MJADALA: AI na Kesho ya Vyombo vya Habari: Fursa au Tishio?

MJADALA: AI na Kesho ya Vyombo vya Habari: Fursa au Tishio?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
706
Reaction score
1,230
mjadala.jpg

Kadiri Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inavyoendelea kukua kwa kasi katika maisha yetu ya kila siku, sekta ya Habari nayo haijaachwa nyuma. AI inabadilisha namna tunavyokusanya, kuchakata na kusambaza taarifa. Lakini je, inaathiri vipi Uhuru wa kujieleza? Inasaidia au inahatarisha Uadilifu wa Vyombo vya Habari?

Kufahamu haya usikose kushiriki katika Mjadala maalum kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, tukijadili kwa kina nafasi ya AI katika Sekta ya Habari, changamoto, fursa na wajibu wa wadau kuhakikisha matumizi yake yanakuwa ya Haki, salama na yenye kulinda misingi ya Demokrasia
1744730956957.png

Ni leo hii Jumanne, Aprili 15, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya
https://jamii.app/WPFD2025XSpace

Maoni ya Wachangiaji

TONY ALFRED (The Chanzo)


AI inaweza kusaidia katika vitu vingi, imesaidia kurahisisha kazi ambazo ingekuchukua muda mrefu kuzifanya, Mfano; kuandika hotuba unaweza kuitumia kuandika na kukusanya taarifa mbalimbaliLengo kubwa la AI ni kufikia Akili ya Binadamu kwa njia ya Mashine, hatujafika huko ila ndio inapoelekea

Imerahisisha vitu kama utengenezaji wa mdundo (Instrumental), bila yenyewe ungeweza kutumia gharama kubwa kutengeneza au kupata lakini kwa sasa kuna urahisi mkubwaChangamoto ni kwamba imesababisha mkanganyiko wa baadhi ya vitu kuwa na ugumu katika kutofautisha. Mfano picha inaweza kutengenezwa kwa AI na ikawa ngumu kutambua kama ni halisi au la.

Tuliozoea kuangalia Taarifa za Habari Saa 2 Usiku, tunatakiwa kutegemea kuona zikisomwa na AI bila kuhusisha Wasomaji Binadamu kama tulivyozoea kwa sasaAI haiwezi kufikiria ila inaweza kutabiri kutokana na aina ya taarifa inazopewa

IMANI LUVANGA (Crown Media)

Hatuna budi kuichukulia AI kama fursa, kwani kila kitu kinachokuja kina faida na changamoto zake lakini hatuwezi kuikimbia.

AI inarahisisha mambo mengi kwa Wanahabari, inasaidia kupunguza gharama ambazo zingekuwa kubwa katika Utendaji Pamoja na uwepo wa AI, kuna umuhimu wa kila Chombo cha Habari kutengeneza Sera kuhusu AI, kwa kuwa ili AI ifanye kazi inahitaji taarifa ambayo sisi ndio tunailisha

Pamoja na uzuri wa AI kuna umuhimu wa kujiandaa na changamoto zake, Mfano; Kwenye suala la Lugha inaweza kutafsiri tofauti na uhalisia, hivyo bila kuhakiki (fact check) inaweza kukupoteza na kukuondolea maana nzimaAI inatakiwa kurahisisha kazi na sio kutufanyia kila kitu, kwa kuwa tunatakiwa kuvipa uhai vitu tunavyovifanya, tusiishie katika kutegemea Mashine

Ukisoma Sera za IA zinakwambia zenyewe hazipo sahihi kwa Asilimia 100, hivyo Waswahili wanasema "za Kuambiwa Changanya na zako"AI haitakiwi kukufanya uwe mvivu, ukiwa mvivu hiyo ni tabia yako, AI inatakiwa kuwa kama sehemu ya kukuongoza na kukurahisishia kazi yako

AI inatakiwa kuwa sehemu ya kukushauri, kisha wewe unaangalia kama inaendana na Sera ya Chombo chako cha Habari au mazingira yako.

Ukiendekeza uvivu kwa sababu ya matumizi ya AI ipo siku itakuaibisha, inaweza isiwe leo au kesho lakini itakapokuaibisha inaweza kuwa na madhara makubwaTusijifiche katika AI kuwa inatufanya kuwa wavivu, ukiona mtu wa hivyo ujue alikuwa mvivu siku zote ila anatumia tu AI kama kisingizio

NUZULACK DAUSEN (Nukta Africa)

Uandishi wa Habari wa Takwimu na Uandishi mwingine kuna msaada mkubwa kutoka kwa AI, kwa kuwa hata kama hauna uzoefu mkubwa, inakurahisishia kupata na kuelewa takwimu mbalimbaliWanahabari ambao wanaogopa kufanya uchambuzi wa takwimu wanapata msaada mkubwa kutoka kwa AI katika kuchakata namba.

AI inasaidia kupatikana kwa maamuzi mengi ndani ya Vyombo vya Habari, kwa kuwa inaweza kukuonesha kwa aina ya taarifa yako kukueleza Watu wanatumia muda gani kusoma taarifa fulaniHiyo inasaidia kupata uhakika wa kujua uandae taarifa za aina gani na kujua tabia za wateja au walaji wako

Pamoja na uwepo au matumizi ya AI tunatakiwa kuwa makini katika kuhakiki, kwa kuwa kwa Sheria zetu huwezi kusema ulisaidiwa na AI Sheria zetu zinawafuata Waandishi na Chombo pia, hivyo umakini mkubwa unatakiwa kuhakiki.

Tools nyingi za AI zinakupa taarifa kuwa zinaweza kufanya makosa wakati unapotumia, mfano majina ya watu au Jinsia Picha au Video ambazo zimeandaliwa na AI mara nyingi huwa zinakuwa na kasoro ndogondogo mfano vidole, nguo n.k

NUZULACK DAUSEN (Nukta Africa): Wakati Watu wanapoteza kazi kutokana na AI kuna watu wanapata kazi kutokana na uwepo wa AI Mfano; Miaka kadhaa nyuma kulikuwa na Karani ambaye Teknolojia ilipoingia majukumu yake yalibadilika na inawezekana alipoteza kazi, kisha Mtu mwingine akapata kazi kuratibu Teknolojia husika

ISACK NYAIMAGA (Mdau)

Ukuaji wa AI unachangia ukuaji wa sekta mbalimbali kuanzia uandishi, Ubunifu wa michoro sanifu n.k Jamii inapaswa kuhakiki taarifa wanazopata huko kabla ya kuziweka Mtandaoni na pia kuwa na tahadhari kwa taarifa tunazoipa AI, ili kuepuka Kuweka data nyeti

KENNETH SIMBAYA (Mkurugenzi Mtendaji UTPC)

Teknolojia inapokuja inakuja pamoja na fursa nyingi, hivyo ni jukumu lako wewe mtumiaji kutambua umuhimu na jinsi ya kuitumiaMara nyingi Teknolojia inapokuja kama ilivyo AI, Watu wamekuwa wakitaka kuitumia bila kufanya utafiti wa matumizi sahihi ya Teknolojia husika

ESAU EZRA NG'UMBI (Mdau)

Kuna Watu wana dhana ya zamani kuwa ili uwe bora lazima utumie nguvu kubwa kufanya jambo au utumie muda mwingi kufanya kazi fulaniMaendeleo ya Teknolojia kama ilivyo kwa AI yanakuja ili kurahisisha na kuondoa dhana hiyo, haina haja ya kutumia Akili, nguvu na muda mwingiAI ni kifaa kinachotakiwa kutambua matumizi bora ambayo wewe unatakiwa kutambua jinsi ya kutumia

GEORGE HELAHELA (Mdau)

Kuna Waandishi ambao hawana Elimu kuhusu matumizi ya AI, lakini haohao ndio ambao wanaitumia, je matumizi yao yanawafanya kupata taarifa sahihi?Nadhani kuna umuhimu wa Mamlaka kuwekeza nguvu kuhusu Matumizi sahihi ya AI kwa Wanahabari ambao ndio wanaoilisha JamiiKuna haja ya kuongoza mafunzo kwa Wanahabari kuhusu AI, kwa kuwa wanapokosea wao inamaanisha Jamii nzima inalishwa kitu ambacho sio sahihi na hilo ni jambo la hatari

EUGENE KABENDERA (Mdau)

AI ni fursa lakini ni tishio pia kwa Wanahabari, hiyo itategemea na aina ya matumizi ya mtu au watu husikaNchi nyingi za Dunia ya Tatu matumizi ya AI ni tishio kwa aina fulani, kwa kuwa kuna taarifa nyingi ambazo AI imelishwa hazina uhalisia wa kwetu, kuna watu wengi wa nchi tofauti wanalisha taarifa za kwetu ambazo zinaweza zisiwe na uhalisia
 
wahariri wanaweza kutumia AI kuwezesha au kuboresha kazi zao, lakini akili ya kibinadamu inasalia kuwa kiini cha uzalishaji wote wa uhariri Hakuna maudhui yatakayochapishwa bila usimamizi wa awali wa binadamu." Ili kutoa uwazi kwa wasomaji, kila nakala itaendelea "kusainiwa" na angalau mwandishi wa habari mmoja "ambao wanabaki kuwa wadhamini wa ukweli na umuhimu wa habari iliyomo.
 

Kadiri Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inavyoendelea kukua kwa kasi katika maisha yetu ya kila siku, sekta ya Habari nayo haijaachwa nyuma. AI inabadilisha namna tunavyokusanya, kuchakata na kusambaza taarifa. Lakini je, inaathiri vipi Uhuru wa kujieleza? Inasaidia au inahatarisha Uadilifu wa Vyombo vya Habari?

Kufahamu haya usikose kushiriki katika Mjadala maalum kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, tukijadili kwa kina nafasi ya AI katika Sekta ya Habari, changamoto, fursa na wajibu wa wadau kuhakikisha matumizi yake yanakuwa ya Haki, salama na yenye kulinda misingi ya Demokrasia

Ni leo hii Jumanne, Aprili 15, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya
https://jamii.app/WPFD2025XSpace
Waandidh wasiohope AI, bali watumie kama chombo cha kuboresha habari zao, kuhakiki na kuboresha machapisho yao
 
Moja Kati ya Faida Zitokanazo Na Matumizi ya Ai Kwenye Uandishi Wa Habari ni hasa Kufanya Kazi za Uchunguzi Ambapo . AI inaweza kuhariri kazi zinazojirudia kama vile kuingiza data, unukuzi, na hata uandishi wa makala za habari moja kwa moja. Hii inaruhusu wanahabari kuzingatia zaidi kazi ngumu kama vile kuripoti uchunguzi na uchambuzi wa kina.
 
Moja Kati ya Faida Zitokanazo Na Matumizi ya Ai Kwenye Uandishi Wa Habari ni hasa Kufanya Kazi za Uchunguzi Ambapo . AI inaweza kuhariri kazi zinazojirudia kama vile kuingiza data, unukuzi, na hata uandishi wa makala za habari moja kwa moja. Hii inaruhusu wanahabari kuzingatia zaidi kazi ngumu kama vile kuripoti uchunguzi na uchambuzi wa kina.
Nakubaliana na wewe mkuu iwapo waandishi wa habari watatumia vizuri akili mnemba basi inaweza kuwapa wao nafasi nzuri ya kuziboresha kazi zao na kuwa za kuvutia zaidi na kuondokana na mtazamo wa kuwa teknolojia hii inakuja kuchukua kazi za watu.

Shida ni pale jamii pia inapoiogopa teknolojia na kuona kwamba ni tishio kwao ama wanaotumia AI basi ni wavivu wa kufikiri nk
 
Waandidh wasiohope AI, bali watumie kama chombo cha kuboresha habari zao, kuhakiki na kuboresha machapisho yao
Shida wanaiogopa hata kuitaja tu kwani wanajihisi wataonekana ni wavivu wa kufikiria ndiyo maana wanatuia AI, wakati unaweza kuandaa kazi yako vizuri kisha ukatumia AI kuiboresha
 
Back
Top Bottom