Daah haya mambo ya imani siku hizi hata sitakagi kuhukumu sana, maana tunaweza tukawa tunahukumu hapa kumbe hatujui labda mwenzetu alivyotoka pale alitambua kosa lake akaenda kumlilia Mungu wake amsamehe ila sisi tumekaa huku tunamjadili vibaya.
Tukumbuke kwamba kuwa mtumishi wa Mungu hakukufanyi uwe malaika kwamba hautatenda dhambi hilo hata Mungu analijua, hata kina Solomon na David na unabii wao walitenda dhambi (walizini waliua) lakini walikuwa na imani kali na mwisho wa siku walimlilia Mungu awasamehe na bila shaka aliwasamehe.
One thing I believe for sure hawa watumishi wa Mungu (wengi wao) wanajua sana kuishi na Mungu, tunaweza tukaona huku wanatenda dhambi tunasikia oohh sijui mchungaji amezini sijui padre ameua tunawahukumu na kuwatolea kashfa za kila aina kana kwamba sisi ni watakatifu sana.
Lakini hatujui wakiwa peke yao majumbani mwao wanaongea nini na Mungu hatujui wanamlilia Mungu kiasi gani awasamehe, na tukumbuke kuwa hakuna dhambi chini ya jua isiyosameheka isipokuwa dhambi moja tu ya kumkufuru Mungu basi and to God there is always a second chance for as long as you are still alive.