Mizigo na SGR: Muda umefika kuondoa malori barabarani

Mafanikio ya treni ya abiria kwa sasa kufika Dodoma yanatia moyo.

Hata hivyo ufanisi wa reli kiuchumi ni usafirishaji wa mizigo.

Muda umefika sasa kwa wizara ya uchukuzi kuanza kuratibu namna ya kuyaondoa malori barabarani.

Juhudi za kufufua Central Railway ziendane sambamba na kufufua reli ya TAZARA.

Hongera SGR kwa mwanzo mzuri.
Kabisa yanasababisha foleni na uharibifu mkubwa wa barabara
 
Sasa na sisi wa kupeleka mizigo masasi je
 
SASHA hawezi kazi ya kuondoa malori barabarani maana huko vita yake nikubwa sana. Na hii vita angeiweza JPM lakini huyu SASHA ni mlaini mno.
Watakaochukua tenda ya kusafirisha mizigo ndio hao watakaofaidi na malori yatapungua sana
Na Train zikifika mpaka DRC basi tena
Rais hawezi kuongea kwa mdomo tu bali vitendo vitaonekana
Ipo siku hata kina Bakhressa wataacha kutumia malori kubeba juice bali zitqtufikia Kigoma kwa mabehewa ya mizigo

Hakuna uchawi ila ndio biashara zinavyoenda hakuna kuhurumia kisa unafunga biashara za wengine hapana ila zote zitaenda sambamba tu kama tutazalisha bidhaa nyingi Zaidi
 
Kabisa yanasababisha foleni na uharibifu mkubwa wa barabara
Hii kauli ya kusema malory yanaharibu barabara zetu huwa naipinga vikali sana, aidha ni watu hawajatembea wakaona barabara za wenzetu zimejengwa kwa viwango gani na wingi wa magari hayo je yanalingana na ya kwetu??.

Ukweli ni kwamba barabara zetu zinajengwa chini ya viwango na wala si wingi wa magari, sisi hatuwezi kulingana idadi ya magari na nchi kama South Africa 🇿🇦 na tazama viwango vya barabara zao halafu linganisha na za kwetu.

Majirani zetu tu hapo Zambia🇿🇲, Burundi🇧🇮, Rwanda🇷🇼 na Kenya 🇰🇪 wanatuzidi viwango vya ubora wa barabara zao.
 
Mafanikio ya treni ya abiria kwa sasa kufika Dodoma yanatia moyo.

Hata hivyo ufanisi wa reli kiuchumi ni usafirishaji wa mizigo.

Muda umefika sasa kwa wizara ya uchukuzi kuanza kuratibu namna ya kuyaondoa malori barabarani.

Juhudi za kufufua Central Railway ziendane sambamba na kufufua reli ya TAZARA.

Hongera SGR kwa mwanzo mzuri.
Mabasi nani kayaondoa Barabarani?
 
Huku rushwa ya watumishi wa umma
 
Sasa hivi mabasi yamevutwa shati.

Huko ndiko kuna faida na ndiko kwenye vita nyingine kubwa sana.
Hakuna nchi inajenga reli kwa ajili ya kusafirisha abiria, hii inatokea kwetu sisi wapenda chawa tusiojali gharama za ujenzi wa reli.
 
Mwingereza alijenga reli ya Mtwara kwenda Nachingwea kwa ajili ya uchukuzi wa mkonge na karanga, hata hivyo miradi hiyo iliposhindwa kukidhi mafanikio mwingereza aliamua kuing'oa hiyo reli.
 
Sasa hivi mabasi yamevutwa shati.

Huko ndiko kuna faida na ndiko kwenye vita nyingine kubwa sana.
Vita ipi? Wakati serikali imesema ruksa mtu binafsi kuleta treni yake waingie Ubia. Hao wamiliki wa basi wanunue treni na mwendokasi maana huko kuna faida zaidi.
 
SGR gani, hii hii inayokwamishwa njiani na ngedere kwa masaa 5?
 
Mafanikio ya treni ya abiria kwa sasa kufika Dodoma yanatia moyo.

Hata hivyo ufanisi wa reli kiuchumi ni usafirishaji wa mizigo.

Muda umefika sasa kwa wizara ya uchukuzi kuanza kuratibu namna ya kuyaondoa malori barabarani.

Juhudi za kufufua Central Railway ziendane sambamba na kufufua reli ya TAZARA.

Hongera SGR kwa mwanzo mzuri.
Hilo linawezekana ila biashara za wakubwa wengi zitaathiriwa kama wenye bandari kavu walivyathiriwa na ujio wa DP World. Serikali haijashidwa kufufua na kuwa na behewa za kubeba kontena na mizigo kwa njia ya reli ila tu kinachotokea ni hujuma ili biashara zingine ziendelee kukusanya hela.
 
Back
Top Bottom