Mafanikio ya treni ya abiria kwa sasa kufika Dodoma yanatia moyo.
Hata hivyo ufanisi wa reli kiuchumi ni usafirishaji wa mizigo.
Muda umefika sasa kwa wizara ya uchukuzi kuanza kuratibu namna ya kuyaondoa malori barabarani.
Juhudi za kufufua Central Railway ziendane sambamba na kufufua reli ya TAZARA.
Hongera SGR kwa mwanzo mzuri.
Mimi kama mdau wa sekta ya usafirishaji kwa kutumia malori bado siioni SGR kuyatoa molori barabarani na itachukua muda sana kwa namna miundo mbinu ilivyo
Mfano Leo hii mfanya biashara amenunia ngano kwa bakhresa 30t anataka apeleke Arusha kwa Morombo
Akisema asafirishe kwa njia ya relief itamgarimu muda wake na garama kubwa sana
Atapaswa akodishe gari Toka kiwandan Hadi stesheni aipelekee treni mzigo wake alafu ikifika Arusha akodishe gari nyingine aupeleke dukani kwake
Sambamba na hilo treni haiwez kuonza safari kwa mzigo wa tan 30 analazimika kuungana na wenzake Hadi wajaze behewa nyingi Ili TRC waweze kupata faida
Tukumbuke mfanyabiadhara ni mtu wa kwenda na muda sana hapa atakua amekwama atalazimika kutafuta usafiri ambao ni WA haraka na usiokua na mambo mengine
Ukipakia mzigo dsm mchana Lori likaondoka kesho yake mchana tiyari litakua Arusha kwa mfanyabiadhara
Kwa iyo bado watu wa malori na sisi kampuni za usafirishaji tunayo nafas ya kuendelea kuwepo na kuchangia uchumi wa nchi na hata kulete ushindani mkubwa kwa SGR
NB: SADIRISHA mizigo Yako na FSF COMPANY LTD ndani na nje ya nchi
FSF NLni wamiliki wa malori na wasafirishaji wa mizigo kama vile mazao,mbolea,kontena, vyakula vya mifugo, n.k
Tunapatikana Arusha na Dar wa salaam
Wasiliana nasi 0714797079
Vitalis Ndossi - Logistics and transport manager