Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Rostam anachanganya mambo hapa.hao ndugu zake hawajapona kutokana na dhambi zake alizotufanyia watanzania.na si ajabu hta lowasa nae akaponza ndugu zake wasipone.
laana yao haiondoki wala hawasameheki kama wamemtukana Roho Mtakatifu.
maskini mjomba Hassan kaponzwa na rostam
 
Lakini sio kwa sababu Rostam basi kila kitu apingwe.
Yeye amesema ndugu zake watano walipewa hiyo tiba ya babu na hawajapona so ana haki ya kutoiamini hiyo tiba lakini ndugu zake hao wangepona na angesema kuwa haiamini hapo ndipo tungemshangaa.
 
unajua dawa zoote zilizopo hazitibi watu wote kwa 100% lazima utasikia mwingine anakuambia akiwa na malaria akinywa mseto haponi mwingine fansida haponi hata ARV kuna wengine haziwakubali, kikubwa dawa ya babu ni ya kiimani km imani yako ni ndogo na matendo ysko machafu km ya huyu rostam na ukoo wake kamwe haiwezi kukuponya. so kashfa ni mfa maji haishi kutapatapa!! shuhuda zipo kibaaaaao watu wamepona.
 
Uncle wake Dowans hajapona kwa babu?? whaaaaaaayyyyyyyyyy,,,,,, this is so sad Dowans, enewei sio shida cheki ya $96 million ipo atakuwa well taken care of,,,:wof: :rolleyez:
 
Ila bwana ulimwengu una kingeledha kigumu! mbona hata wadhungu wenye lugha yao wakiandika makala hawaweki mavocabulari kama yako? Lengo ni watu wote hata wenye kujua cha kuibia kama sisi tuelewe au ni nini? Anywei nimedonoa kama kuku......
 
Uncle wake Dowans hajapona kwa babu?? whaaaaaaayyyyyyyyyy,,,,,, this is so sad Dowans, enewei sio shida cheki ya $96 million ipo atakuwa well taken care of,,,:wof: :rolleyez:
maskini mjomba hassan hata akipewa cheki ya bilioni 10,bado kivuli Rostam kitasababisha asipone
 
Yani ameona ya BABU ndiyo anaweza kuzungumza, mambo tunayotaka ayazungumzie hatumsikii. Aache kupotezea......
 
Wana Jf tuwaombe wale wasemao tiba kwa babu haifai, watupe njia mbadala mf;
Wajenge hospitali na huduma/tiba zenye viwango ambapo kila m/nchi atamudu.
Waone kama watu watahangaika na usumbufu wa foleni kwa babu ili atibiwe malaria sugu!
 

Nimefurahishwa sana na maelezo yako. Mungu akubariki sana kwa kusema ukweli huu. Wakristo tafadhali tuwe macho, tusibali kuchuliwa na kila upepo wa elimu unaotokea
 
Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:22 0diggsdigg

Shija Felician, Igunga
WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.

Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... “Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?”

Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.

Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.

Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.



Dhu inaelekea naye alishaenda huko kupata kikombe chake!!!
 
Ila bwana ulimwengu una kingeledha kigumu! mbona hata wadhungu wenye lugha yao wakiandika makala hawaweki mavocabulari kama yako? Lengo ni watu wote hata wenye kujua cha kuibia kama sisi tuelewe au ni nini? Anywei nimedonoa kama kuku......

Anajifanya tu; Kiingereza kigumu kiko England na wala hawaandiki hivyo kama yeye wanapotaka kuwasiliana na Umma.
 
Kwani Rostam hana mawasiliano best wake Jakaya Mrisho Kikwete akampa ushuhuda wa tiba ya babu?
 

Na Bwana Mungu akamwambia Abram, hutaitwa tena Abram ila tangu sasa utaitwa Ibrahim. Atakayekulaani wewe atalaaniwa, naye atakayekubariki atabarikiwa. Tumsifu Yesu Kristu.
 
Hawo ndugu zako wapeleke ulaya wakatibiwe kwani zimeisha? Sisi tutaendelea tibiwa na babu tu hatuelewi kitu.Ww mwenye nazo na nduguzo huwezi pona kwa sababu huna huruma na watanzania.Kama ungekuwa na huruma ungewekeza kwy matibabu.Acha kuponda tiba za sie wanyonge wapeleke jamaa zako Iran na canada wakatibiwe
 

Asante ndugu kwa ufafanuzi.
 


Nilikuwa nisichangieee hii..mada lakini kwa upupu wako huu..naona nikujuze nafikiri umechoka kuishi wewe kwa maaana haya unayoandika hapa ni laana tuupu...
 

Good explanation and I hope watu kama Miss Judy wataelewa sasa
 

Thanks ndugu, mi watu nashangaa wewe kama huamini si ukae kimya.
 

Kwahiyo wewe unaona aliyosema Rostam, Mwingira na Kakobe ni MAONI SIYO. Wao walikandia na siyo maoni. Naomba usiniharibie siku dada yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…