Mjadala kupinga adhabu ya kifo nchini. TLS yajali utu, yaonesha njia. Adhabu hii ifutwe

Mjadala kupinga adhabu ya kifo nchini. TLS yajali utu, yaonesha njia. Adhabu hii ifutwe

Wanabodi,

View: https://www.youtube.com/live/clOESBBmMmI?si=WZKqn4KF5vTxrtGR

Leo Tarehe 10 October ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo. Niko hapa jengo la Wakili House kuwaletea live mjadala kuipinga adhabu ya kifo nchini, ulioandaliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, TLS.

Kiukweli TLS imeonyesha kujali utu wa mtu, yaonyesha njia ya kuachana na adhabu hii ya kikatili, na kiukweli adhabu hii Ifutwe kabisa ni very barbaric, very unfair, it's inhuman, cruel and degrading human dignity!.

Mgeni Rasmi ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pindi Chana.

Kongamano limeanza, Rais wa TLS, Harold Sungusia, anazungumza.

Karibu

Paskali
Rejea

Hiyo adhabu huwa inatekelezwa au ni mambo ya mijadala ya wasomi ya kupoteza muda?
 
Hii Adhabu isifutwe Ten iboreshwe zaidi Wauaji wauliwe kwa Njia tofauti tofaut zinazovutia ili Iwe fundisho kwa wengine.

Njia ambzo mimi napendekeza ni Hizi
1. Kukatwa kichwa kwa kisu kama Kuku

2. Kupewa Sumu inayoua taratibu kuanzia siku 5-10 ili apitie mateso siku kadhaa

3. Kuingizwa kwenye Mashine yenye mfano wa Kusagia mahindi mtu aingizwe humo asagwe mpak kufa.

Etc,.... adhabu hiz zitolewe huku Ndugu wa upande wa Muuaji wakiwa wanashuhudia ten kwa lazima ili kujenga jamii itakayoheshimu Maisha ya Mtu mwingne.
Naunga mkono hoja. 🤝
 
Wanabodi,

View: https://www.youtube.com/live/clOESBBmMmI?si=WZKqn4KF5vTxrtGR

Leo Tarehe 10 October ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo. Niko hapa jengo la Wakili House kuwaletea live mjadala kuipinga adhabu ya kifo nchini, ulioandaliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, TLS.

Kiukweli TLS imeonyesha kujali utu wa mtu, yaonyesha njia ya kuachana na adhabu hii ya kikatili, na kiukweli adhabu hii Ifutwe kabisa ni very barbaric, very unfair, it's inhuman, cruel and degrading human dignity!.

Mgeni Rasmi ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pindi Chana.

Kongamano limeanza, Rais wa TLS, Harold Sungusia, anazungumza.

Karibu

Paskali
Rejea

Kamwe siungi mkono kabisa kuondolewa kwa adhabu ya kifo hapa Tanzania na hata katika nchi zingine zote kabisa, hususani nchi za Afrika. Sikubaliani kabisa na Hoja hii ya kufuta adhabu ya kifo.
Wapo baadhi ya Wahalifu wanastahili kupewa adhabu ya kifo, na pia wanastahili kunyongwa hadi kufa.
Matahalani, kwa hapa Tanzania kuna Askari Polisi wengi Sana wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu wa kupora Mali za raia na kisha raia hao wamekuwa wakiuawa makusudi ili kupoteza Ushahidi, watu wengi pia wamekuwa wakiuawa kwa makusudi wakiwa mikononi mwa Askari Polisi au wakiwa kwenye Vituo vya Polisi, na Wauaji wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote zile Kali za kuwapa fundisho juu ya uhalifu wao huo. Askari Polisi wamekuwa wakihusika katika uhalifu kama huo kwa kuwa Wana uhakika kuwa na wao hawatauwa badala yake wanahamisika zaidi na zaidi kuendelea kuua watuhumiwa. Mimi binafsi naamini kwa dhati kabisa kwamba Endapo kama Rais wa nchi hii angesaini Hati ya Kifo dhidi ya OCD Christopher Bageni, yule Askari Polisi aliyewaua kikatili wale Wafflanyabiashara wa madini kutoka huko Mahenge Morogoro, Basi Polisi wangeogopa kufanya matukio mengine ya uporaji na mauaji dhidi ya Wananchi.

Aidha, Endapo kama OCD Christopher Bageni angenyongwa hadi kufa Basi lile tukio la mauaji la Bw. Hamza Mohamed pale Selander Bridge Dsm kamwe lisingeweza kutokea, na hata yule Mfanyabiashara kijana wa madini kule Mtwara pia asingeweza kuuawa na wale Askari Polisi walioongozwa na OC-CID Kalanje.

Mwisho:
Namshauri Rais SSH akubali kusaini Hati ya Kifo ili aliyekuwa OCD Christopher Bageni aweze kunyongwa hadi kufa, kwa sababu Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani tayari zimeshatoa idhini na baraka zote kabisa kwamba mtu huyo anastahili kunyongwa hadi kufa. Huku mitaani kuna chuki kubwa sana dhidi ya hao Watu.
Endapo kama Rais anaona labda pengine kutokana na Imani yake ya kidini hawezi kusaini Hati za Kifo ili Watu hao wanyongwe, Basi namshauri AKASIMISHE MADARAKA hayo kwa Watu wengine walio chini yake ili waweze kutekeleza jukumu hilo kwa niaba yake.

Inakera Sana kwa kweli kuendelea kuwaona Watu wauaji ambao waliua wenzao kwa makusudi Halafu wao bado wanaachwa waendelee kufaidi maisha, Kamwe jambo hili halikubaliki hata kidogo.
 
Back
Top Bottom