Mjadala kipi kifanyike cha kudumu ili kukomesha mambo ya mizengwe yanayochangia kughairisha mechi?

Wanyama na ndege wa kufugwa hawaruhusiwi eneo la mchezo timu itakayobainika kuleta viumbe hao itapewa adhabu kali
Bila kusahau kupiga marufuku vizee vyenye mavazi ya asili kama vibwaya na kaniki vikiwa vimebeba tunguri na ambao sio sehemu yeyote ya benchi la ufundi la timu siku ya mazoezi ya mwisho ya timu kabla ya mechi.
 
Bila kusahau kupiga marufuku vizee vyenye mavazi ya asili kama vibwaya na kaniki vikiwa vimebeba tunguri na ambao sio sehemu yeyote ya benchi la ufundi la timu siku ya mazoezi ya mwisho ya timu kabla ya mechi.
Hahah
 
Hapa tunajadili solution ya wakati huu, siyo mambo ya miaka 50 ijayo.
Hiyo mechi iliisha ahirishwa, hakuna anayeweza kurudisha muda nyuma.

Tunajadili ya mbele. Simba wmalize uwanja wao Bunju wafanye mazoezi hata usiku kucha, na Yanga wamalize uwanja wao Jangwani au Kigamboni, na wao wakeshe huko sawa tu, lakini viwanja vya ligi visiwe viwanja vya mazoezi, isipokuwa kwa timu za mikoani au zitokazo nje ya nchi.

Vilabu vinapesa, mnawaacha watu wapuuzi wana filisi halafu mnataka mfanye mazoezi viwanja vya ligi.
 
Hebu tuongee ukweli, simba ni mgeni na uwanja wa mkapa? Game ya azam si alichezea pale?

Suluhisho la kudumu ni kuondoa usimba na uyanga kwenye ligi yetu. Hii inaathiri mpaka ustawi wa timu nyingine.

TFF na bodi ya ligi hawana meno kwasababu ya huu usimba na uyanga. Kanuni zimekaa vizuri ila msimamiaji hayupo
 
1. Polisi walinde Uwanja kama inahitajika kulinda Uwanja. Badala ya kutumia watu wasiotambulika kisheria.
2. Watu maalumu wabainishwe ktk timu inaporuhusiwa kuingia kufanya mazoezi kabla ya mechi wanapoambatana na timu.
3. Wamiliki wa Uwanja waanishe muda maalumu wa timu kufanya mazoezi, e.g masaa
4. Kanuni zifuatwe na zitafsiriwe endapo zitavunjwa
 
Hoja nzuri sana
 
Hahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…