******SIJUI WALE ''MAGWIJI'' WA INFORMATION TECHNOLOGY TOKA RWANDA WALIOOMBWA NA RAIS MAGUFULI WALISHAANZA KAZI HAPO ATCL? JAMANI TUKUMBUKE NA VIZAZI VIJAVYO TUACHE UBINAFSI TUSIWATENGENEZEE WATOTO WETU MA GENOCIDE YA AJABUAJABU,MTU MNAYE DEAL NAYE KASEMA ANAONDOKA MADARAKANI 2034 ISIJE IKAFIKA POINT TUKAWA KAMA CONGO REMOTELY CONTROLLED FROM KIGALI
INASIKITISHA
ERIKALI inayoongozwa na Rais John Magufuli inastahili kuonewa huruma, hasa na watu makini wanaoitakia mwisho mwema. Natoa wito huo kutokana na namna ambavyo inaongozwa kwa namna ya kipekee.
Ndiyo Serikali inayoomba kusaidiwa msaada ambao wanauwezo wa kuutatua, hata kuliko nchi wanayoiomba. Ni nchi pekee inayopewa misaada na nchi zilizoshindwa kuwamudu raia wake wenyewe kujikwamua katika lindi la umasikini.
Sababu kubwa iliyonichagiza kuandika kwenye safu hii, imechangiwa kwa kiasi kikubwa na msaada waliopewa Watanzania na India. Tanzania imepokea msaada kupitia Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya kiserkali ya siku mbili.
Ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili, India imeahidi kuisaidia Tanzania miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta za maji, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano na afya. Miradi ya maji yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 92, itaifaidisha miji 17 katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, na Zanzibar. Miradi yote hiyo inakadiriwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 92.
Mkataba mwingine unaohusisha mafunzo ya ufundi yatakayosaidia kuzalisha wataalamu mbali mbali. India pia imeahidi kuanzisha viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali kama malaria, figo na kisukari. Aidha India pia itaiwekeza Tanzaania kwenye viwanda, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha tengeneza vifaa tiba kwa ajili ya hospitali mbalimbali nchini.
Msaada huu kwa Tanzania nakiri kwamba ni neema, kwani pia Wahindi wamefungua milango kwa Watanzania kwenda kuwekeza nchini India pamoja na biashara.
Rais Magufuli aliwata Watanzania kujikita katika kilimo cha biashara kwa mazao ya kunde, dengu na choroko kwa sababu kuna
pia kusikia Dk. Magufuli anaomba ushauri wa kufufua shirika la ndege Rwanda wakati Tanzania imeanzisha Shirika la Ndege mwaka 1977, Rwanda wakiwa hawana uwanja wala ndege hata moja.
soko kubwa India na wataweza kuuza mazao hayo moja kwa moja bila kupitia wakala.
Sababu ya kushirikiana na India katika suala la uwekezaji nayo inaacha maswali eti kwa sababu ni nchi ya tatu kwa uwekezaji lakini cha kuchekesha Tanzania ndiyo inayofuatiwa na Uingereza na China.
Inasikitisha kuona India ambayo inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa lakini hadi sasa wananchi wake wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku raia milioni 400 nchini humo hawana umeme.
Kuna mambo mengine ukiyasikia katika serikali ya Dk. Magufuli kama una akili unaishia kucheka na kupuuza.
Kioja hicho cha India ni muendelezo mwingine kwa serikali inayoongozwa na Dk. Magufuli cha kwanza kilikuwa ni kile cha rais kukiri kusaidiwa mawazo ya kiuchumi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli, amewaomba Rwanda na wamemkubalia kusaidia wataalamu wa kufufua shirika la Air Tanzania na kwamba wataleta jopo la wataalamu wa teknolojia.
Uamuzi huo wa Daktari Magufuli kuitaka Rwanda kutusaidia kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ni dhihaki kwa wataalamu wetu.
Historia inaonyesha kwamba wataalamu wa kwanza wa Teknolojia Rwanda wamezalishwa mwaka 2001 wakati Tanzania ikiwa na wataalamu wengi wakiwa wakifanyakazi katika taasisi mbalimbali nje na ndani ya nchi.
Kwa ukweli huo naamini Rais Magufuli alianguka kusema hivyo na hakuwatendea haki wa wasomi wa Sayansi na Teknolojia nchini.
Naamini Daktari Magufuli alikosa la kuomba kushauriwa kwa sababu kama Rais alisahau kabisa kwamba hata Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia cha Nelson Mandela kinachotegemewa na nchi zote za SADC kipo Arusha, Tanzania.
Inasikitisha pia kusikia Dk. Magufuli anaomba ushauri wa kufufua shirika la ndege Rwanda wakati Tanzania imeanzisha Shirika la Ndege mwaka 1977, Rwanda wakiwa hawana uwanja wala ndege hata moja.
Rais Magufuli hakutakiwa kuomba wataalamu wa sayansi na Teknolojia bali alitakiwa kutazama hasa wapi tulipojikwaa kama taifa ili aweze kupata suluhu.
Magufuli anatakiwa kujua kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo inayoongoza kwa teknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki na hata katika usafiri wa anga Tanzania ndiyo yenye Rada ya kisasa kuliko nchi ukanda huo.