Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Ukweli utabaki pale pale siku zote ni kwamba barakoa aina ya N95 respiratory masks, Surgical masks,FFPI ndio zipo imara kuzuia maambukizi ya Corona .Na kwa mujibu wa Intergrated Pharmacitical company " Varsoy healthcare" na American lung association Barakoa hizi ndio zenye uwezo wa kuzuia maambukizi "Particles of virus in Droplets" kwa asilimia kubwa karibu 95.
Barakoa za vitambaa au sponji (Cloth Masks ) ina asilimia ndogo sana kuzuia maambukizi.Na kumekuwa na mjadala kutoka kwa wanasayansi na wataalamu mbalimbali ulimwenguni ,mfano.American lung Association wao wanasema barakoa za vitambaa zinasaidia kwa kiasi kidogo na sio upande wa mvaaji (wearer) ila kwa upande wa mtu mwingine kama aliyevaa anaviashiria vya ugonjwa anaweza akapunguza kuusambaza kwa kuvaa hicho kitambaa dhidi ya mtu mwingine ila hicho kitambaa hakimsaidii yeye kiasi kikubwa kujilinda asipate kutoka kwa ambaye ni infected na hajavaa hiyo barakoa.
American lung association wanasema"Home made masks or Cloth Masks are not intended to protect the wearer but to protect against unintended transmission in case you(wearer) are asymptomatic".
American lung association wanapendekeza watu watumie barakoa za N95 , Surgical masks na FFPI zile ambazo ni Medica masks ila wanasema kama upatikanaji ni mgumu ,barakoa za vitambaa ziwe kimbilio la mwisho yaani " Last resort" .
"The Last resort " ndio njia iliyotumiwa na Marekani.Mara zote wahudumu wa afya ambao wanawauguza walio athirika na Corona katika nchi zilizoathirika sana kama marekani ndio hupewa kipaumbele kutumia hizo barakoa imara za N95 na Surgical masks sababu kwanza upatikanaji kuwa mdogo na matumizi yake ni makubwa.Pia uimara wake unafaa sana watu kama wataalamu wa afya ambao wapo katika mazingira ya hatari ya kuambikizwa.
Kuna watu wanazungumzia juu ya kauli ya Surgeon Jerome Adams daktari wa Marekani,pia muongozo wa CDC juu ya mapendekezo ya kutumia Barakoa za vitambaa hoja hii imebebwa sana na Shangazi yangu Maria Sarungi akitetea sana .Mimi sitaki kupinga mapendekezo ya CDC ,White House Coronavurus Task Force na kauli ya Dr.Jarome Adams.
Ila tunapaswa kuelewa kwamba ukweli wa hili upo wazi kabisa.Marekani imekuwa ikipata uhaba mkubwa wa Barakoa za N95 , Surgical masks hata FFPI.Hivyo kupelekea hata wahudumu wa afya kuwa na uhaba wa hizo barakoa.
Jambo hili limefanya White House Corona virus task force ,CDC na huyo Surgeon Jerome Adams kutoa muongozo (Guidelines) mnamo tarehe April 3 ,2020 kutaka Barakoa ya vitambaa ivaliwe na umma "Cloth Face Coverings voluntary for public health measures" .Sababu kuu ni kutoa mwanya wa Medical masks kama N95 , Surgical masks na FFPI kupatikana kwa urahisi kwa ajili ya wahudumu wa afya (Healthworkers) huku wakijua kabisa barakoa za vitaa hazina nguvu kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ingawa inapunguza kwa kiasi kidogo sana hasa transmission ila sio guaranteed ya kuwa salama sana.
Na unaweza kulishuhudia hili kupitia huyo huyo Surgeon Jerome Adams ambaye ni daktari wa Marekani ambaye kuna watu wanamtumia kutetea barakoa za vitambaa ,tarehe 29 Feb, saa 3:08 Pm ali tweet akisema "
" Seriously people -Stop buying masks,they are not effective in preventing general public from catch up coronavurus ,but if healthcare providers can't get them to care for sick patients ,it puts them and our communities at risk".
Mtu mwenye akili ataelewa kwanini medical masks kama N95 na Surgical masks aseme sio preventive na awaambie watu wasitumii sio muhimu Ila wahudumu ndio watumie hizo N95 , Surgical masks na FFPI ?
Maana yake N95 na Surgical Masks na FFPI ni muhimu sana katika kuzuia maambukizi ila ukweli kwa muda wamekuwa na uhaba hadi leo ndio maana walitumia njia ya kuwaaminisha Raia kwamba hata Cloth Mask (Barakoa za vitambaa zinafaa ) ,hii ndio hoja ambayo imebebwa na watu huku kwetu na kuaminishana kwamba Barakoa za vitambaa ni bora .
Dr.Fauci Anthony ni Mkurugenzi wa National Institute of Allergy and infectious Disease,huyu ndiye aliyeweka wazi kwanini CDC na Whitehouse Corona virus task force na huyo Surgeon Jerome Adams walipendekeza matumizi ya barakoa za vitambaa.
Dr.Fauci Anthony anasema ,"There is currently shortage of N95 and surgical masks ,if every one wears mask the healthworkers who need ,they may not get them." Anasema kila mtu akivaa mask , wahudumu wa afya wanaozihitaji hawawezi zipata ,ila hapo hapo wanaendelea kushauri kama kuna upatikanaji wa hizo barakoa za N95 na Surgical masks watu wavae. "Mwenye akili aelewe sasa" haya tuje kwetu Tanzania.
Nilimsikia RC Makonda jana akitangaza watu wavae barakoa ,akisema "Nunua au kata kitambaa cha kanga ,leso au rababendi " .Haya mambo lazima yafanywe kwa utaratibu ndio maana nilisema tamko kama hilo alilotoa Makonda lilipaswa litolewe na Mh.waziri kwa nchi nzima au kwa mikoa ambayo ina maambukizi ,wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanapaswa kupokea maelekezo kutoka kwa Waziri kuliko wao kutoa matamko.
Kuwaambia watu wavae barakoa ni jambo jema ila barakoa zipi ? Je, wananchi wana elimu ya hizo barakoa kwanza ? Je wanajua zinatumika namna gani na zinatumika wapi na wapi ? ,Je wanazitumia siku moja au wanarudia kutumia baada ya kufua ? .Ni wananchi wangapi wanajua elimu ya barakoa ?
Je,Barakoa zipi zinapaswa kutumiwa ? ,N95 au Surgical masks ,FFPI au barakoa za vitambaa .Mimi binafsi nina amini katika barakoa za N95 , Surgical masks na FFPI ,Shangazi yangu Maria Sarungi ana amini katika barakoa za vitambaa za kutengeneza ,Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda anaamini katika barakoa za vitambaa vya khanga ,Leso na rababendi ,Naibu Waziri wa Afya Dr.Faustine Ndugulile alitoa tamko Bungeni akisema barakoa zinazopaswa kuvaliwa ni N95 na Surgical masks na sio ya vitambaa.
Mimi binafsi siwezi kukubaliana na mtu kusema tuvae barakoa za vitambaa ikiwa hakuna maelezo ya mamlaka na jitihada za kurahisisha upatikanaji wa barakoa za N95 , Surgical masks na FFPI . Serikali inapaswa ioneshe jitihada za kurahisisha upatikanaji wa barakoa hizo na udhibiti wa bei isiwe juu .Kama Bei itashindwa kudhibitiwa na upatikanaji wa barakoa hizo za N95 , Surgical masks na FFPI utakuwa wa shida ,ndio sasa tunapaswa kwenda katika kimbilio la mwisho (The last resort) la kutumia barakoa za vitambaa kwa wasio weza kuumudu upatikanaji wa barakoa hizo za N95 na Surgical masks.Kwa hatua hii ndio nitakuwa nimeungana na Shangazi yangu Maria Sarungi kutumia barakoa za vitambaa.
Tuelewe kama watu watakosa namna na kuamua kutumia barakoa za vitambaa (Cloth Masks ) , kunapaswa kuwe na maelekezo ya wataalamu juu ya aina bora ya barakoa ya vitambaa inayopaswa kutumika.Nimesoma andiko la Chama cha watoa huduma ya tiba ya dharura Tanzania (Emergency Medicine Association of Tanzania) wao wameelezea kama watu watatumia barakoa za vitambaa basi wanapaswa kushona kwa kutumia kitambaa kigumu aina ya kitenge na sio kitambaa aina ya Polyester (Polyester Fabric).
Ushauri wangu, Serikali au mamlaka za afya zitoke hadharani ituambie tathimini ya upatikanaji wa barakoa za N95 , Surgical masks na FFPI ,Kama barakoa hizi zipo serikali itoe bei elekezi na idhibiti bei namna inavyopaswa bei kuwa.Kama upatikanaji wa barakoa hizo ni mgumu na ni ghali ndio sasa watu waambiwe kwa maelekezo kama wanaweza tumia barakoa za vitambaa na waambiwe kwa maelekezo ya serikali aina ya vitambaa hivyo.
Mimi siamini sana katika Barakoa za vitambaa ingawa kukiwa hakuna jinsi inabidi tutumie tuu kama kimbilio la mwisho (The last resort). American lung Association wanasema "Cloth masks are not effective at blocking particles of virus in Droplets as surgical,still they did provide protection" . barakoa za vitambaa hazizuii sana ila sio sawa na kutovaa kabisa.
Naomba pia nimpongeze Shangazi Maria Sarungi kwa kuibua mjadala hii inaonesha namna gani yupo concerned na jamii yetu juu ya ugonjwa huu ,ingawa mimi kukubaliana na hoja yake itakuwa ni kimbilio la mwisho.
Shukrani sana .
Abdul Nondo.
Mwenyekiti Ngome ya Vijana ,Act wazalendo.
Sent using Jamii Forums mobile app