1. Tvs kwenda km 60 kwa lita ni sahihi kabisa na inaweza fika 70km, it's 125 cc compared to boxer hizi za siku hizi.
2. Tvs haina tofauti sana na boxer kwa sifa ambazo nilizitaja huko juu kuanzia starehe, kutokuwa na vibration, uimara wa spare nk (zote mtengenezaji ni mhindi). Tofauti iliyopo kati ya pkpk hizi ni muonekano na speed. Boxer inachanganya kwa haraka sana na speed ya kutosha nafikiri unajua kuwa ndio mana zilikuwa zinatumika sana na wahalifu....nafikiri mpaka sasa hata vijana wanaopora mabegi na simu za watu huwa wanatumia boxer mara nyingi😀
3. Haojue is good ila kama ni kwa biashara, lkn kama ni matumizi binafsi sikushauri sana(hapa ni kwa ajili ya status)
4. Honda ace: huu ni mziki mwingine kabisa, sina uzoefu kwa matoleo yaliyopita lakin mimi natumia honda ace125 toleo la 2017 ya kazini, ni tamu sana kuanzia ustarehe, uimara, mafuta kiduchu nk. Hizi zinatengenezwa na mjapani lakini mchina pia naye amegonga copy zake ambazo huwezi tofautisha na ya mjapan, zipo kwa kiwango kilekile kinachofanana na za japani, nasema hivyo kwasababu nnayotumia ni ya mchina na nmetumia mwaka mmoja bila kugundua kama ni ya mchina mpaka baada ya kupitia manual yake vizuri lakin still iko vizuri haijawahi kubadilishwa spare ya aina yoyote ile zaidi ya kumwaga oil tu