Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Wakuu, someni updates kule kwenye ORIGINAL POST,....KUNA HABARI TUMEPATA..SASA HIVI
 
Wakuu, someni updates kule kwenye ORIGINAL POST,....KUNA HABARI TUMEPATA..SASA HIVI

dah!
Inabidi watakaoenda wawe na ruhusa ya kutoenda job j3.
Kwani kumuona huyo mtu mnaingia kwa utaratibu upi?
Kama wanaandika majina kwanza, tafuteni mtu ambae yupo huko awaandikie majina ili mjue nafasi zenu kama itawezekana kumuona ndani ya siku hizo.
Kuhusu vyakula mnaweza kubeba bites na nyama za kukaushwa au kukaangwa.
Poleni ila kama mmeamua nyie nendeni msikate tamaa mapema. Nionavyo foleni itazidi kuongezeka. Sasahivi mtasikia majirani nao wanaenda.
 
Hizi habari tena si nzuri,
Nami nimefuatilia watu walioondoka Jumatano jioni hawajarudi hadi sasa. kuna uwezekano habari hizi ni sahihi kwa hiyo labda tujipange upya wakati mwingine ili tujiandae kukaa huko muda mrefu.
Vilevile inawezekana Mchungaji hakuwa na maandalizi ya kupokea watu wengi kiasi hicho kwa mara moja hasa kuanzia Jumatatu wiki hii. pengine sasa atafanya marekebisho ili huduma iende kwa haraka (just nawaza)
 
jamani aste aste, huyu babu antumia mizimu ya babu zake au ya nani .maana nimesikia alioteshwa ndoto usingizini,akaonyeshwa mti wa kutumia kutibu magonjwa.mjihadhari hizo roho zisije zikawavaeni halafu mshindwe kutoka mi simo!

Anatumia nini sio muhimu kwa sasa, nitakachojali mie ni kama tu hiyo dawa inatibu kweli magonjwa hayo full-stop!!
 
Hakika nitaenda huko ili niwaletee habari njema kama ni kweli
 
Kama mkiondoka leo Jioni siku tatu unahesabu kuanzia Kesho Jumamosi, Jumapili mzee afanyi kazi, Jumatatu alafu Jumanne. Kwa ushauri wango ombeni ruhusa kabisa ofisini ya wiki ijayo japo siku mbili (mpaka j4). Chakula unaweza kupata huko ila nahisi itakua ni ya garama sana. Kama mnaenda na gari lenu ni vizuri. Mkikodi gari mnawachwa huko dreva anarudi mjini kuchukua wengini alafu anwachukua baada ya hizo siku tatu.

Hizi ni information nilizo pata kutoka kwa mtu aliyerudi jana jioni.
Wakuu, someni updates kule kwenye ORIGINAL POST,....KUNA HABARI TUMEPATA..SASA HIVI
 
Kumbe wanadamu tuna matatizo mengi sana pakuyapeleka ndio hakuna hilo sasa nimeamini!!! hizi hospitali na makanisa yooote huyu babu kawapiku na kweli anatibu mana mimi nina rafiki yangu Arusha alikua na matatizo ya unyumba kwamba ( jogoo yake haifanyi ) kwa hiyo mkewe akaja juu kijana wa miak 29 haisimami?!! ameenda huko juzi leo amesema hawajalala amerudi ana nguvu kama simba!! true story
 
Mkuu mkirejea mtujuvye sasa naona Tanzania nzima na East Afrika itapiga kambi hapo Loliondo. Km ni kweli, basi Mungu anamaajabu makubwa.

Nadhani hata wamarekani watakuja, na bei ya 500 kwa dozi ukizidisha mara watu milioni moja 500X1,000,000= 500,000,000 milioni mia tano km sijakosea si haba.

mungu amlinde huyu mtu wasije wakamfanyia mizengwe watu wabaya.

Huyo babu hahitaji hela ndugu kwani wapo waliopeleka cruiser VX V8 baada ya kupona ukimwi wakarudishwa nayo!!
 
Babu anaweza kututibia mkulu wetu asianguke tena?...hebu muulize
 
kaka PakaJimmy

umetoa maelezo ya. kina Thankx
 
Kwa wale waliopo Arusha kuna magari yanatoka stand adi hapo kwa mchungaji. Nauli ni elfu sitini kwenda na kurudi. ANGALIZO: kwa wale wenye magari binafsi barabara ni mbaya sana. Gari za kufaa ni landcruse,landrover na yote ya aina hiyo. Ukiwa Arusha city watu wanaonda ni wengi so njia ya kwenda utafahamu.

sasa naanza pata Mashaka mimi nina Nnisan HardBord 4X4; siwezi fika huo
 
Hata nyakati za Yesu kuna watu hawakuamini kwamba alikuwa akiponya viwete, vipofu na wenye ukoma. Akina Tomaso hawaishi duniani, wapo kila sehemu, kila wakati. Kumbuka kwamba imani inabomoa milima. Kuna Mama mwingine mwenye kutoa huduma kama hiyo, yuko katika kijiji cha Kwemasimba wilayani Korogwe, mkoa wa Tanga, kilometa chache toka barabara ya Tanga-Moshi, unakatishia eneo la kona za Msambiazi. Ukifika Korogwe tu stendi, ukiuliza mama anayeponya kwa maji unapelekwa na watu wa bodaboda, sio mbali.
 
mbona kila mtu anasema "KUNA MTU KAENDA....KUNA MTU KAENDA".......mi nataka kumsikia huyo MTU KAENDA aje hapa aseme mwenyewe.....acheni uzushi.
 
Jamani baada ya kusoma post nyingi za kushawishia na kukatatisha taamaa; nikamkubuka mdau wangu mmoja katika kazi yuko Arusha, kanisibitishia habari hizi ni za kweli, na kuna mtu offisini kwake alikuwa anasumbuliwa na kisukari anasema toka atoke huko anaendelea vizuri kabisa. pia kuna jamaa yake mwingine yuko na alikuwa mtu wa 70, amfikie hiyo DR wa ukweli. Inaonekana ni mtu mmoja kwa mmoja anapita kwa mtaraamu na kupata dawa. Bado natafuta mdau mwingine anijuze

mengineo
Inabidi Loliondo waweke kodi ya wageni kuingia humo wilayani ili waongeze kipato cha almashauri yao.
 
Ukweli nilikuwa nina wasiwasi na wazazi wangu maana wameenda uko jana na watu wengi kutoka moshi,hawapatikani hewani katika simu zao za viganjani,ila sasa napata faraja kumbe watu wengi wanaenda huko nami nikirudi tu Tz lazima nifike huko.
 
Back
Top Bottom