Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itv kila juma pili saa tatu na dk 5 usiku. Au kila jumamosi marudio nadhani kuanzia saa tano asubuhi hiyo ndo MizengweTv gani na muda gani kipindi
KweliKikundi cha kash kash, kinajojishughulisha na shughuli za sanaa kwa kucheza ucheshi unaojulikaba kama Mizengwe ndio kikundi pekee hivi sasa kilichobakia kwenye tasnia ya ucheshi kwa kuweza kuendelea kuiburudisha jamii kupitia vichekesho vyao!
Kikundi hicho kilichojaliwa kuwa na wachekeshaji wenye vipaji akiwemo mkwere original, maringo7, safina na wengineo wameweza kutawala na kukiimarisha kikundi hiki kwa kubuni vichekesho mbalimbali ambavyo huwezi kuboreka pindi unavyotazama vichekesho vyao!
Kundi hili liwe mfano kwa makundi mengine yanayofanya sanaa kama hizo, hakika hawa jamaa wanastahili pongezi!
My take; Hawa jamaa wasije wakajiingiza au wakakubali kuhadaiwa na wanasiasa, watapotea na huo ndio utakuwa mwisho wao, watakapojiingiza kwemye masuala ya siasa hilo kundi lazima litavurugika, wasikubali kamwe kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuonyesha mrengo wao hadharani kama wanataka kuendelea kupendwa na kufanya vyema!
Wakiingia kwenye siasa tu, watapotea kabisa kwenye ramani ya comedy kama ndugu zao ze comedy!Yaani Mizengwe ni moto wa kuotea mbali asikudanganye mtu, wameimarika sana, wabunifu sana, wasikubali kuingizwa kwenye siasa wala kufanya colabo na makundi mengine. Natamani ningekutana walau mmojawapo au kupata mawasiliano na hao nikawapa kile kilichoko moyoni mwangu ikiwa pamoja na shukrani za dhati ila nawakubali sana
Kazi yao kunyonga mimacho na kutoa ndimi utadhani kenge kaona mzogaAcha masihara bana....Futuhi wale wanalazimisha fani ya uchekeshaji
Labda ameolewa Mzee akapiga marufuku kufanya comedy.Bi kiroboto sijui yupo wap