Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mkuuu rudi moja hiyo oil utaipata wapi na inaitwaje hii itasaidia kwa wale wanaotaka kununua na hata walionazo naomba uje tena utuambie
Imeandikwa kwenye stick yake. Inapatikana sana.
 
Ukiweza kulivumilia xtrail kwa gharama za kui-maintain hata bombadier utaweza kuimiliki
 
Wacheni kuwadanganya na kuwatisha watu, Nissan xtrail ni gari nzuri sana kama zilivyogari nyingine ikiwa utaitunza vizuri, kila kitu kinataka matunzo, hata mke au mume usipojitunza au kutunzwa utachakaa tu. Mimi ninayo Xtrail na sijawahi kusumbuka kwa chochote, na kwa safari za mikoani ndio utaifurahia inavyotulia barabarani.
 
Voxy na Noah model inayofanana na Voxy sio gari zile. Chukua Exurb Noah, hujajutia pesa yako.
 
Spea original zipo mkuu, labda huku pats fundi mzuri. Na ni gari ambazo ukifunga spea original unafuta namba ya simu ya fundi, sababu hautamuhitaji tena kwa siku za karibuni
Uko sahihi kabisa, gari za Nissan haziharibiki hovyo na hiyo inaweza kuwa moja ya sababu kwanini spea zake original kupatikana ni ngumu kwa sababu ya wauzaji kuona zinakaa muda mrefu madukani mwao.
 
Kuna jirani hapa limelala chini tumelitafutia mafundi hadi[emoji114] [emoji119]. kila Fundi anakuja na majibu yake kifupi limeatamia. sijui tatizo ninini

Kama alikosea kuanzia service ya kwanza hasa ktk kubadili ATF basi imekula kwake. Wengi hawaangalii ATF inayopendekezwa na nissan mwisho wa siku gear box inazingua sanaa. Lkn kama umeweka oil zake za kiwango huwez kupata ttizo lolote zaid utabadili sensor kama imechoka au plug. Nina uzoefu na hayo nissan xtrail. Tatizo la mafundi hawayajui haya magari na ukizingatia uwezo wao wa kufikiri wengi wao ni wa chini sanaaa.
 
Napenda x-trail ya 2007na kuendelea .spea zake zinapatikana dar.tatizo LA steering na umeme linauvumbuzi hapa bongo
 
Kwa hiyo ukishindwa kununua Xtrail bora ununue Subaru Forester ya 2008 tu. Manake ndo gari za kiumeni zilizobaki
 
Katika magari ninayotamani kuendesha ni hii Nissan, lakini maelezo ya wakuu hapo juu yamenikatisha tamaa kabisa. Bora niangalie uwezekano wa Brevis.
 
Hii gari iko stable barabarani. Kama ni suala la spare kuwa taabu ni tatizo la magari ya Nussan yote. Ila tatizo board yake plastic na ulaji wa mafuta uko juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…