Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

taarifa za kuaminika zinasema kuwa Mtoa tiba huyu, kufika Jumatatu atakuwa anaanza MAFUNGO ya aidha KWARESIMA au kitu cha namna hiyo, na hatokuwa operative tena kwa muda fulani..
Kwahiyo kwa waliodhamiria ni bora wawahi wikiendi hii!
 
1. sina jibu
2. Mgonjwa ndie anayemfuata Dr. Pia haya mambo ni ya imani, ukifika mpaka huko aliko tayari umeonyesha imani kuwa utapona.
3. Inawezekana gharama za dawa na kuchemsha etc. hazizidi 500shs. kwahiyo hataki kuwaibia wagonjwa.
 
huyo mchungaji nimeshamsikia habari zake sana-kuna ndugu zangu wataenda hukuo muda si mrefu-namini watakaporudi na kuona mabadiliko yao ndo nitaaamini kua kweli anatibu
 
haiwezekani kuhama....alipoelekezwa na roho ni huko Loliondo...usonjoni......hata sisi watu wa Arusha tulipenda sana asogee sogee hata hapo Mto wa Mbu....kwenda Loliondo si ishu ndogo...lakini habari ndio hiyo....lipa elfu 70 za usafiri, dawa sh 500....hili ni fumbo la imani....Tafakari
kweli nauli ni kubwa sana-na niliuliza kwa nini watu wasitume dawa kwa hao wanaoenda-nikasikia kuwa eti dawa unatakiwa kupewa wewe unayeumwa,na si mtu mwingine then akuletee-ukifanya hivyo,dawa haitafanya kazi
 
Kwa muda sasa habari zimetapakaa kuhusu tiba ya magonjwa sugu inayopatikana huko Loliondo wilaya ya Ngorongoro. Dawa hiyo inasemekana ni ya kunywa na unalipa sh mia tano tu. Anayetibu hataki chochote zaidi.

Wanasiasa mbalimbali wanaenda huko kutibiwa. Tiba hiyo haina TBS wala TFDA hawaijui.

Ikatokea ikawekwa tone la sumu, tutakuwa na janga la taifa. Namkumbuka mtu aliyeitwa Kibwetere.

Sina tatizo na suala kwamba imani yako inaponya ila in the unlikely event something goes wrong as it usually does at least I said.

Kama tungekuwa na viongozi na si wanasiasa wangekuwa wametoa tamko na maelekezo. Tatizo letu nchi imejaa wanasiasa. Na wao wanaenda huko kutibiwa. Kama kuna aliyepona atujulishe.

Jana kuna mgombea Ubunge mmoja ameniambia kuna daktari amemueleza kwamba kuna wagonjwa wawili wa HIV wameenda kunywa hiyo dawa ila nao its worse!

Nimesoma humu kila mtu anasema kasikia fulani kapona, amna anayesema yeye ndiye kapona; ila ujue kuwa kama wakipona ni vyema kabisa na pia kama anawapa sumu kwa maana ya kuwaua pia ni vyema sana, maana kote ni kuponyesha Ukimwi. Hizo njia mbili zote zinakubalika katika kuponyesha Ukimwi.
 
usiwadanganye watanzania wakapata matumaini, dawa ya ukimwi ni kuacha zinaa ndugu zangu.
 
Ona sasa watu imani yao inavyokuwa ya mashaka; mm nimejitolea kutibu watu humu sijapata mteja hata mmoja simply kwasababu sitoi concotions which means akili imeshakuwa programed ki karumanzila....The word of God says we rwestle not on blood and flesh but on principalities powers and against all imaginations untill we subject our minds unto Jesus or in other name word of God. It says again be renewd in your minds.....hapa ngoma ile ile bila mila na jadi watu hawa poni..ndiyo maana watu wakiambiwa na Ndodi toa milioni hata kama anakupa maji basi unaamini kwakua maji ya Ndodi yanafanana na yule Kalumanzila uliyemzoea tofauti ya Dr. Ndodi ni masafi lakini ya Kalumanzila machafu...tena kwa wale walio kolea kwenye tradition akiona hayo masafi haamini kama yana ponya ila ukiweka rangi inayofanana na ya kalumanzila utahamisha population yote kwenye makazi yako.....Poleni sana ndugu zangu...My people perish because of lack of knowledge...
 
Wakuu nimepata taarifa kwa mtu wa karibu kutoka mikoa kaskazini, kuwa kuna ex-mchungaji anatoa huduma ya ajabu(anaponya magonjwa), kwamba ana dawa aina ya miti aliyooteshwa(kimaono). hiyo dawa huchanganywa na maji halafu kila mtu ambaye ataitaji hunywa kikombe kimoja, na matokeo ya kupona hutokea mda mfupi. magonjwa ni kama sukari, pressure, ukimwi etc.

Kwa hiyo watu wanamimika sana hilo eneo aliko huko loliondo ARUSHA.


mdau mwenye data kamili anaweza kutusaidia
 
Hilo halina kuuliza mzee,ni ww tu ndio umebaki kwenda kunywa dawa kwa babu,fanya fasta kabla hajasitisha huduma.
 
Ndg wanaJF kutokana na hali iliyopo nchini kwa sasa kwa watu kwenda loliondo kwa mchungaji kujipatia matibabu ya magonjwa sugu km Kisukari, kansa, pumu, degedege na HIV/AIDs nashauri serikali ijenge barabara hiyo kwa kiwango cha lami haraka iwezekanavyo ili kupunguza adha ya usairi iliyopo kwa sasa.
Magari ya serikali yanaongozana kwenda loliondo kwa ajili ya nguvu kazi yake kupata tiba.
Ikiwezana wakandarasi wapewe km 2 kila mmoja ili kuharakisha kukamilika kwa barabara hiyo kwa muda mfupi iwezekanavyo.
Nauli ni juu ukilinganisha na umbali wenyewe kutokana na ubovu wa barabara.
wasafiri wanalazimika kulipa kati ya tshs 40,000 hadi 100,000 kama nauli.
Nawakilisha ili tuweze kupata mawazo mengine kutoka kwa great thinkers (wanaJF)!!!
 
Labda wapitishe grader na kushindilia kama rourine maintenance. Kujenga lami sio rahisi hivyo mkuu.
 
I sometimes dont understand these things:
1. Ameoteshwa na Mungu
2.Lazima akuone ndio upone
3.Dawa ni 500 tu.
Hivi Mungu anabagua? yule bibi kizee pale mtwara ana kansa halafu nauli ya kwenda kule hana si utakufa na hiyo kansa!
Ina maana hii ni tiba kwa wenye uwezo wa hiyo 70,000 ya usafiri tu.
kwanini anacharge 500, dawa ambayo angeweza charge 100,000,000,000,000..... na akapata wateja?
Siwezi chemsha hiyo mizizi mwenyewe nikanywa nikapona?

1. sina jibu
2. Mgonjwa ndio humfuata Dr. Pia hapa kuna suala la imani hivyo kufika huko utakua umeshaonyesha imani
3. Inawezekana gharama za kutengeneza hiyo dawa hazizidi 500 shs, na hataki kuwaibia wagonjwa au kupata faida kupitia kwa wagonjwa
.
 
Habari wana Jf, mji wa Arusha umezizima kwa wageni wanaoingia kutoka mikoani kuelekea Loliondo kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya magonjwa sugu ukiwepo ukimwi kwa gharama ya sh.500 tu, mwanzo habari hizi hazikupewa uzito hasa hapa Arusha ila baada ya watu kupona kabisa kisukari, presure na ukimwi dawa hiyo imethibitika ni kweli inafanya kazi, Mchungaji aliyeonyeshwa maono ya kutengeneza dawa hiyo haihitaji chochote kutoka kwako ila sh.500 tu, nipo kwenye taasisi moja kubwa ya kutoa tiba hapa Arusha tayari imeshathibitika kwamba dawa hiyo either inaponyesha ukimwi au inavificha virusi coz watu waliokuwa hoi baada ya kumeza dawa hiyo wanaonekana Negative, kwa taarifa zaidi soma gazeti la Mwananchi, mimi nimeshuhudia mtu aliyepona kabisa kisukari!! MUNGU NI MKUBWA
 
Afadhali uwaambie akina Tomaso..
Tumejaribu kuwaeleza watu juu ya hii ishu lakini wanakuwa reluctant...By the time wanagundua itakuwa too late!
 
Afadhali uwaambie akina Tomaso..
Tumejaribu kuwaeleza watu juu ya hii ishu lakini wanakuwa reluctant...By the time wanagundua itakuwa too late!

Mimi nipo hapa Arusha, kaka sio uongo, kama una ndugu yeyote Arusha uliza, nauli tayari imeshapanda mara mbili ya viwango vya zamani, nauli ilikuwa 30,000 kwenda na kurudi sasa ni 60,000-100,000 na kuna jamaa zangu wana Cruizer wana make sana tu!!!
 
Back
Top Bottom