Mjadala: Je, ni kwanini gari hupoteza nguvu? Je, unawezaje kutatua tatizo hili?

Tafuta fundi acheki sensa nilishakutana ugonjwa hu kwenye suzuki v6 nilipoteza zaidi ya milioni 1 badae ikaja kugundulika ni sensa nikatibu kwa sh120000 unaweza ukakuta ghafla inapoteza nguvu na ikirudi kama inastuka kuwa makini sana unapoiendesha
Kaka nimepata tatizo Kama lako kwenye suzuki swift nimebadilisha pump, coil lakini bado tatizo lipo
Ulikuta sensor gani imekufa
 
Kwenye gari hasa Nissan ikikosa nguvu unasikia kama imezibwa pumzi shida inakuaga kuziba kwa Exhaust Masega unaweza kubadilisha sensor zote usipokua makini na tatizo likabaki pale pale na hata ukipima inaweza isishtakie hiyo shida ya kuziba exhaust Masega mpaka umpate fundi makini wa kuskilizia gari
 
1. Je inapoanza kosa nguvu taa ya Overdrive inakuwa ina blink au hai blink?

2. Inawezekana sensor moja chini ya gari inapata maji.inabidi isafishwe na kama imekufa ibadilishwe. Nina fundi anaweza kukusaidia.ni wa umeme na gearbox pia.
Mkuu huyo fundi wa gearbox bado anapatikana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…