MJADALA: Je, ni sahihi waimbaji wa nyimbo za dini kushiriki matamasha ya kidunia?

MJADALA: Je, ni sahihi waimbaji wa nyimbo za dini kushiriki matamasha ya kidunia?

kwani anachokiburudisha si kina mistari ya Mungu ndani yake au?
Si ndiyo hapo sasa tatizo ambacho watu wengi wanashindwa kuelewa ni kwamba injili inahubiriwa popote pale na ili watu wakupe attention wakusikilize ni lazima ujifanye mmoja wao kwanza yaani uendane nao kwa muda ili muelewane mfano unataka kuwahubiria mateja wasiomuamini Mungu hauwezi ukafika pale ukaanza tu moja kwa moja "Bwana Yesu Asifiwe" nakuambia watakufurumusha na mawe au watakuachia kijiwe wao wanaondoka ubaki unaongea peke yako

Ni lazima ufike pale uanze "Oya Masela Niaje" unagonga nao tano kwanza hapo lazima wakujibu na wakishakujibu unakaa nao unaanza kupiga nao kwanza story mbili tatu kuhusu maisha halafu ukishaona wamekuchamgamkia ndiyo unaanza sasa kuwahubiria kidogo kidogo

Sasa kufanya hivyo hakumaanishi kwamba eti na wewe umeshajiingiza kwenye dhambi hapana ila ile ni gia tu ya kuwafanya wakupe attention yao na wakusikilize sasa alichokifanya GG nakifananisha na hicho asingeweza kupanda stejini na kuanza kutoa step za kwaya kuwaimbia watu wa imani tofauti eti ili tu ajitofautishe nao anaonekane anawahubiria

Na kama angekuwa ni mkataji viuno si angeshafanya hivyo kwenye video ya ule wimbo wake kama wanavyofanya kina DP maana hao mara nyingi ndiyo huwa wanarudia step za kwenye video zao stejini sema tatizo wanadamu badala ya kusikiliza ujumbe wao wakawa wanawaza vile viuno vilivyokatwa pale bila kujua kuwa mwenzao pengine alifanya vile kulingana na hadhira iliyokuwa pale maana bila shaka asingeweza kukata vile viuno kanisani lakini anyway mwisho wa siku binadamu tunatofautiana mitazamo jamani so I stand to be opposed and corrected
 
Hakuna mahali amehukumiwa, wengi wanaonesha ni kwa nini hayuko sahihi kwenda kwenye tamasha lile anyways nimekuelewa
Basi labda mimi nimewaelewa vibaya, Sawa.
 
Gospel ni Injili, ni ujumbe wa kristo kwa wenye dhambi ili waachane na njia zao mbaya. Je ni nani wanaotakiwa kuubeba ujumbe wa Injili? Ni wale ambao ujumbe wa Injili umepata nafasi katika maisha yao; yaani wamempokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao (wameokoka). Kuimba nyimbo za Injili sio kitu kwani hata walevi wakishalewa huimba wakiwa klabuni lakini la muhimu ni je huyo Goodluck ameokoka? Ana sifa za kuubeba ujumbe wa Injili? Kama Goodluck anazo sifa za kuubeba ujumbe wa Injili basi alichosema herman joshua hapo juu (Thread no 9) ndio muongozo sahihi.

Ahsante
 
Ukiona hivyo ujue muziki wake unafanana na huo wa kwenye matamasha ya fiesta. Hivyo ni sawa tu, hilo jina la Yesu ni kinga ya kujificha tu, na wanamuziki wengi wa injili wako hivyo.
 
I dont know why... but he really look drunk to me hapo kwa stage .
 
Modern gospel, kuna uno moja hatari hapo kuanzia sekunde ya 55 , like uno la uzazi kutafuta mtoto
 
Hii inategemea na Mahusiano ya mtu huyo anayemwita roho mtakatifu na Mungu mwenyewe.
Kwenye kundi kubwa hivyo Roho angeshuka japo kwa watu mia wakaanza kunena kwa lugha katikati ya fiesta
 
Gospel ni injili maana yake kutangaza habari za kristo. Sasa kwa formula ya paulo jichanganye usitende dhambi. Kama alienda kubiashara kosa! Lakini kama nia yake ni kumtangaza yesu sawa kabisa. Je dhamiri yake ilikuwa wapi? Piano hutumika makanisani lakini hutumika katika macasino. Je utahukumu matumizi ya piano? Tuangalie message aliyoitoa labda kuna mtu mmoja alipata ujumbe na akaokolewa
Wwla Biblia haiko hivyo mkuu. Tusijaribu kupindisha kweli ya Mungu. Nikipata muda nitaandika kwa vifungu. Kwa kifuoi hicho alichofanya ni kushiriki ibada ya sanamu, kwa kisingizio cha kumtaja Mungu. Hilo ni tamasha la kumwinua shetani naye amejidhihirisha kuwa mwenye nguvu kiasi kwamba sifa za Mungu Mwenyezi zimetolewa kwenye ibada yake ili kumtukuza. The music industry!!
 
“Hawaogopi hata kusema HUKUMU imekaribia, na waimbaji wa DINI hata wao pia... WANATUNZWA na wanaotengeneza BIA”.

Alisema Joe Makini, HAO.
 
Wwla Biblia haiko hivyo mkuu. Tusijaribu kupindisha kweli ya Mungu. Nikipata muda nitaandika kwa vifungu. Kwa kifuoi hicho alichofanya ni kushiriki ibada ya sanamu, kwa kisingizio cha kumtaja Mungu. Hilo ni tamasha la kumwinua shetani naye amejidhihirisha kuwa mwenye nguvu kiasi kwamba sifa za Mungu Mwenyezi zimetolewa kwenye ibada yake ili kumtukuza. The music industry!!


Unajua mjadala huu ulikuwa sio wa kuhukumu bali kukumbushana uhalali wa kushiriki matamasha ya kidunia kwa waimbaji wa nyimbo za injili. Wengi wanafikiri tunamuhukumu Goodluck, No. yeye ni mfano tu maana ameshiriki kila mtu ameona. Huwezi kusema ameenda kuhubiri injili wakati amelipwa ili kwenda kuburudisha watu kwenye tamasha la kumsifu shetani... watu wamelipa viingilio wakaburudike.
 
Amani iwe nanyi nyote.

Nimeona clip ikimuonyesha muimbaji wa nyimbo za injili mchini, Goodluck Gozbert akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo Fiesta huko Mwanza. Nimeshangaa na kujiuliza maswali;

i/Mtumbuizaji anaelewa maudhui ya tamasha lile?
ii/Waandaaji walifikiria nini kumleta muimbaji wa nyimbo za injili kwenye tamasha linalokutanisha watu wa imani tofauti tofauti?
iii/Je, kilichofanyika ni halali kidini na kijamii pia?

Karibuni tujadili na kueleweshana pale pasipoeleweka.

Nawasilisha.


Hayo matamasha ya kidunia ndipo wanapatikana wenye dhambi, wasikie injili waokoke.

Huko kanisani kila mtu kaokoka.
 
Wanatuzwa na wanaotengeneza bia-Joe Makini.

Enzi hizo Jo akiwa anaimba vitu vya maana sio siku hizi anaimba upumbavu wake eti MCHELE.
 
Watu hawajielewi,kwenda fiesta ni sawa na kwenda baa au club ,watu wanapiga pombe hawajielewi we unawahubiria, mtaani kwetu kuna jamaa huwa anaenda baa kusumbua watu kwa kuhubiri,Siku moja watu wakamkaba baa wakamnyesha kwa nguvu hadi akazima ,baada ya hapo na yeye akawa mlevi
 
Huyo jamaa amejivika tu ngozi ya kondoo,kuna baadhi ya wasanii wakubwa wa bongo fleva anawaandikia nyimbo za mapenzi na bang za club,kwahiyo ni mtu alijificha tu hayupo real.
Wwla Biblia haiko hivyo mkuu. Tusijaribu kupindisha kweli ya Mungu. Nikipata muda nitaandika kwa vifungu. Kwa kifuoi hicho alichofanya ni kushiriki ibada ya sanamu, kwa kisingizio cha kumtaja Mungu. Hilo ni tamasha la kumwinua shetani naye amejidhihirisha kuwa mwenye nguvu kiasi kwamba sifa za Mungu Mwenyezi zimetolewa kwenye ibada yake ili kumtukuza. The music industry!!
 
Walokole wa Tanzania wanafiki..makanisani mnavuana vyupi daily...Mlisikiliza wimbo wa wakina Beyonce “if Jesus say yes nobody can say no “wakati Beyonce na mumewe sio walokole
 
Ile ni sehemu ya burudani, watu walienda kuburudika pale sio kuhubiriwa... kwa lugha rahisi yenye alienda kuburudisha waliofika pale ndio maana alitumbuiza mpaka na viuno alikata ili watu wafurahi.
Mfalme Daudi alivyopiga kinubi hadi nguo zikamvuka?acheni unafiki
 
Back
Top Bottom