Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Hizo ni changamoto ambazo zipo, na zisisababishe maisha yako yaharibike, hiyo ilikuwa ndoa ya baba yako na mama yako, una nafasi ya kutengeneza yako ambayo ni nzuri kuliko ya wazazi wako
Mahusiano tu wapenzi wangu tunashindwana sembuse Ndoa kabisa ? Hapo naona nitaleta madhara tu kama sio kumpotezea muda mwenza wangu.
 
Hiyo ni karma inatembea kwenye damu yako kutoka kwa baba yako na wahenga wako jitahidi umuombe Mungu amruhusu malaika wa karma aiondoe kwenye damu yenu na wewe ujifunze upendo kurekebisha hayo makosa.
 
Pole sana mkuu. Wazazi wako wote bado wapi hai?

Vipi mahusiano yako na baba ako yapo vipi
 
Ni bora ambavyo umechagua kutokuoa kwa sababu ukioa utataka kumlipia kisasi mama ako kwa ku compensate na kile ulicho shindwa kukifanya kwa mama ako ( kumtetea mama ako) ili kusatisfy your mind
 
Sababu yako naona ni nyepesi sana...Ina maana umechukua negative za ndoa lisa wazazi wako...Vipi Babu yako na Bibi waliokulea nao Ndoa walikuwa wanatesana? kwanini usingeamua kuchukua uamuzi kwa kuangalia hata Babu na Bibi basi
 
Wakuu habari

Ok nimefanya just a brief research kuhusu mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke

Nimegundua haya baada ya miaka 10 au 15 mbele

1. Swala la ndoa litakuwa sio jambo la maana tena haswa Kwa mtoto wa kiume ambae anao, hapa itakuwa ni mwendo wa kuzalisha watoto na kusepa, Yani hakuna ndoa.

2. Idadi ya single mother itaongezeka Kwa kiasi kikubwa sana kuliko Sasa, na litaonekana ni jambo la kawaida tu.

3. Mwanamke kuwa na watoto zaidi ya watatu na kila mtoto ana baba yake pia litakuwa ni jambo la kawaida katika jamii nyingi.

4. Mwanaume kumiliki wanawake zaidi ya watano , pia litakuwa sio jambo la kushangaza, na hii inasababishwa idadi ya wanaume ni ndogo kuliko wanawake

5. Wanaume tutakuwa kama wanyama wengine kama mbuzi, ng'ombe, jogoo , Yani kazi yetu itakuwa kuweka mbegu na kusepa, tena Kwa wanawake tofauti tofauti.

Haya mambo sio kwamba watu hawafanyi, ila Kwa projection ya baada ya miaka hiyo, hayo mambo yataongezeka Kwa kiasi kikubwa na itakuwa ni jambo la kawaida kuliko Sasa hivi
 
Wale team kataa ndoa naombeni mtupe sababu kubwa iliyoko nyuma ya hii kampeni.
Kwa busara zangu naamini kuna matukio mliyopitia hadi mnafikia maamuzi hayo.
Uwanja ni wenu sasa naombeni mtuambie mlikutana na nn hadi mkafikia hatua hiyo ya kukataa ndoa nisije nikajichanganya na mm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…