Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mimi nadhani labda wanataka waolewe wao!!!

Eeh,maana kama mtu ulitokana na ndoa na umekulia kwenye familia ukiwaona wazazi wako pamoja mpaka wamezeeka kinachokufanya usiowe ni nini?

Mfumo walioutumia wazazi wetu, Kanuni wanazozitumia ndani ya Ndoa mpaka wamefikisha uzee sio mfumo wa sasa na sio Kanuni za sasa zinazotumiwa na Vijana WA SASA.
Hiyo ndio Sababu ya hoja za wanao kataa ndoa.

Wewe huoni kuwa wanahoja?
 

Mwisho wanaamua kumwaga Sufuria
 
Duuh . . . .

Kweli umetutakia sabato njema kwa style ya aina yake.

Nakuunga mkono asilimia 100. Ili ndoa idumu lazima mwende kizamani. Ukileta usasa kwa hawa broilers umeliwa

Ndoa yenyewe ni mfumo wa kizamani alafu unataka uiendeshe kisasa huoni kama unatafuta matatizo mazito.

Vijana wawe watulivu, wasiendeshwe endeshwe kipumbavu,
Tunaowajibu wa kufundisha kizazi hiki jinsi ya kuishi Kwa HAKI
 
Mfumo walioutumia wazazi wetu, Kanuni wanazozitumia ndani ya Ndoa mpaka wamefikisha uzee sio mfumo wa sasa na sio Kanuni za sasa zinazotumiwa na Vijana WA SASA.
Hiyo ndio Sababu ya hoja za wanao kataa ndoa.

Wewe huoni kuwa wanahoja?
Sifa ya kwanza ya mwanaume ni ku-face reality wao wanakataa ndoa leo 2023 hao watoto wao wanaotaka kuzaa hovyo hovyo na mama huyu na mama huyu watakuzwa vipi,wao hao watoto watakuwa na bond gani kuwajenga kisaikolojia kwamba maisha ya familia yanakuwa hivi hayawi vile?

Watafute nao mfumo wao wa kuishi na hao wanawake kama baba zao walikuwa na mfumo wao muhimu ni uzao wa mtu ukue ktk maadili na kujielewa hatuwezi kuwa na kizazi cha mtoto huyu analelewa na house maid yule analelewa na shangazi itafika kipindi kwa sababu hawana mtu wa kuwafunza maadili mema watakuwa wanafanya mambo ya ajabu mitaani.
 

Kabla ya malezi ya mtoto lazima Mahusiano ya Baba na Mama yawe thabiti.
Na watu Wawili hawawezi ishi pamoja kama hawajapatana,
Na ili Watu wapatane lazima kuwa na sheria,
Na sheria zinajengwa kulingana na mfumo.

Ndoa ni mfumo wa kizamani, huwezi ingizwa sheria za kisasa au mfumo wa Kisasa.

Hata uishi na Mkeo au Mumeo kama hakuna Ndoa Watoto hawawezi Kukua kwenye Maadili.
Huwezi mfundisha mtoto maadili ikiwa ndoa imekushinda, hiyo haipo.

Mfumo ndio humjenga mtoto kuliko mafundisho
 
Africa haiwezekani na haifai kusema mtu hataki kuowa na kama hataki kuowa bora mara 1,000 asitake pia kuwa na mtoto kwa sababu hatuna mifumo stable kwa ajili ya kusaidia watoto wenye shida na wazazi.

Mfano kijana atakaposema hataki kuowa moja kwa moja ataiga uzungu wa kutaka kutafuta mwanamke amzalie watoto amlipe asiingiliane kwa namna yoyote na watoto sasa ikitokea huyu kijana hayupo hawa watoto watakaa ktk mazingira gani?ndugu wengi hatupendani sometimes unakuta ndugu wengine hata watoto wao kuwatunza hawawezi utegemee watoto wanaoranda randa mitaani hawataongezeka?

Na serikali zetu hizi za kiafrika hazina mifumo ya kutunza watoto wasiokuwa na wazazi hii si hatari sana maana wanaosema kuowa hawataki siyo matajiri useme wataacha mali za kuwasaidia watoto in case of anything ni maskini wengine watakufa hawana hata nguo ya pili si hawa watoto wataishia kwenye uchokoraa na wizi mtaani pamoja na ushoga kuongezeka!!!

Vijana acheni kuiga upumbavu wa wazungu siyo kila kitu ni cha kuiga ukitaka kuwa na kizazi bora kama ulivyo wewe ndoa huwezi kuikwepa.
 

Ikiwa hiyo haiwezekani basi Watu wafuate mfumo wa Ndoa za kizamani.

Kukataa mfumo WA kizamani hakuna tofauti na kuishi bila ya ndoa. Yaani yote ni sawasawa.
Zaidi kuishi kwenye Ndoa ya Kisasa ndio kuna matokeo mabaya zaidi.
 
Mkuu umechambua vizuri mno itafika kipndi ndoa zitajifia kabisa , kumbuka pia idadi ya wananchi wa tanzania itakuwa kubwa ni watoto wa ma single mother , ivi kunahitajika unabii gani apo kuona kifo cha ndoa?
 
Ndoa sio lazima kufanya harusi...
Mnaweza funga ndoa bila makelele wala karattasi za sheria...
Kama kuna waliokuelewa vijana watembee humu.

Kinacholeta shida Sasa hivi siyo ndoa, ni hizi harusi na haya makaratasi mnayoita cheti cha ndoa.

Ukiacha utajili wa CR7 tunamchukulia kama case study kwa sababu ni maarufu, yeye ana mke na Watoto lakini hana harusi wala ndoa.

Ili muishi Kwa raha mustarehe hawa wanawake wa toleo hili inatakiwa kuishi nao hivi na mtadumu sana.

Nilikuwa na Boss wangu mzungu naye ana mke na mtoto mmoja tena ni tajiri haswa lakini hana ndoa wala harusi.

Sijaelewa wanawake wengi ukishafunga nao ndoa na kusaini Yale makaratasi sijui wanapatwa na wazimu gani?
 
Kila mtu afanye maamuzi jambo jema ni kwamba hakuna sheria inayokufunga usipooa au kuolewa,
Sema hizi kampeni za kataa ndoa zimekaa kishoga.
Ikifikia wakati ndoa zikawa hazina maana zitachochea zaidi vitendo vya maadili mabaya kabisa
Tofautisha kati ya kuoa na kuoa kwa ndoa , nina mke ila sina ndoa kwa sababu ndoa ni utapeli.
 
Umenena vema mkuu.
 
Ndoa sio lazima kufanya harusi...
Mnaweza funga ndoa bila makelele wala karattasi za sheria...
Wao hoja yao siyo harusi au mkataba wanachokataa wao ni ile "kuishi pika pakua na mwanamke" kwamba watafute wanawake wawape hela kwa ili wawazalie watoto then baada ya hapo hakuna kujuana.
 
Mimi nimegundua kitu baada ya tafiti zangu mkuu.

wakataa ndoa wengi mara nyingi wanakuaga washauri wazuri sana kuhusu ndoa, kuliko wanaume ambao wameoa.
SIKU MOJA NILIBAHATIKA KUKUTANA NA MZEE MMOJA ALIKUWA ANASHUGHULIKIA KESI YAKE BAADA YA KUWA DIVORCED NA MKEWE,
alinieleza mengi.
"if you are single, just keep it that way"
 

Yeah! Kama haujapata MTU sahihi ni Bora ubaki single tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…