Mjadala: Haki ya kutoa maelezo Polisi

Mjadala: Haki ya kutoa maelezo Polisi

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,472
KWA WALE WANASHERIA<

Tunajua CPA section 50 mpaka 58 inatoa namna interrogation inavyotakiwa kufanyika kama ukikamatwa. Kwa uelewa wangu nilikuwa najua kuwa, mtu kuandikwa maelezo ya onyo (cautioned statements) kama yale anayofanyiwa Gwajima, anatakiwa kuyatoa kwa hiari yake bila kulazimishwa, that means akiamua anaweza kukataa kuyatoa na kuwaambia polisi mimi sitaongea hapa kama mnaona nina kosa nipelekeni mahakamani nitaenda kujitetea mahakamani. Hebu tujaribu kuijadili haki hiyo kama niko sawa au siko sawa.

Kwa kifupi ni kwamba, wewe mtuhumiwa ukiamua kuwapa nafasi polisi wakupeleleze, yaani yale utakayowaeleza ndiyo hayo watayatumia kukupelelez ana kukupekua zaidi, watakumaliza kabisa kabisa. hivyo dawa yake ni kunyamaza tu usiwaeleze chochote.

Ukianza kuwaeleza kuwa una account, una kampuni, una kanisa, una nini sijui ujue baadaye wanaenda kufuatilia hadi biashara zako kama umekosea ili wakuongeze makosa, account yako ina nini wataifuatilia kila kitu watakupekenyua hadi uchoke.
 
kuna marekebisho inafika hadi 58.

huwezi kupelekwa mahakani bila kuhojiwa na polisi au na mlinzi wa amani. hivyo hilo huwezi kukwepa
 
kuna marekebisho inafika hadi 58.

huwezi kupelekwa mahakani bila kuhojiwa na polisi au na mlinzi wa amani. hivyo hilo huwezi kukwepa
weka na vifungu mzee vya sheria vinavyosema hivyo sisi wengine tunataka tujifunze pia. ni sheria ipi inasema huwezi kupelekwa mahakamani bila kuhojiwa na polisi au mlinzi wa amani?
 
weka na vifungu mzee vya sheria vinavyosema hivyo sisi wengine tunataka tujifunze pia. ni sheria ipi inasema huwezi kupelekwa mahakamani bila kuhojiwa na polisi au mlinzi wa amani?

Huwezi kataa kuhojiwa, labda kama kuna haki zako zinakiukwa. na haki mojawapo ni uwepo wa mwanasheria wako
 
Huwezi kataa kuhojiwa, labda kama kuna haki zako zinakiukwa. na haki mojawapo ni uwepo wa mwanasheria wako
unaweza kukataa kuhojiwa, na wao wataandika amekataa kuhojiwa amesema atajieleza mahakamani. kwani ukikataa watakufanya nini? imagine kama umegoma kutoa maelezo watakufanya nini? wakikupiga ndio sababu nzuri tena wakati huo umeshaita na mwanasheria wako na ndugu wako pale halafu unawaambia polisi kuwa nitatoa maelezo yangu mahakamani, hapa sitaki kutoa maelezo.watakufanya nini?

ni sheria gani inalazimisha utoe maelezo?

kwa wale ambao zamani walishapitia polisi au attorney general, lazima walishawahi kuona cautioned statement nyingi tu mshitakiwa amekataa kutoa maelezo, na polisi ameandika kuwa 'amekataa kutoa maelezo amesema atatoa mahakamani" basi. watakufanya nini ukikataa?
 
Huwezi kataa kuhojiwa, labda kama kuna haki zako zinakiukwa. na haki mojawapo ni uwepo wa mwanasheria wako
mzee wewe ni polisi? ndivyo mnavyowadanganya watu hivyo? weka vifungu vya sheria basi tuvisome.
 
kuna marekebisho inafika hadi 58.

huwezi kupelekwa mahakani bila kuhojiwa na polisi au na mlinzi wa amani. hivyo hilo huwezi kukwepa

Vifungu vinavyohusika kuchukua maelezo ni vifuatavyo, 9,10, 50,57 na 58 vya CPA. Ni lazima mtuhumiwa akubali kutoa hayo maelezo kwani ana uwezo wa kukataa kusema chochote mpaka mbele ya hakimu. Hayakichukuliwa kwa nguvu yakifika mahakamani mtuhumiwa atayakaa chini ya kifungu cha 27 cha sheria ya ushahidi. Ila kwa kesi kubwa mtuhumiwa anabananishwa mpaka aseme yote, ukigoma chupa na pliers zitakufanya useme hata ya uongo.
 
si ndo maana nimesema huwezi kataa kusema wakakukubalia eti wakupeleke mahakamani bila maelezo. haiwezekani. zipo mbinu nyingi za kutoa maelezo, hadi za kutumia walinzi wa amani yaani mahakimu. utasema tu
 
hizo ni kesi kubwa kama za mauaji na ujambazi. lakini kwa kesi ya gwajima kumtukana pengo unafikiri wangefika huko? mwanasheria wake nafikiri atakuwa amejifunza kitu siku nyingine asiache mteja wake kuanikwa hivi, ukifungua mlango mmoja kwa polisi wanaongeza kosa lingine. angalia alienda pale kwaajili ya kumtukana pengo sasaivi wanataka kusachi na nyumba yake, kwa tuhuma ipi nyingine? ukifika pale si wanakwambia tuhuma yako na kuwa upo kwaajili ya kutoa maelezo kutokana na tuhuma hiyo? sasa kusachi nyumba na kanisa na kuleta hizo nyaraka ni kwa tuhuma ipi? hiyohiyo? mbona irrelevant kabisa?
 
si ndo maana nimesema huwezi kataa kusema wakakukubalia eti wakupeleke mahakamani bila maelezo. haiwezekani. zipo mbinu nyingi za kutoa maelezo, hadi za kutumia walinzi wa amani yaani mahakimu. utasema tu
ukiena kwa mlinzi wa amani kutoa extra-judicial statement procedure inayotumika ni ileile, ipo chief justice manual ambayo pia kula ukimwambia justice of the peace kuwa hautoi maelezo anaandika tu kuwa umekataa basi. habari imeishia hapo. ila labda ungeniambia wanaweza ukirudi polisi wakakutesa kwa kukuingiza chupa kwenye tigo na kukupiga kukulazimisha, lakini hata polisi nao ni wanadamu watafanya hivyo kwa makosa yale makubwa kama ya mauaji, ujambazi etc ila haya ya kubadilishana matusi na pengo unafikiri wangefika huko? hata hivyo polisi wanatia aibu kwasababu wameenda mbali sana hadi i meonekana wazi kuwa either:-

1. kuna kiongozi mmoja juu analazimisha issue iendelee hadi wammalize

2. polisi walikuwa wanammendea kwa muda mrefu

3. wameona gwajima ana mwelekeo wa upinzani na serikali

itafika kipindi hao viiongozi tutawataja humu ndani.
 
si ndo maana nimesema huwezi kataa kusema wakakukubalia eti wakupeleke mahakamani bila maelezo. haiwezekani. zipo mbinu nyingi za kutoa maelezo, hadi za kutumia walinzi wa amani yaani mahakimu. utasema tu

Mimi huwa nadeal na haya masuala daily kupelekwa mahakamani bila statement ipo na ni kawaida . Ila kwa kesi kubwa kuna mambo ambayo polisi wanalazimisha kutoa statement. Kwa mlinzi wa amani ambaye mara nyingi ni hakimu hakuna kupigwa na ni lazima mtuhumiwa amwambie hakimu kuwa jambo ambalo anataka kulisema. Hakimu humwangalia mwilini kama ana majeraha au la ndio anaanza kuchukua maelezo. Polisi wanachokifanya ni kumpiga biti kuwa amwambie hakimu kile kile alichosema akiwa polisi.
 
Hute;

Mkuu pengine ulitaka kusema chief Justice Rules na siyo manual. Mtu kuhojia polisi kwa kosa moja hawaizuii polisi kupeleleza kosa lingine lililopatikana kutokana na maelezo unayotoa.

Kuulizia mali alizonazo ni kuangalia isije ikawa anajihusisha na money laundering ie utakatishaji wa pesa.Kumbuka kuna wakati baadhi ya maaskofu walihusishwa na biashara za unga. Kikubwa ngoja apeleke vielelezo afu tusikie
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pengine ulitaka kusema chief Justice Rules na siyo manual. Mtu kuhojia polisi kwa kosa moja hawaizuii polisi kupeleleza kosa lingine lililopatikana kutokana na maelezo unayotoa. Kuulizia mali alizonazo ni kuangalia isije ikawa anajihusisha na money laundering ie utakatishaji wa pesa.Kumbuka kuna wakati baadhi ya maaskofu walihusishwa na biashara za unga. Kikubwa ngoja apeleke vielelezo afu tusikie
angalia ndugu. mtuhumiwa anakuja kwako wewe kama polisi, unamwambia aisee gwajima upo hapa kwaajili ya kutoa maelezo kutokana na kosa ........, unaanza kumpa haki zake kama una haki ya kuita ndugu wakili au rafiki wawepo wakati wa ktuoa maelezo. hivyo hivyo haulazimishwi kwa namna yeyote ile kutoa maelezo haya bwana gwajima, na ukiyatoa yanaweza kutumika mahakamani kama ushahidi dhidi yako.

hapo sasa gwajima alitakiwa kusema kuwa, kwasababu mimi silazimishwi, basi mimi sitoi maelezo nitaenda kujieleza kulekule mahakamani wakati wa defence yangu. hiyo manual aliyotoa chief justice (or rules whatever you call it), ambayo mahakimi wa mahakama za mwanzo au justice of the peace yeyote yule anaitumia, procedure yake ni kama ileile tu ya kwenye cautioned statement kuanzia pale suspect anapokabidhiwa kwa JP polisi anatakiwa kuondoka awaache wawili tu, na voluntariness na correctiness ya uchukuaji wa confession statement vyote vinafanana. sasa, kama angekataa tangu mwanzo, hayo maelezo yaliyozaa vitu vingine yangetokea wapi?

na kama umwmwita mtu kwa kosa la kumtukana pengo na umemweleza tuhuma yake kabla ya kuanza kuchukua maelezo, hiyo tuhuma nyingine umemweleza saa ngapi itakayohusiana na money laundering? amesafisha pesa kwa tuhuma ya kumtukana pengo?

na kama kuna tuhuma ya kuuza unga, na wewe unataka kuona kama labda chopa amenunua kwa pesa za unga ungemwambia tuhuma yake tena, kwamba sasa tunabadilisha tuhuma au kuna tuhuma nyingine unatuhumiwa yano ambayo ni kuuza unga, tunataka kuchukua maelezo yako kutokana na tuhuma hiyo ya unga....ndio hayo mambo ya utakatishaji wa fedha, au kuangalia account za kufreeze etc vingekuja. ninyi mmemwita pale kwa tuhuma ya kutukana pengo na hakuna tuhuma nyingine mmemwambia kuwa anatuhumiwa nayo halafu unaingiza mambo ya money laundering hivi una akili timamu? na kama wewe ni polisi no wonder kesi huwa hazishindi kwasababu nahisi polisi wengi wakiwa na uelewa kama wa kwako utaweza kupeleleza kesi na ikafika mahakamani mkatushinda kweli?

maelezo tu hayo si ajabu hayajaandikwa kwa kufuata sheria yamepita masaa 4 baada ya kukamatwa...hahaaha.
 
Hute;

Kwa bahati nzuri mimi siyo polisi lakini hoja zako ziko too theoretical na kama hauna experience yoyote ya namna mashahidi wanavyohojiwa. Najua ungekuwa wakili ungekuwa una picha kidogo ya zoezi zilivyo. Kwa hiyo style unayofikiria wewe hata mwizi wa kuku humpati.
 
sasa kama wewe sio polisi, na sio mwanasheria, unaongea kutoka wapi? unajua nini? kwa kifupi ni kwamba, miaka kadhaa iliyopita kabla sijawa wakili wa kujitegemea nilikuwa wakili wa serikali, hizo cautioned statements na extra-judicial nimetender sana, na nimeshashiriki mara nyingi sana kwenye interrogation ya suspects kwa kuwaongoza mapolisi katika operation kadhaa. sijui kama unaongea kwa experience au umesikia tu kwa mtu.ninajua namna mashahidi wanavyohojiwa, ninajua wajibu wa polisi na haki za suspect. watu wengi sana kama wewe hawajui hilo, na wengine ni polisi hawajui hilo. ukisema theory unakuwa haujui unachoongea kwasababu hivyo nilivyokueleza ndivyo hata polisi aliyeandika cautioned statement ndivyo anavyotakiwa kuviingiza wakati wa kutender statement mahakamani as a confession ya accused. inawezekana haujawahi kufika mahakamani au pengine huwa unaenda lakini haujui kinachoendelea.
 
Mimi huwa nadeal na haya masuala daily kupelekwa mahakamani bila statement ipo na ni kawaida . Ila kwa kesi kubwa kuna mambo ambayo polisi wanalazimisha kutoa statement. Kwa mlinzi wa amani ambaye mara nyingi ni hakimu hakuna kupigwa na ni lazima mtuhumiwa amwambie hakimu kuwa jambo ambalo anataka kulisema. Hakimu humwangalia mwilini kama ana majeraha au la ndio anaanza kuchukua maelezo. Polisi wanachokifanya ni kumpiga biti kuwa amwambie hakimu kile kile alichosema akiwa polisi.
kuna jamaa hapa anasema sisi hatuna experience yeye ndio anayo hiyo experience na anajua kuwa mtu hawezi kupelekwa mahakamani bila kuandikwa maelezo. huyo jamaa atakuwa wale polisi wanaotumia nguvu lakini upstairs ni empty, ndio hao waliokuwa wananiharibia sana kesi kwa kupeleleza kesi vibaya, kuhoji mashahidi nje ya muda na kwa cautioned statement ambazo haziwezi kuingizwa mahakamani. kama ulishawahi kudeal na hii kitu utakubaliana na mimi kuwa polisi wa aina ya huyo jamaa ndio mara nyingi husababisha wahalifu kutofungwa kwa sababu wanaharibu kesi bila hata haijafika mahakamani.

haelewi maana ya "voluntariness" wakati wa kuchukua confession statement, haelewi kabisa. kama unafikiri mimi niko free kutoa maelezo, hiyo haimaanishi tu kwamba wakiwepo ndugu jamaa rafiki au wakili ndio lazima nitakuwa free, its beyond that...hata hao wakili, ndugu jamaa au rafiki wakiwepo bado polisi anayechukua maelezo atanieleza kuwa unao uhuru kutoa maelezo haulazimishwi, that means unaweza kukubali au kukataa, na ukikataa unawaambia tu kwamba nitajitetea mahakamani ninyi nipelekeni tu mahakamani nitajieleza huko. kuna kifungu gani cha sheria kimeeleza kuwa suspect akigoma kutoa maelezo hawezi kupelekwa mahakamani?kwani essence ya kuchukua maelezo ni nini? na je, confession zote huwa zinapokelewa?
 
Hute;

Nilieleza vizuri pengine ni kukimbilia kucomment kabla hujasoma. Nilisema kuwa huwa nadeal na hizi issue daily kusema vile haiimanishi kuwa mimi ni polisi I a pure lawyer. Hizo statements mawakili huwa wanadeal nazo na pia mahakimu huwa wanadeal nazo.Kwa nini hukuweza kufikiri naweza kuwa wakili au hakimu! Hapo ni shida ya kufikiria vizuri. Na pia kwenye baadhi ya kesi hata uwepo wa wakili unaweza usaidie kidogo tu, hivi hujiulizi wakili maaarufu kama yule Mwale wa Arusha akijua vifungu hivyo bado alilazimika kutoa statement! Acha kuongelea sheria za kwenye tamthilia.
 
Last edited by a moderator:
Hute;

Aliyekuambia mimi siyo mwanasheria ni nani? Hii hoja umeitoa wapi? Ni vizuri uliacha kazi kwa sababu mawakili hawa wasieweza kuelewa hata vitu vidogo ndio mnaosababisha serikali kupoteza kesi kila siku. So far chambers ilikuwa na wakili mmoja ndio aliyekuwa anafahamika ambaye ni Bonifasi Stanislaus Makulilo .Wewe ulikotokea hukuwa lolote au chochote na wala usifikiri kujitangaza wakili ni sababu ya kuzipa nguvu hoja zisizokuwa na mashiko. Wengine ni very senior members wa TLS.
 
Last edited by a moderator:
Hute;

Na zaidi hakuna operation ya polisi iliyoleta mafanikio mazuri ndio badala ya operations za polisi sasa wameamua kutumia task force.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom