu ambao hawakupewa fursa ya kujitolea .mfano, luna mwanataaluma flani amemaliza chuo akkamua kufungua genge lake la nyany , vitunguu , mchicha na n.k huku akisubiri ajira zitoke aombe 'je? unapomuomba barua ya kpendekezwa ataitoa wap huyu?, si ndio itakua haki yake ya kupata ajira imekandamizwa kwa kigezo cha barua moja tu?.
- kutolewa kipengele cha uzoefu(experience), katika mfumo wa maombi ya ajira za serikali yale ya kielektroniki na yasiokua ya kielekroniki kumekua na hiki kipengele kinacho wataka waombaji wa taaluma kuambatanisha nakala za vyeti vinavyoonesha anauzoefu wa miaka mingapi katika sekta hio na ukizingatia katika mfumo wa elimu uliopo hatuna chuo cha kufundisha uzoefu baada ya kuhittimu mafunzo ya taaluma husika.na bahati mbaya sana hata katika ajira za uma kipengele hiki kinazingatiwa sana ilihali ni kipengele kandamizi na hakina usawa na sio haki.
ili kuleta mabadiliko chanya na yenye tija ni lazima sekretarieti ya ajira ikae na kutafakari kwa makini mambo kama hayo ambayo yananaleta mkanganyiko ndani ya nchi na kufanya wananchi kukosa imani na ajira zitolewazo kwani wanaamini kua ajira hizo ni kwa ajili ya kundi fulani la watu wachache ambao tayari wana watu waliowatangulia kuwaandalia mazingira. Na hii hupelekea tabaka katika jamii, vijana kukosa morali na viongozi na serikali yao, vijana na wananchi kutotoa ushirikiano katika mambo ya kimaendeleo ya letwayo na serikali, machafuko kama vile maandamano, lugha chafu katika mitandao mbalimbali kwa kuwa hawalizishwi na mfumo kandamizi uliopo kwa kipindi kirefu sasa.
Upvote
0