MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Hebu wewe nieleze....Sitaki kurudia mara kumi kumi kitu kile kile.....

Wewe unafikiri hao wazee 24 na wale 4 ni nyanya zako wako dongobeshi...?
 
Ndio maana nikasema apa panahitatajika Taaluma Mungu(THEOLOGY) huwezi kuelewa hili jambo,ila kwa kifupi Wakatoliki hawamwombi Maria/Watakatifu direct Bali wanamwomba Mungu kwa njia ya mwanae Yesu Kristo na pia wanakazia sala zao kupitia watakatifu akiwemo Maria Mtakatifu mama wa Mungu,njoo na Uzi unaohusu mambo haya kisha tutakuja,ila Taaluma Mungu muhimu sana kwako na mengine style yako.
 
Leta mistari ya bible iliyozuia mvinyo
 
Wivu mbaya jamani. Kwani ulimwomba bwana Yesu kupitia kwa MAMA Maria ni Dhambi???!
 
Eee! Unaelewa maana ya huo Mstari..unajua alikuwa anamaanisha nini? Mwanamke ni nani huyo?...Jua na mwezi zinawakilisha nini? Taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake ni nini hicho?
Usimeze mistari tu bila kujua maana yake..!
Laiti ungejua hata hiyo tafsiri unayoamini chanzo chake ni nini usingeangaika kumshangaa mwenzako....kwani nini unaamini tafsiri yako ni sahihi na huyu ni potofu? Mchungaji wako? Tumieni akili kwenye vitu vinavyohitaji akili tu!
 

Nilichojifunza jamii ya Walokole wengi elimu ya Kimungu hawaijui. Ndio maana hata ukweli wakati mwingine wanaupinga.
 
Jambo la muhimu kutambua ni kuwa Biblia iliandikwa na watu waliipewa ufunuo na Mungu na pia walivuviwa na Roho Mtakatifu ili katika mazingira yao wakati huo waandike kwa usahihi kile walichofunuliwa na Mungu ili kiweze kufaa kwa mafundisho. Andiko nililonukuu kutoka kwa Paulo linathibitisha hilo. Kwa akili ndogo ti, je hapo Mtume Paulo alikuwa anazungumzia maandiko yapi? Ni wazi kuwa kumekuwapo utaratibu wa kuhifadhi maandiko ya Mungu kwa utaratibu ulioongozwa na Roho Mtakatifu. Kuanzia Mwanzo, Mungu aliongoza uhifadhi wa maandiko hata Yesu alipokuja alinukuu Maandiko ya wakati huo, Mitume pia walinukuu Biblia hiyo hiyo.Tangu awali sio kila kitu kilichofanywa na manabii au wafalme wa Israeli kiliandikwa kwenye Biblia, ukisoma vitabu vya wafalme wa Israel utaona hilo jambo limesemwa. Hata wakati wa agano jipya, utaratibu ulitumika huo huo. Yaani Mungu anawafunulia na kuwavuvia waandishi ili kuandika kile kilichokuwa cha msingi kwa wokovu wetu. Hili limefanyika kabla ya kanisa kuungana na upagani wa kirumi ambao walianza kupotosha maandiko chini ya kanisa la roman catholic. Na ndio maana Wakristo waaminifu waliihifadhi Biblia halisi tuliyonayo leo. Cha ajabu kanisa la roma linajipa mamlaka ya kuandika Biblia jambo ambalo si kweli. Kanisa la roma halitaki kukiri kuwa Biblia ilikuwepo tangu enzi za manabii na zaburi, Yesu aliitumia Biblia hiyo ikiwa na agano la kale. Kanisa la mitume likaendekeza kazi hiyo na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, vitabu 27 vya agano jipya vikachaguliwa kukamilisha Biblia ya vitabu 66. Kumbuka hii ni kazi ya Mungu, mtu yeyote asijisifu. Na yote yaliyo katika Biblia hii, yafaa kwa mafundisho na kwa wokovu wa mwanadamu.
 
Mnakazia maombi! Kwa andiko lipi? Ndiyo maana Luther aliwapinga mlipoanza kuchakachua Biblia. Mungu anasema "Neno lake litasimama".
 
Hiyo ndio sababu iliyomfanya aondoe vitabu 7 vya Agano la Kale....

Hiyo ndio sababu iliyomfanya atake kuondoa vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania..

Hebu nipe sababu kama unaijua, uniambia aliviondoa kwa mamlaka ya nani...??
Sasa kwa taarifa yako, sio Luther pakee aliyepinga hayo maandiko mnayodai yalifichwa. Wana matengenezo wote walipinga uovu huu wa kanisa la roma kuongeza vitabu ambavyo havikuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu. Nia ovu ya kanisa la roma ilishindwa na itashindwa milele kwani neno la Mungu litadumu milele bila kuchakachuliwa. Roma iliongoza kuchoma Biblia halisi ili walete ya kwao bandia lakini wameshindwa. Mungu mwenyewe amehifahi Biblia yake, na hii ndio inamfunua Kahaba mkuu wa ufunuo 17:15. Roman Catholic.
 
Yesu aliacha kanisa katoliki lini? Wakristo wenzangu hamna tofauti na walevi.
 
Rejea hapo kwenye bold.Mimi naamini Biblia moja tu yenye pumzi ya Mungu 2 Timotheo 3:16-17. Hizo za waroma baki nazo ninyi huko mwendelee kudanganyana.
Kwani hiyo Biblia unayoisoma wewe ni nani walikusanya maandiko na kuyaweka pamoja na kuipata biblia? Ukiweza kulijuwa hili utakuwa umefahamu kitu kikubwa na hitolikebehi tena kanisa katoliki.
 
Hivi ndivyo mnavyowadanganya mapunguwani wenzenu huko kwenye NGO zenu?

Insanity, binadamu akusamehe dhambi kwenye thread za JF, ndio maana Waislamu huwa wanaamini kuna tatizo kwenye akiri za wakristo "Uchwara"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…