Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mengine yote sawa ila hoja number 4 haipo applicable kea kila familia.Zipo familia nyingi Sana hasa za vijijini ambazo hazina house girl Wala baby sitter.Na Mara nyingi katika ndoa hizo baba pekee ndio mtafutaji mama anakaa nyumbani kuwaangalia watoto na mengineyo.

Kikubwa Ni kumtafuta mwenza sahihi wa kuishi naye Kama mume/ mke.
 
mkuu

kamata mountain Dew, kunywa hata 100, mimi nalipa,
 
Kila mtu afanye maamuzi jambo jema ni kwamba hakuna sheria inayokufunga usipooa au kuolewa,
Sema hizi kampeni za kataa ndoa zimekaa kishoga.
Ikifikia wakati ndoa zikawa hazina maana zitachochea zaidi vitendo vya maadili mabaya kabisa
Umenena vizuri Sana mkuu
 
Kwa mabinti wa sasa bila harusi haoni kama kaolewa😂😂
Hapo ndipo shida inapoanzia
Usigeneralize. Tuko malegend tulioolewa kimya kimya braza. Tulitoka kanisani, tukaenda restaurant opposite na mlimani. Nikiwa nimevaa gauni la 35k la kariakoo. Tukala sisi na wazazi wetu pande mbili na baadhi ya mashem, wifi na dada kwa upande wangu. No photoshoot, no mc, no champagne, no cake. Kibingwa..af fresh. Na tunadunda tu. Kiroho safi.
 
Yeah! Kama haujapata MTU sahihi ni Bora ubaki single tuu
hawa wa generation z mkuu plus ka system kanawajaza ujinga.
kikubwa ni kuenjoy life na atakayekuwa tayar

asilimia kubwa vijana huwa wanafeli hapa.
"wana confuse own energy needs with commitment in love"
wanajikuta wanakuwa surprised when in few months, energy needs inachange,
mara boom wana wanajikuta walifanya superficial choice. ndoa zinavunjika/ usaliti na mengine kibao.

nachosema ndoa sio lazima now days. otherwise kama unaamua kutake risk. NA KWANN UTAKE RISK?
 
"Kataa ndoa, zaa hovyo"
Haya ni maneno ya waja...
 
Upo sahihi kwa asilimia kubwa “ ndoa kwa sasa ni mihemko ya vijana wajinga ”.
 
Mfumo walioutumia wazazi wetu, Kanuni wanazozitumia ndani ya Ndoa mpaka wamefikisha uzee sio mfumo wa sasa na sio Kanuni za sasa zinazotumiwa na Vijana WA SASA.
Hiyo ndio Sababu ya hoja za wanao kataa ndoa.

Wewe huoni kuwa wanahoja?
Mambo yame badilika sana sasa, ukiishi kizamani lazima mambo yakushinde. Kutokana na uzamani kwa sasa umepungua kwa kiwango kikubwa sana.
 
Kiwango cha mwanamke kujitambua huwa ni kidogo sana kutokana na umri alio nao.
 
Kijana kataa ndoa.

Ndoa ni utapeli.

Ndoa ni hatari kwa afya ya mwanaume.

Ndoa haimnufaishi mwanaume.
Ndoa ipo kwa ajili ya kumnufaisha mwanamke kwa sababu kwake ni ajira ya kudumu!

Ndoa humfanya mwanaume kufa mapema. Nimeona jinsi baba Mdogo alivyokufa kizembe.

Kataa Kabisa katakata!
Kataa kwa herufi kubwa na kwa sauti nzito ya kiume.
 
Mimi mambo yakikaa vizuri nitaoa lakini ni ile kwenda kumtolea mahari binti na kumchukua kwao kihalali ila upuuzi wa kusaini makaratasi ya sheria na kula kiapo kanisani sitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…