Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Kataa ndoa na single mother bora kuoa mama wa marehemu kuliko kuokota single mother
 
Umeanza vzr sana ila kwenye any way hapo UMEKUNYA MKUU[emoji23]
 
We jamaa!
utaruhusu mwanao wakiume wa miaka 25 akaoe mwanamke ambae amesha gonga ukuta wa miaka 35?

Hebu twende pole pole mama yako mzazi na dada zako watakuwa ok kabisa ukaenda kumtambulisha mke mtarajiwa kwenu ambae amekuzidi miaka 5? yaani alishaanza gegedwa na kutafunwa na CHEEK SLAYING WARRIORS MANY YEARS AGO WAKAT WEWE Hujui hata how to be a man?
 
Kaka semina yako unaifanyia wapi tuudhurie kaka😂😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
Usioe mwanamke anayekuzidi urefu. Hata kwa wanyama beberu siku zote anakuwa giant. Hata kuku hivyo hivyo jogoo anakuwa giant. Ukizidiwa urefu na mwanamke na confidence yako kama mwanaume inashuka
Kwa wanyama sawa ila kwa Binadamu tuna utashi flani hivi. Ilimradi una uanaume ndani yako unaweza kumcontrol hata awe mrefu kiasi gani..
 
Ukijijua wewe ni mwanaume dhaifu usioe kabis

Ukijijua wewe ni mwanaume dhaifu usioe kabisa😃😃👋
laws of attraction
mwanaume mdhaifu mara nyingi ananasa kwa toxic strong masculine woman.
kwaiyo wala huna haja ya kuwakumbusha wanaume wadhaifu.

nikuulize ? unajua sifa za wanaume ambao si wadhaifu? unawajua wakoje?
wasaidie wapo wengi humu hawajijui wanadhani wao ni strong masculine? but deep down wapo weak af
 
Pamoja na yoote uliyoandika Mkuu, Mimi naoa mwezi wa 3 panapo uhai, Napokea michango yenu, kuanzia Buku na kuendelea, baada ya ndoa Updates zitafuta.
 
HEBU vuta picha baba yako mzazi anapitia hii comment yako?
wow!
hahahaha naamini atajivunia.

You ain't got no game sis!
jarbu kuwafundisha wezio what it takes to attract a fine masculine man.
just be submissive and feminine enough to attract real men.
 
HER PAST BRO,
Huwa tunatizama historia yake bro
narudi wanaume huwa tunajali historia ya mwanamke hatujali kesho , hatujali atakuja kuwa tajir au nin!

wanawake huwa hawajali ulidate na nani body count yako ipoje, they don't give a damn about your excellent track record , your past behaviour mean nothing to her THEY ONLY BASE ON CURRENT ENERGY.

Her past will always come back and haunt you.
 
WANAOSEMA "KATAA NDOA" WANAHOJA NZITO.

Anaandika, Robert Heriel

Mimi ni mfuasi wa maadili ya kizamani. Na kama ni mfuasi wa maadili ya kizamani basi kwangu ndoa ni lazima.

Alafu kuna lile kundi la Wanausasa, kimsingi, kwenye Maadili ya Kisasa Ndoa haina umuhimu wowote. Ni Utapeli Mkubwa.
Ndoa ili idumu na ilete matokeo yaliyotarajiwa lazima itumie mfumo wa kizamani. Kwa sababu ndoa kama Ndoa ni mfumo wa kizamani.

Utakapotumia mfumo wowote wa kisasa kuendesha ndoa yoyote Ile lazima ndoa hiyo Ikwame.
Ndoa inahitaji Watu Wawili mwanaume na Mwanamke ambao wanafikra za kizamani ili idumu.

Kijana kama unaoa au kuolewa, elewa kuwa kama mwenza wako au wewe unamambo au fikra za usasa basi Ndoa hiyo itakushinda tuu!

Zifuatazo ni hoja za wanakampeni wenye Sera ya "KATAA NDOA" Ambazo hoja zao hata Mimi naziunga mkono Kwa 90%.

1. Mfumo wa sheria hausapoti Ndoa kudumu.
Sheria za nchi yetu na sheria za dini hasa Ukristo zinazohusu ndoa ni sheria zilizochanganya usasa na uzamani, Jambo ambalo linaleta machafuko ndani ya Ndoa.
Taikon kama ningekuwa mtunga sheria za ndoa basi Kwa hakika ningefuta sheria nyingi zenye kila dalili ya usasa.

Sheria ya haki Sawa,
Sheria za mgawanyo wa Mali wa pasu Kwa pasu Baada ya kuachana ilhali mtafutaji ni Mwanaume. Angalau zile familia ambazo Mwanamke naye anafanya kazi.
Sheria ya kumpa mamlaka Mwanamke kukopa Pesa Kwa jina la Mume wake.

2. Mmomonyoko wa Maadili ya kizamani, na kuzaliwa Kwa maadili Mapya ya hovyo.
Zamani ili mtu awe Mkeo na ndoa ifungwe sharti Mwanamke awe Bikra. Hiyo ni moja ya maadili ya ndoa.
Kukithiri Kwa Tabia za kimalaya, uasherati na tabia zingine za uzinzi kunawapa nguvu wenye Sera ya kukataa Ndoa.

Unaoa Mwanamke anakuwekea kibao kisemacho; " kwani wewe sio WA Kwanza wala sio wamwisho, wapo walionianza na watakaokuja kesho"

Uwepo wa Ma-ex lovers wa Mwanamke utakayemuoa una-play role kubwa katika ndoa yako.
Ni kawaida Watu kujidanganya.

3. Tamaa na uroho wa Pesa.
Ndoa za sasa zimejengwa katika mfumo wa tamaa na uroho wa Pesa na Mali.
Wakati ndoa za kizamani zimejengwa katika mfumo wa utu, heshima na Maadili.
Sio Mwanamke unayemuoa, sio wazazi utakaoenda kupeleka posa wote wanatamaa na uroho wa Pesa na Mali.
Unategemea nini hapo.
Hiyo ni biashara.
Mchakato wa kuanzisha mahusiano siku hizi ni pesa imewekwa Mbele,
Mchakato wa kutoa posa, Pesa Mbele,
Mchakato wa kufanya harusi, Pesa Mbele,
Mchakato wa kuachana ni pesa mbele na malumbano ya kugombea Mali.

Michakato yote na pessa na Mali mwanaume ndiye anapata Hasara, yaani ni pesa ya kijana ndio inaliwa.
Hivyo Vijana wa Kampeni ya KATAA NDOA wanayohoja NZITO.
Wanaona ndoa ni Utapeli, usukule, unyonyaji katika Zama za Leo.

Na kiukweli hatta Mimi Taikon nikisema niseme Kweli kabisa, basi hawa vijana wapo sahihi kuwa na mtazamo huo.

4. Hakuna Huduma ya maana ndani ya Ndoa.
Zamani Ndoa ilijengwa na Mama na Baba.
Baba alikuwa na jukumu la kuitunza familia, huku Mama akitoa malezi Kwa Watoto. Hii ilifanya Watoto wakue katika makuzi Mema yenye maadili (hili ndio lengo kuu la Ndoa)

Lakini ndoa za siku hizi hazina mfumo huo tena, Kwa sababu
I) Mama anatafuta na Baba anatafuta automatically hakuna Ndoa hapo.
ii) Mlezi wa Watoto ni Housegirls au Babysitter au
iii) Mtoto apelekwe Boarding School.
Mtoto akapewe malezi na watu Back Huko.

Wenye Kampeni ya KATAA NDOA wanahoja ya msingi.
Huduma pekee ya msingi iliyopatikana ndani ya Ndoa na ambayo haipatikani mahala popote pale ni malezi ya Baba na Mama Kwa Watoto wao.
Sasa Kama Watoto hawapati malezi ya Baba na Mama, umuhimu wa Ndoa unakosa nguvu.

Kama ni Ngono popote MTU atapata,
Kama ni chakula mama ntilie wapo,
Kama ni huduma za usafi, Housekeeper au Housemaid wapo,

Kitu pekee ambacho hata Mimi Taikon ninakiona kwenye Ndoa ni malezi ya Watoto wetu. Na kama malezi hayo hayapo, sasa umuhimu wa Ndoa ni upi?

Haya, Mama anatoa malezi lakini malezi yake yanakinzana na malezi ya Baba/mume.
Yaani mume au Baba anatoa maelekezo Watoto wafundishwe hivi na kukatazwa kile, Mama MTU anakataa, sasa hapo umuhimu wa Ndoa ni upi
Kwa MTU kama Taikon, huwaga hapo sina salia mtume.

5. Mashindano.
Ndoa ya kizamani imejengwa katika mfumo wa MKE kumtii mume, lakini ndoa za sasa nyingi zimejengwa kwenye misingi ya mashindano.
Kimsingi Sisi wanaume sio Watu wa mashindano. Yaani hatunaga wivu WA kijinga.
Lakini Wanawake ni Watu wa mashindano.

Unaoa Mwanamke anakushindanisha na watu wengine,
Mwenzako kajenga, sijui mwenzako kanunua Gari,
Sijui Watoto wa Fulani wanasoma Medium sijui boarding, naye anakushinikiza,
Huku akikununia, hakika Vijana kama kina Taikon hatutavumilia vioja vya kipuuzi kama hivyo.
Yaani tukose Utulivu na Amani kisa wivu wako wa kijinga.
Kama unataka nyumba au Magari ya haraka wafuate wanaume wenye magari au hizo nyumba, kwangu unasubiri nini.

Kampeni ya KATAA NDOA wanayohoja NZITO katika kipengele hicho kwani Vijana wanajua Maisha sio mashindano.
Fanya Kwa uwezo wako wote kisha utakachojaliwa shukuru.
Mambo ya kulinganishwa hayo hakuna.

Hata Mungu hataki kulinganishwa na kufananishwa au kushindanishwa.

6. Kupewa Majukumu yasiyoyako.
Ndoa za sasa sio ajabu Mwanamke anakuletea mtoto asiyewako anakuambia umpende kama mtoto wako. Kisha majukumu kama yote anakuachia utadhani huyo mtoto Hana Baba au Ndugu za Baba yake.
Ukimuambia mpeleke mtoto Kwa Baba yake au Kwa Ndugu zake halitaki.
Ni full Dharau,
Ndoa za kizamani, Mwanamke akitaka kuolewa anaacha Watoto Kwa Baba husika na sio kupeana majukumu yasiyo na kichwa wala miguu.
Wenye Kampeni ya kukataa Ndoa wanayohoja.
Hata Mimi naungana nao, kama Akili zenyewe ndio hizo bora ukatae tuu Ndoa.

7. Ubinafsi uliopitiliza.
Ndoa za kizamani Wanawake walijua thamani ya kuhudumiwa hata kama ni Kidogo waliridhika.
Lakini Wanawake wengi WA siku hizi ni wabinafsi wa kiwango cha lami.
Wanajifikiria wao tuu! Uwafanyie wao tuu! Alafu hata ukiwafanyia hawana shukrani, wanakuona hamnazo, HAKIKA! Vijana kwa Hali Hii mnayohaki ya kukataa Ndoa.
Na hii inatokana na Tabia za kimalaya Malaya, Mwanamke mwenye Silika ya umalaya hawezi kuwa na Shukrani. Kwa sababu anakulinganisha na pia anatamaa ya vitu vizuri na vingi Zaidi.

Yaani kijana uache Kula na kunywa na kuvaa vizuri unahangaika na jitu ambalo tena haukumkuta Kigoli na bado hakushukuru wala kukuheshimu, labda uwe hamnazo.

Binafsi nipo upande wa wafuasi wa Ndoa za kizamani. Na Sisi wenye mifumo ya kizamani tupo radhi tuoe kila Mwaka na kutoa talaka kila mwezi ikiwa Kanuni na mifumo yetu itaguswa bila kujali athari au matokeo yoyote Kutoka upande wowote Kwa MTU yeyote.
Tutafanya majukumu na wajibu wetu Kwa Watu wanaofuata mifumo ya Ndoa.

Ni Bora mara elfu 10 uishi pekeako kuliko uishi Kwa mateso na MTU Kwa kisingizio cha ndoa ya Kisasa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Angalizo; Haki na Wajibu ndio muhimu kuuzingatia. Usitweza Haki ya mtu wala usikubali MTU akakudhulumu Haki yako kama Mwanaume.

Nawatakia Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndoa nyingi za Modern zinafungwa kimhemko.

Mtu anaoa kwasababu ya uvivu kupika au kufanya usafi pindi akitoka katika mishuhuliko ya kazi.

Mtu anaoa kwasababu watu aliokuwa nao katika rika lake wengi wameoa.

Ikifika mwezi mmoja kabla ya kuufikia mwezi mtukufu utaona wimbi la ndoa nyingi zikifungwa. Hizo ndoa zote zimefungwa kwa ajili ya kufanya sex iliyo halali

Miezi kadhaa kupita baada ya kuizoea hali ndio wanagundua kumbe ndoa ni zaidi ya kupika na sex wanabaini wanacho ki face ni jambo geni ambalo hawakujipanga nalo before.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…