Mjadala kipi kifanyike cha kudumu ili kukomesha mambo ya mizengwe yanayochangia kughairisha mechi?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Lawama hazijawahi kuondoa tatizo,
Kila jambo lina faida na hasara!
Moja ya faida ya mizengwe iliyotokea katika mpira wetu ituamshe ili tuboreshe kanuni na sheria ili kulinda hadhi ya ligi!

Pasipo kunyoosheana vidole kipi kitakuwa suruhisho la kudumu ili haya mambo ya mizengwe yasiendelee kiasi cha kuumiza wapenzi na washabiki wa mpira?

Kwa maoni yangu! Tuboreshe kanuni isomeke hivi.

1. Timu ngeni itahitaji kuutumia uwanja siku moja kabla ya mechi pasipo kuomba ridhaa ya timu mwenyeji, Timu wenyeji wakibainika wameihujumu timu ngeni kwa namna isiyofaa ili kukwamisha zoezi watapokonywa point 6
2. Timu hairuhusiwi kugomea mechi kabla ya malalamiko ya shauri lao kutolewa maamuzi na bodi ya ligi, kutangaza kutoshiriki kabla ya maamuzi ya bodi itatafsiliwa kuwa ni kuizarau mamlaka ya ligi
3. Timu yoyote itayothibitika kuzarau mamlaka ya ligi itashushwa daraja
4. Mechi iliyo ahirishwa kwa sabababu za kinanuni haitakuwa na kiingilio kwa mashabiki endapo timu zote mbili zitakapokutana awamu inayofuata.
5. Bodi ya ligi itatoa ufafanuzi wa malalamiko masaa 6 kabla ya mechi kuchezwa, Bodi ya ligi haitakuwa na mamlaka ya kuahirisha mechi kwa makosa ya kikanuni ndani ya masaa 12 kabla ya mechi
6. Uongozi unaosimamia uwanja utalazimika kuwepo eneo la uwanja masaa 60, kutokuwepo eneo la uwanja kutatafsiliwa kuahilishwa kwa mechi na bodi ya ligi itatangaza hilo.
7. Waamuzi wa mchezo wanaweza kubadilishwa kuamua mechi endapo kuna malalamiko yatayowasilishwa kwa nakala kabla ya saa 6 za mchezo kuchezwa

HAYA NI MAONI YANGU; WEWE UNA Maoni gani ili kuwepo kanuni za kudumu kukomesha mizengwe karibu katika mjadala!
 
Mechi za wapinzani zisiwe na timu mwenyeji wala mgeni bali wote watawathili katika uwanja husika muda wa mechi kwa ajili ya mazoezi ya awali (warm up) na mchezo
 
Iko hivi ukiona unaongoza taasisi fulan na ndan ya hao unawaongoza wapo waliojuu ya taasisi, juu ya viongozi wa taasisi yan wanaweza amua lolote au chochote na ww kiongoz usiwafanye lolote na ukakubaliana na matakwa yao bs kama unajielewa achana na hiyo kazi haraka sn maana hata kama una profile kubwa uwezo mkubwa utaonekana ww ni kilaza tu na utachafua cv yako tu.
 
Unashauri suruhisho la kudumu ni kujiuzulu!
 
Number 4 hapo umechemka.
Mechi ikihairishwa watakaopaswa kuingia kwenye mechi ya pili ni wale waliokua wamelipia kiingilio Cha mechi ya kwanza.

Sio eti mechi nzima iwe bure, ili ufanikishe nini Sasa?
 
Number 4 hapo umechemka.
Mechi ikihairishwa watakaopaswa kuingia kwenye mechi ya pili ni wale waliokua wamelipia kiingilio Cha mechi ya kwanza.

Sio eti mechi nzima iwe bure, ili ufanikishe nini Sasa?
Nini maoni yako
 
Kanuni zifanye kazi kwa timu zote, sio kanuni hizo hizo zinawaadhibu wengine na hapo hapo zinawalinda simba na Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…