LGE2024 Mizengo Pinda ajitokeza kwenye kampeni za CCM Mtwara. Ataka wagombea wasibweteke baada ya ushindi wa kishindo 2019

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Wakuu huyu baba alikuwa wapi siku zote? Kwani bado yupo kwenye siasa?

Mlezi wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mizengo Pinda, amewahimiza viongozi na wanachama wa chama hicho kutobweteka na mafanikio ya uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, ambapo maeneo mengi yalishinda bila kupingwa.

"Tumieni muda uliobaki vizuri kwa ajili ya kupeleka nguvu kwenye mashina na matawi ambayo ndio yanayosaidia kuongeza uelewa na kura siku ya uchaguzi na kuzidi kuimarisha chama,"


Source: Jambo TV
 
Kama ule upuuzi uliofanywa na dikteta magufuli 2019 anauita ushindi wa kishindo basi akapimwe akili
 
Reactions: IIS
Sema UCHAFUZI wa 2019..ambapo Uchafuzi huo umeendelea 2020 na 2024
 
Reactions: IIS
Kama ule upuuzi uliofanywa na dikteta magufuli 2019 anauita ushindi wa kishindo basi akapimwe akili

Mazee ya CCM huwa hayanaga haya ..... Halafu Jumapili anakaa kiti cha mbele kanisani. Anyway, tumuonee huruma, hapo yupo busy kutetea TONGE la Kijana wake.

Huyo Mzee alikuwa Mozambique kusaidia FRELIMO wizi wa kura. Damu ikimwagika huko .... atakuwa na mchango wake kwa kuhalalishisha huo uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…