Mizengwe, kundi pekee la comedy lililosalia Tanzania!

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Kikundi cha kash kash, kinajojishughulisha na shughuli za sanaa kwa kucheza ucheshi unaojulikaba kama Mizengwe ndio kikundi pekee hivi sasa kilichobakia kwenye tasnia ya ucheshi kwa kuweza kuendelea kuiburudisha jamii kupitia vichekesho vyao!

Kikundi hicho kilichojaliwa kuwa na wachekeshaji wenye vipaji akiwemo mkwere original, maringo7, safina na wengineo wameweza kutawala na kukiimarisha kikundi hiki kwa kubuni vichekesho mbalimbali ambavyo huwezi kuboreka pindi unavyotazama vichekesho vyao!

Kundi hili liwe mfano kwa makundi mengine yanayofanya sanaa kama hizo, hakika hawa jamaa wanastahili pongezi!

My take; Hawa jamaa wasije wakajiingiza au wakakubali kuhadaiwa na wanasiasa, watapotea na huo ndio utakuwa mwisho wao, watakapojiingiza kwemye masuala ya siasa hilo kundi lazima litavurugika, wasikubali kamwe kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuonyesha mrengo wao hadharani kama wanataka kuendelea kupendwa na kufanya vyema!
 
Umesahau na Futuhi
 
hahaha nawakubali sana hawa jamaa wanaelimisha na kuburudisha kabisa hawa ndio walio baki Tanzania
 
Nakubali wako vizuri na ni wabunifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…