MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Usiongee usichokijua na pia unapo-quote mstari hebu uandike ili tunapopitia tuusome na tuelewe ulichokuwa unataka tujue..mfano Ufunuo 5:8 inasema: Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana - Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato ambayo ni maombi ya watakatifu.''
ehe..Ulitaka kusema nini juu ya Mstari huo kwa kufuatana na maelezo ya Mwanadamu kuchukua nafasi ya Yesu Kristo kupitisha maombi yetu..
Hebu wewe nieleze....Sitaki kurudia mara kumi kumi kitu kile kile.....

Wewe unafikiri hao wazee 24 na wale 4 ni nyanya zako wako dongobeshi...?
 
Yn.14:6 inasema: 'Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi'....Yesu Kristo peke yake ndiye njia ya kumfikia Mungu Baba, hakuna mtu mbadala wala mwingine aliye kiunganishi kati ya mwanadamu na Mungu Baba. Huo mstari ndiyo tafsiri yake kwa ufupi...Haya..elezea Mstari gani unampa mwanya mtu mwingine zaidi ya Masihi...Yesu Kristo Kumfikia Mungu Baba ..!
Ndio maana nikasema apa panahitatajika Taaluma Mungu(THEOLOGY) huwezi kuelewa hili jambo,ila kwa kifupi Wakatoliki hawamwombi Maria/Watakatifu direct Bali wanamwomba Mungu kwa njia ya mwanae Yesu Kristo na pia wanakazia sala zao kupitia watakatifu akiwemo Maria Mtakatifu mama wa Mungu,njoo na Uzi unaohusu mambo haya kisha tutakuja,ila Taaluma Mungu muhimu sana kwako na mengine style yako.
 
Ni kwl mkuu nina mjomba wangu ni padri nilienda kumtembelea pale ofcn kwao kurasini nkakuta friji yake imejaa mivinyo plus bia za kutosha akawa anapga bia kama kawaida kwhyo kwa mujibu wa biblia yao pombe kwao ni halali kbsa sikushangaa hata maparoko huwa wananyonya sana mivinyo
Leta mistari ya bible iliyozuia mvinyo
 
4a15e6a294979733a35e7f26aee11d13.jpg
 
Yn.14:6 inasema: 'Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi'....Yesu Kristo peke yake ndiye njia ya kumfikia Mungu Baba, hakuna mtu mbadala wala mwingine aliye kiunganishi kati ya mwanadamu na Mungu Baba. Huo mstari ndiyo tafsiri yake kwa ufupi...Haya..elezea Mstari gani unampa mwanya mtu mwingine zaidi ya Masihi...Yesu Kristo Kumfikia Mungu Baba ..!
Wivu mbaya jamani. Kwani ulimwomba bwana Yesu kupitia kwa MAMA Maria ni Dhambi???!
 
Eee! Unaelewa maana ya huo Mstari..unajua alikuwa anamaanisha nini? Mwanamke ni nani huyo?...Jua na mwezi zinawakilisha nini? Taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake ni nini hicho?
Usimeze mistari tu bila kujua maana yake..!
Laiti ungejua hata hiyo tafsiri unayoamini chanzo chake ni nini usingeangaika kumshangaa mwenzako....kwani nini unaamini tafsiri yako ni sahihi na huyu ni potofu? Mchungaji wako? Tumieni akili kwenye vitu vinavyohitaji akili tu!
 
Alafu ili kulibeza Kanisa Katoliki Walokole wengi wanambeza sana Bikira Maria....wanasahau Yesu ni Mungu kweli na Mtu kweli ....sijui wewe utajisikiaje watu wakimkejeli mama yako .....Pale anaposema vizazi vyote wataniita mbarikiwa bila Kanisa Katoliki kwa mwenendo wa makanisa ya sasa angeitwa mbarikiwa ili hilo neno litimie?

Nilichojifunza jamii ya Walokole wengi elimu ya Kimungu hawaijui. Ndio maana hata ukweli wakati mwingine wanaupinga.
 
Ndg yangu cjui umenipata concept yangu....?biblia imeandikwa na Mungu kupitia watu wake hata hiyo barua ya pili ya kichungaji kutoka kwa Paul kwenda kwa Timotheo mstari 3:16-17 ujaweza kuutumia vzuri,mm namaanisha biblia ya Kikatoliki yenye vitabu 73 imejaribu kumrahisishia msomaji aweze kupata mahudhui kirahisi zaidi kwani wanaanza na mhutasari kwenye kila kitabu kisha unaanza kusoma kitabu husika,NB:Unajua historia ya kuandikwa biblia...?Je unajua biblia ya kwanza iliandikwa kwa lugha gani...?Kwann Leo waprotestant biblia yao INA vitabu 66....?Kwann Leo wayahudi biblia yao INA vitabu 39....? na kwann Leo Wakatoliki biblia yao INA vitabu 73....?ndg hv ni vtu muhimu sana kabla ujaanza kunukulu barua za Paul kwa Timotheo.
Jambo la muhimu kutambua ni kuwa Biblia iliandikwa na watu waliipewa ufunuo na Mungu na pia walivuviwa na Roho Mtakatifu ili katika mazingira yao wakati huo waandike kwa usahihi kile walichofunuliwa na Mungu ili kiweze kufaa kwa mafundisho. Andiko nililonukuu kutoka kwa Paulo linathibitisha hilo. Kwa akili ndogo ti, je hapo Mtume Paulo alikuwa anazungumzia maandiko yapi? Ni wazi kuwa kumekuwapo utaratibu wa kuhifadhi maandiko ya Mungu kwa utaratibu ulioongozwa na Roho Mtakatifu. Kuanzia Mwanzo, Mungu aliongoza uhifadhi wa maandiko hata Yesu alipokuja alinukuu Maandiko ya wakati huo, Mitume pia walinukuu Biblia hiyo hiyo.Tangu awali sio kila kitu kilichofanywa na manabii au wafalme wa Israeli kiliandikwa kwenye Biblia, ukisoma vitabu vya wafalme wa Israel utaona hilo jambo limesemwa. Hata wakati wa agano jipya, utaratibu ulitumika huo huo. Yaani Mungu anawafunulia na kuwavuvia waandishi ili kuandika kile kilichokuwa cha msingi kwa wokovu wetu. Hili limefanyika kabla ya kanisa kuungana na upagani wa kirumi ambao walianza kupotosha maandiko chini ya kanisa la roman catholic. Na ndio maana Wakristo waaminifu waliihifadhi Biblia halisi tuliyonayo leo. Cha ajabu kanisa la roma linajipa mamlaka ya kuandika Biblia jambo ambalo si kweli. Kanisa la roma halitaki kukiri kuwa Biblia ilikuwepo tangu enzi za manabii na zaburi, Yesu aliitumia Biblia hiyo ikiwa na agano la kale. Kanisa la mitume likaendekeza kazi hiyo na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, vitabu 27 vya agano jipya vikachaguliwa kukamilisha Biblia ya vitabu 66. Kumbuka hii ni kazi ya Mungu, mtu yeyote asijisifu. Na yote yaliyo katika Biblia hii, yafaa kwa mafundisho na kwa wokovu wa mwanadamu.
 
Ndio maana nikasema apa panahitatajika Taaluma Mungu(THEOLOGY) huwezi kuelewa hili jambo,ila kwa kifupi Wakatoliki hawamwombi Maria/Watakatifu direct Bali wanamwomba Mungu kwa njia ya mwanae Yesu Kristo na pia wanakazia sala zao kupitia watakatifu akiwemo Maria Mtakatifu mama wa Mungu,njoo na Uzi unaohusu mambo haya kisha tutakuja,ila Taaluma Mungu muhimu sana kwako na mengine style yako.
Mnakazia maombi! Kwa andiko lipi? Ndiyo maana Luther aliwapinga mlipoanza kuchakachua Biblia. Mungu anasema "Neno lake litasimama".
 
Hiyo ndio sababu iliyomfanya aondoe vitabu 7 vya Agano la Kale....

Hiyo ndio sababu iliyomfanya atake kuondoa vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania..

Hebu nipe sababu kama unaijua, uniambia aliviondoa kwa mamlaka ya nani...??
Sasa kwa taarifa yako, sio Luther pakee aliyepinga hayo maandiko mnayodai yalifichwa. Wana matengenezo wote walipinga uovu huu wa kanisa la roma kuongeza vitabu ambavyo havikuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu. Nia ovu ya kanisa la roma ilishindwa na itashindwa milele kwani neno la Mungu litadumu milele bila kuchakachuliwa. Roma iliongoza kuchoma Biblia halisi ili walete ya kwao bandia lakini wameshindwa. Mungu mwenyewe amehifahi Biblia yake, na hii ndio inamfunua Kahaba mkuu wa ufunuo 17:15. Roman Catholic.
 
Nani kakudanganya...?na biblia haitakiwi isomwe mstari kama mnavyofanya wasabato kisha mnaibuka na matusi,biblia ni fasihi ya hali ya juu mno,mf:Kitabu cha Daniel unatakiwa ujue historia ya kitabu,kwann Daniel anakuwa main character,ukifuatilia biblia za wakatoliki huwa kila kitabu kinaanza na historia ya kwamba kiliandikwa BD/AD na mtajwa kwenye kitabu husika ni kwann amekuwa main character na mahudhui ya kitabu kwa jamii za ulimwengu,ndg zanguni msisome biblia mstari tuu kisha mkaja na maswali na majibu,ebu angalieni babu yenu William Miller aliyetabiri ujio wa Yesu Kristo 1844....!hiyo aibu wasabato hamjawahi kuifuta na huku mkipambana na kanisa mama,kanisa lililoachwa na Yesu mwenyewe Roman Catholic.
Yesu aliacha kanisa katoliki lini? Wakristo wenzangu hamna tofauti na walevi.
 
Rejea hapo kwenye bold.Mimi naamini Biblia moja tu yenye pumzi ya Mungu 2 Timotheo 3:16-17. Hizo za waroma baki nazo ninyi huko mwendelee kudanganyana.
Kwani hiyo Biblia unayoisoma wewe ni nani walikusanya maandiko na kuyaweka pamoja na kuipata biblia? Ukiweza kulijuwa hili utakuwa umefahamu kitu kikubwa na hitolikebehi tena kanisa katoliki.
 
Baada ya kusoma nyuzi zote hapo juu, sema maneno haya kwa dhati:

"Mungu baba, nakuja mbele zako, Mimi ni mwenye dhambi. Natubu dhambi zangu zote, kwa maana ya kuziacha kabisa. Naomba rehema na neema zako Mungu zinifunike. Sitaki dhambi tena kuanzia sasa. Bwana Yesu, nisafishe kwa damu yako iliyomwagika msalabani. Asante kwa kunisafisha n.a. kunisamehe dhambi zangu. Ni katika jina la Yesu Kristo ninaomba. Ameni."

Asante kwa kusoma sala hii kwa dhati; Mungu amekusamehe dhambi zako zote. Na sasa wewe ni kiumbe kipya na umeokoka.
Hivi ndivyo mnavyowadanganya mapunguwani wenzenu huko kwenye NGO zenu?

Insanity, binadamu akusamehe dhambi kwenye thread za JF, ndio maana Waislamu huwa wanaamini kuna tatizo kwenye akiri za wakristo "Uchwara"
 
Back
Top Bottom