Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Si ndiyo hapo sasa tatizo ambacho watu wengi wanashindwa kuelewa ni kwamba injili inahubiriwa popote pale na ili watu wakupe attention wakusikilize ni lazima ujifanye mmoja wao kwanza yaani uendane nao kwa muda ili muelewane mfano unataka kuwahubiria mateja wasiomuamini Mungu hauwezi ukafika pale ukaanza tu moja kwa moja "Bwana Yesu Asifiwe" nakuambia watakufurumusha na mawe au watakuachia kijiwe wao wanaondoka ubaki unaongea peke yakokwani anachokiburudisha si kina mistari ya Mungu ndani yake au?
Ni lazima ufike pale uanze "Oya Masela Niaje" unagonga nao tano kwanza hapo lazima wakujibu na wakishakujibu unakaa nao unaanza kupiga nao kwanza story mbili tatu kuhusu maisha halafu ukishaona wamekuchamgamkia ndiyo unaanza sasa kuwahubiria kidogo kidogo
Sasa kufanya hivyo hakumaanishi kwamba eti na wewe umeshajiingiza kwenye dhambi hapana ila ile ni gia tu ya kuwafanya wakupe attention yao na wakusikilize sasa alichokifanya GG nakifananisha na hicho asingeweza kupanda stejini na kuanza kutoa step za kwaya kuwaimbia watu wa imani tofauti eti ili tu ajitofautishe nao anaonekane anawahubiria
Na kama angekuwa ni mkataji viuno si angeshafanya hivyo kwenye video ya ule wimbo wake kama wanavyofanya kina DP maana hao mara nyingi ndiyo huwa wanarudia step za kwenye video zao stejini sema tatizo wanadamu badala ya kusikiliza ujumbe wao wakawa wanawaza vile viuno vilivyokatwa pale bila kujua kuwa mwenzao pengine alifanya vile kulingana na hadhira iliyokuwa pale maana bila shaka asingeweza kukata vile viuno kanisani lakini anyway mwisho wa siku binadamu tunatofautiana mitazamo jamani so I stand to be opposed and corrected