MJADALA: Je, kuna madhara yoyote ya kufanya mapenzi wakati wa hedhi?

MJADALA: Je, kuna madhara yoyote ya kufanya mapenzi wakati wa hedhi?

Hata kende hupata madhara, huvimba na kuuma sana kiasi ya kushindwa kukaa ama kutembea. Hii utokea siku chache baada ya tendo.
Ofcz ni kweli ishawahi ntokea mi binafsi ziliuma sana na moja ilivimba zaidi ni baada ya siku mbili tendo kufanyika at.
 
MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA HEDHI.

Kufanya mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana (hedhi) ni hatari sana.

Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.

Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajali sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hilo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa kizazi hiki.

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati mwanamke yupo katika siku zake {period}.

MADHARA KWA MWANAUME:

- Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

- Maambukizi katika tezi dume (Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

-Kuziba kwa njia ya mkojo.

-Utasa au ugumba.

-Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

-Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji, utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.

Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata ufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.

MADHARA KWA MWANAMKE:

- Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID (PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

- Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

- Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

- Utasa au Ugumba.

- Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

- Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe/mpenzi wake hamjali wala hampendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.

Pia kuona kuwa mumewe/mpenzi hajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume/mpenzi anataka tendo.

Jali afya ya mwenza wako na yako pia, vumilia acha hedhi ipite zuia hisia zako za kingono, tengeneza msisimko wakati wa tendo bila madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wa kula tunda kimasihara ina maana hamjawahi kukutana kabisa na hii kitu kwenyw harakati zenu?
 
Hapa vipi,

Wadau pole na pilika za hapa na pale. Binafsi hili tatizo limenikuta, nilikuwa mbishi kumuelewa Mtoto wa watu.

Sasa najua kuna watu wanauelewa juu ya hili ningeomba nimepata elimu juu ya hili kwa faida ya Wanaume wabishi kama mimi.

Ila ukitumia na Condom madhara yatakupata.

Msaada
 
Na wewe kua mvumilivu basi.unashindwa kusubiri vijisiku vichache tu.
 
usihofu wasiwasi wako ndo utakufanya upatwe na ugonjwa mimi mbona nishafanya mara kibao tu bila tatizo lolote ila kuna harufu mbaya sana
 
Be specific, siku zote mwanamke yupo kwenye siku zake.. hakuna siku atasema leo siku zangu nimeziacha yuko yeye kama yeye bila siku,
But, siku zinatofautiana.

Unaongela siku zipi?
 
Be specific, siku zote mwanamke yupo kwenye siku zake.. hakuna siku atasema leo siku zangu nimeziacha yuko yeye kama yeye bila siku,
But, siku zinatofautiana..
Unaongela siku zipi?
Surya, kweli haujamwelewa?
 
usihofu wasiwasi wako ndo utakufanya upatwe na ugonjwa mimi mbona nishafanya mara kibao tu bila tatizo lolote ila kuna harufu mbaya sana
Una roho ngumu sana wewe,unafaa kuosha hata vidonda vinavyonuka sana.
 
Ngoja nikueleze Jambo,

Mwanamke Kama huifahamu dhahiri afya yake mtumie kwa tafadhali na Kinga.

Mwanamke Kama unamfamu dhahiri afya yake mtumie akiwa msafi.

Mwanamke damu iko nje unataka uingie😲😲😲😲 we huogopi bwana.

Ishu za magonjwa yanayohusu blood contact watu bado hamuyajui!? .
 
Back
Top Bottom