Mizengo Pinda: Serikali ilivyotekeleza Maazimio ya Bunge Richmond

Mizengo Pinda: Serikali ilivyotekeleza Maazimio ya Bunge Richmond

Nasubiri kwa hamu kubwa sana sana hiyo alhamisi ifike nione "tanzania yetu"jinsi inavyopindisha mambo yaliyo wazi...dunia nzima naona ni sisi wa tz ndio tunaweza ....sidhani kama yatakuwa ya kiutendaji kama ilivyodhaniwa na inavyotakiwa..itakuwa ya kisiasa zaidii....just wait and see...for urself..
 
ndugu zanguni hakuna jipya tusiwe wapumbavu wa kuwa kujipa moyo ovyo sasa wacha tusubiri wanavyotaka kutupeleka huyu raisi na bunge lake


mtakuwa mashaidi wa hizi statement
 
Pinda to outline action on Richmond culprits

2008-08-26 10:11:45
By Juma Thomas, Dodoma


Prime Minister Mizengo Pinda is set to unveil on Thursday a report on execution of 23 House recommendations on the Richmond power generation scandal.

Speaker of the National Assembly Samwel Sitta told Parliament yesterday that Pinda would give the report a day before the budget session comes to an end.

The wananchi are eager to know what the government has done to implement the proposals.

The House Select Committee, chaired by the Kyela MP Harrison Mwakyembe, presented its findings early this year.

It implicated former prime minister Edward Lowassa, who together with two ministers? former Minister for Energy and Minerals, Nazir Karamagi and East African Co-operation minister Dr Ibrahim Msabaha? had to resign.

Mizengo Pinda replaced Lowassa in a subsequent cabinet reshuffle.

The report also suggested disciplinary measures to be taken against a number of government officers who were implicated in the scandal.

The government thereafter formed a task force to work on suggestions of the select committee early this year.

Earlier, Speaker of the National Assembly Samwel Sitta had formed the probe committee after Members of Parliament demanded to know reasons that drove the government to enter into a flawed power generation deal.

Richmond Development Corporation secured the contract in 2006 when the country experienced power shortage due to acute drought that dried up power generating dams.

SOURCE: Guardian

Comment on this article
 
Richmond: Wote hawa `out`

2008-08-26 16:46:41
Na Mwandishi wetu, Jijini


Kuna taarifa kuwa vigogo kadhaa ambao walihusishwa na sakata la mkataba `bomu` wa kufua umeme wa dharura wa Richmond, watatupwa nje ikiwa ni hatua ya kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sakata hilo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samwel Sitta alilitaarifu Bunge kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda tayari amekamilisha kazi ya kupitia ripoti ya kamati hiyo na keshokutwa atalieleza Bunge hatua zitakazochukuliwa.

Kwa mtaji huo, wale vigogo watakaomwagwa ama kuchukuliwa hatua nyingine zozote sasa watajulikana.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa, sakata hilo litakuwa kama lile lile lililopelekea aliyekuwa Waziri Mkuu,
Bw. Edward Lowassa, na mawaziri Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi kujivua madaraka . Inadaiwa kuwa hakuna atakayelindwa kwa namna yoyote.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliwasilishwa bungeni na Mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe, vigogo kadhaa wa Serikali ya awamu ya nne kutoka wizara mbalimbali walipendekezwa kuwa wanapaswa kuwajibishwa kutokana na kuhusika kwao katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya kufua umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni \'feki\' ya Richmond.

Waliopendekezwa kumwagwa ni hawa:
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Edward Hosea, ambaye anatuhumiwa kuwa taasisi yake ilipotosha ukweli wa uchunguzi dhidi ya sakata hilo na badala yake ikaifagilia kampuni ya Richmond.

Mwingine ni Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi ambaye ilipendekezwa achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambayo imesababisha hasara kubwa kwa nchi.

Wengine waliopendekezwa kuwa wanapaswa kuwajibishwa ni Kamishna wa Nishati Ndugu Bashir Mrindoko ambaye alielezwa kuwa alishindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na Wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa Bomba la Mafuta.

Pia kamati hiyo ilipendekeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia awajibishwe kwa kushindwa kuishauri vema Serikali na hatimaye kuingia kwenye mkataba huo uliolitia taifa hasara kubwa.

Mapendekezo ya kamati hiyo yalisababisha Bw. Lowassa kujiuzulu wadhifa wake, akifuatiwa na mawaziri wawili, Bw. Karamagi na Dk. Msabaha.adala ya kuwatenga, hali inayowaongezea msongo wa mawazo.

SOURCE: Alasiri

Tuma Maoni Yako
 
Bado masaa machacha kabla ya Kesho na kujua kama zipo hatua ama ataomba kuongezewa muda zaidi kwa ajili ya kufanyia kazi mapemndekezo ya Bunge.

Hivi sheria zinasemaje kama serikali isipotiii maazimio ya Bunge?
 
Bado masaa machacha kabla ya Kesho na kujua kama zipo hatua ama ataomba kuongezewa muda zaidi kwa ajili ya kufanyia kazi mapemndekezo ya Bunge.

Hivi sheria zinasemaje kama serikali isipotiii maazimio ya Bunge?

Nadhani ataomba muda kwa kuwa suala linahusu usalama wa taifa, hadi kipindi kijacho cha bunge atakuwa na maamuzi ya utekelezaji...
 
Haya jamani, tukajimwage sote kesho hapo Diamond Jubilee. Sijafurahia jinsi walivyopanga siku na mda wa tukio. Nafikiri wangepata watu wengi pamoja na michango mingi kama wangepanga tukio hili lifanyike wikiendi.

Kwa habari zaidi pata ujumbe hapa chini.

source: http://michuzijr.blogspot.com/



CUF waandaa kongamano la ukosefu wa uongozi na hatma ya Tanzania

Chama Cha Wananchi
Office of The Secretary General
P.O. Box 10979Dar Es Salaam, Tanzania
www.cuftz.infowww.hakinaumma.wordpress.blog
TAREHE: 26/08/2008

KUHUSU: KONGAMANO LA KITAIFA KUJADILI UKOSEFU WA UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA


Nchi yetu inapita katika moja ya kipindi kigumu katika historia yake tokea ilipopata Uhuru mwaka 1961. Hali ya uchumi ni ngumu sana huku gharama za maisha zikipanda kwa kasi ya ajabu chini ya falsafa ya ari, nguvu, na kasi mpya.

Tofauti za kipato na kiwango cha maisha kati ya matajiri wachache na walalahoi walio wengi inazidi kuongezeka. Migomo ya wafanyakazi na wanafunzi imekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa. Nyufa katika Muungano wetu zinazidi kukua na hata kutishia uhai wa Muungano wenyewe. Migawanyiko ya kidini inaonekana kuzidi kujikita. Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar umeshindwa kupatiwa jibu huku uchaguzi mkuu wa 2010 ukiwa unakaribia.

Serikali inaonekana kuzidiwa nguvu katika mapambano dhidi ya ufisadi na sasa mafisadi wanaonekana kutamba. Taifa linakwenda bila ya Dira wala Mwelekeo unaoeleweka. Wananchi wanaonekana kukata tamaa. Matatizo haya kwa kiasi kikubwa yanaonekana kusababishwa na ukosefu wa uongozi thabiti, makini na adilifu.

Hii si hali nzuri na tusipokuwa makini Taifa litayumba sana. Wazalendo wakweli wa Tanzania hawapaswi kukaa kimya na kusubiri matokeo ambayo kwa vyovyote vile hayawezi kuwa mazuri. The Civic United Front (Chama Cha Wananchi-CUF) kikiwa chama makini kikuu cha upinzani nchini, kinachotegemewa na Watanzania walio wengi, kimeandaa kongamano maalum kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu hali hii ya ukosefu wa uongozi na athari zake kwa hatima ya Tanzania.

Kongamano hilo litafanyika siku ya Alhamis, tarehe 28 Agosti, 2008, kuanzia saa 3.30 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, mjini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba, atawasilisha mada kuhusu UKOSEFU WA UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA na baadaye washiriki watapata nafasi ya kuichambua mada hiyo na kutoa maoni na mtazamo wao.

CUF imewaalika watu mbali mbali kushiriki katika kongamano hilo wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, wahariri na waandishi wa vyombo vya habari, taasisi za kiraia na kijamii, viongozi wa kidini, wasomi na wataalamu, maofisa wa kibalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

HAKI SAWA KWA WOTE

Mbaralah Maharagande,
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano ya Umma.
 
Lakini Uhuru ukizidi ni tabu. Tunaona kama hakuna uongozi dhabiti just kwa vile tuna freedom of speech and press. Kama tungebanwa tungetumia muda mwingi kwenye uzalishaji na kuwa na forum na blog za how to... nk na sio siasa na malumbano. Huo ni mtazamo wangu lakini every guy MUST pool up his her socks au kukaza buti.
 
Mh. Marmo, WN OWM, amewasilisha hati za taarifa ya UTEKELEZAJI wa Azimio la Bunge kuhusu Richmond. Nadhani baadaye WM ataisoma. Tusitarajie ambayo hayapo!
 
kati ya mapendekezo ya kamati ya bunge kuhusu sakata la RICHMOND ni kuwajibishwa kwa Hosea. PM anawasilisha utekelezaji wa mapendekezo leo. je Hosea katimuliwa kazi? je kama atabaki imani yetu kwa PCCB itatoka wapi? kwa unyeti wa nafasi yake katika rushwa na kutokana na yeye kuipamba rushwa badala ya kupambana nayo naona angejiuzulu mwenyewe tu hata kama serikali ikishindwa kumwajibisha.
 
Atapewa nafasi ya kujisahihisha na kujitetea!Kama mnadhani ataadhibiwa tunaota!
 
Msiumize vichwa hapa.....na msitegemee watu watasulubiwa hapa....serikalini siku zote watu wanalindana wenyewe kwa wenyewe kwa hiyo zaidi zaidi labda watakao umia hapo ni dagaa wa pale TANESCO na wizarani mapapa kama EL,Msabaha,Kanywamagi hawataguswa hata kidogo hata huyu Hosea nyie subilini hii ni kawaida kwa serikali.
 
Hakuna Jipya hapo, ikumbukwe kuwa serikali ya JK ni butu sana kulika hata ya Mzee ruksa, tusitegemee kitu chochote, na hashajua hata akifanya pumba mnaandamana kumsifia tena!!

That's true baba H, yaani siamini kama kuna mpya yoyote itatokea hapo. Time will tell...........
 
Sheria ya manunuzi ya UMMA kurekebishwa na kuimarishwa zaidi kwa kuipa nguvu za kuchukua hatua kwa wale watakaoikiuka.
 
Back
Top Bottom