Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.


Duuuuuuuuuuuuuh!
 
wamepata mda wakuongea ss we ngoja mda si mrefu cd itabadilishwa na video ya dowans itaendelea tena
 
hiyo haiwezekani, we hujui kuwa Mungu huwanyeshea mvua walio wema na wabaya?

Lakini Mungu alitoa adhabu jangwani kwa wana Israel walipomuasi. Hii ni kuwakumbusha. Kumbuka daima Yesu alipomponya mtu alisema, 'Enenda zako usitende dhambi tena', na 'Mtu akitaka kutoa sadaka akikumbuka ndugu ana neno naye, sharti aiweke kando aje apatane na nduguye ndipo aje atoe sadaka yake'.
 

Alikua na nia ya kutoa mimba huyo,
na babu hatoi dawa ya upuuzi huo!!
tena mwambie imeandikwa 'Usimjaribu Bwana Mungu wako'
 
Jamani kama Mungu angetuangalia sote na matendo yetu wengi wala tusingemwita kabisaaaa!!! Hata huku JF tupo wengi tu na nadhani ni wote hakuna msafi hata mmoja. Nani kati yetu msafi angali wanadamu tuna mizani ya kupima dhambi za wengine lakini za kwetu wala!!! Ni mara ngapi humu watu wamewatusi wenzao? Ni mara ngapi watu wamechangia uongo na kitu ambacho hata hawakijui lakini ansema mawazo yake kama ndiyo ukweli kabisaaaa?? Ni mara ngapi tumekuwa wazandiki na wanafiki kwa wanasiasa ukimwona unajikomba mheshimiwa ukifika huku JF ambapo wengi majina tumeficha na kuanza kumsema vibaya?
Hakika hata mmoja hakuna wote wametenda dhambi lakini Mungu ni wa ajabu..Yeye alimtuma Mwana wa Adamu aje kutafuta wale waliopotea. Kondoo aliyepo zizini hatafutwi anatafutwa yule ambaye hayuko zizini. Lakini pia tuna ahadi kuwa tukiomba msamaha Mungu atatusamehe na ijapokuwa dhambi zetu ni nyekundu kama damu basi zitakuwa nyeupe kama theluji. Hakika kama Watanzania siku moja tungechukua muda tu wa dakika moja wote kwa umoja wetu kumwomba Mungu katika haki na kweli hakika mabadiliko ya hali tuliyonayo yangetokea mara moja. Tatizo letu..Imani Yetu Haba....
 
Nilishasikia kuna watu waliiba dawa ya babu wakainywa na kwenda zao. Huko kwao walianza kuvimba miili yao na wakakiri walivyofanya kwa babu. chapchap walipelekwa kwa babu na kuomba radhi wakikiri makosa yao. Babu bila hiana akawaonya waache tabia mbaya, akawaombea kwa Mungu nao baada ya dakika mbili wakapona. Kwa hiyo inawezekana hata huyo anayemsema mleta hoja alifanya madudu tofauti na alivyotakiwa kuinywa dawa na hayo ndiyo malipo. Arudi kwa babu akaseme wapi alikosea aombewe naye apone. Kwenye ugonjwa sio vema kuleta mzaha.
 
Una uhakika gani kama dawa ya babu ndo iliyomsababishia maumivu hayo ya tumbo???... Babu alianza kutoa huduma miezi mingi tuu iliyopita na hakuna mtu aliyevimba au kupata any side effects.. Sasa huyo jamaa yako itakua anamatatizo yake binafsi na msimsingizie babu... Babu katibu watu malaki afuu eti mtu mmoja tuu eti ameumwa tumbo!!!!!!???
 

Atakuwa katenda dhambi tena huyu.maana dawa ya babu ukiwa na kagonjwa hako hutakiwi kuchakachua wala kuchakachuliwa sasa yeye kama amekurupuka na kuona amepona....madhara yakutofuata mashart hayo.
 

Kutokana na dhambi ya ufisadi aliyonayo Rostam hawawezi kupona. Hata yeye Rostam akienda hatapona mpaka awe na imani na aache dhambi ya ufisadi
 
Mi siwalaumu wanaoamini kama dawa ya babu inatibu,,pia siwalaumu wanaoamini kama haiponyi k7bu kujieleza ni haki ya kila mtu,,,hatupaswi kuwabeza wanaosema wameponywa na dawa ya babu bali tunapaswa kumshukuru mungu kwa kuwaponya,,lakin pia hatupaswi kuwalaumu au kuwabeza wasioamini kama dawa ya babu inatibu tunachotakiwa kufanya ni kuwapa muda zaidi wa kuweza kujithibitishia wenyewe kama dawa inaponya au haiponyi......




njia atumiayo mtu kupata ufumbuzi wa matatizo ndiyo kielezo cha utu,hekima na busara aliyonayo...........
 
Isije ikawa kwa kutumia pesa yake walihonga wakavuka foleni halafu ndio ikawa hivyo..
 

wewe ndio unabidi ufikirie unamjibu wapi kaandika mambo ya siasa? Ufisadi ndio unaandika pumba mwache mwenzio acha kupurukuka kujibu bila kuelewa na kuangalia maneno kwa ukubwa

Unarukia kumsema mwenzio kwani wewe umeandika cha maana?
 
Kwa maana hiyo hakuna hatammoja atakae pona, maana watu wote pamoja na Babu wamejaa zambi


Hakuna mtu duniani ajuae kama dhambi za mtu nyingi au Mungu kazisamehe or hana etc hivyo


Lazima uombe mungu akusamehe dhambi zako na ndio maana tunatubu

IMANI. Bila hii utaponyaje? Huyu babu ameonheshwa na Mungu hivyo inaeleweka iweje

Mtu uende kunywa kama iingie tu mwilini bila hata thanks you Jesus etc. Mnajua itakuwaje

Oyaaaa
 
Inawezekana ni kweli au ni uongo......Huyu Babu inahitaji kuwa na nguvu ya kimungu ili kugundua kuwa ni kweli au la....................

Mungu ndie awezaye yote. Kwani kama ni kweli au la mie sioni tabu labda mtu asiye na shida ndio hatakunywa kwa kuogopa dawa ila ni dawa ya kawaida kunywa na imani, kwa nini kuangalia kweli au uongo? Wachawi watakimbia na wafuatao nguvu za shetani

Imani yako wengi wanaanda kanisani wanasali wanasaliwa na hapo ndo ngoma unaona wengine Mungu awashukii kuwabadilisha chochote sasa unategemea utaenda kanisani bila Imani na Mungu atakusaidia, pia bila kutoa sadaka, kumsifu bwana, kuna 10% yaupatacho etc

Usisikilize watu as katika kitu kizuri cha Mungu shetani huwa bado anajaribu kuzuia ndo kama usikiavyo.

Kwa kweli ni mengi yakusema ILA naishia hapa, natumaini utapata Imani ya kwamba bwana Mungu ndie king of kings na hakuna mwingine zaidi yake.

Pia mungu hatawaadhibu waendao kwa prophet waongo bali yeye atadeal nao wao imo kwa biblia
 
Namuunga mkono jenerali pia wa2 hawakatai babu kutibu bt masharti anayotoa babu ni ya kitapeli na cyaki mungu ki ufupi BABU + 500 = DECI MPYA

maisha hayawezi kuwa rahisi kiasi hicho NEVER!, wa TZ tuna hulka ya kutaka shortcuts/quick fixes au majibu rahisi kwa mambo magumu, nawasikitikia wale ambao walikuwa wanapata ARV na sasa wamezitupa baada ya kupata kikombe cha babu, huyu babu hakuanza leo wale wenye VVU waliopata hicho kikombe wakati anaanza majority wameshakufa! (samahanini kwa kuwa hampendi ukweli huu)
Proof ya kupona VVU si rahisi kama watu wanavyojitangaza, vipimo vya kawaida vya VVU (rapid HIV tests) kuwa negative si ushahidi tosha, kuna vipimo zaidi ya hapo, kwa wale walio kwenye ARV nawashauri mkishapata kikombe usiache ARV, kwa kuwa mbele yako kuna kazi kubwa ya ku_prove kuwa mwili wako hauna VVU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…