MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Nilichojifunza jamii ya Walokole wengi elimu ya Kimungu hawaijui. Ndio maana hata ukweli wakati mwingine wanaupinga.
Umekosea ndugu, Unataka Elimu gani ambayo itakuthibitishia kuwa jamii ya watu waliokoka wengi hawana Elimu ya Kimungu, Nadhani hoja yako uliyoiweka kwenye forum hii inahitaji michango ya wengi na usizuie uchangiaji wao, Kikubwa kinachoangaliwa hapa ni Je Biblia ndiyo msingi wa michango hiyo..? kama siyo Je madhara yake ni yapi? Maana unapopingwa na ulichosema inamanisha aidha wewe mwenyewe hujui ulichokisema msingi wake au unajua ila umejiapisha kutokubadilika.
 
Great..
 
Hebu tupe tafsiri yako ili kujenga uelewa zaidi na kama ni tofauti utapingwa tu..maana Biblia itabaki kuwa ilivyo na tafsiri za wanadamu zitabaki kuwa tafsiri...karibu
Umekariri ...kwa taarifa yako Biblia yenyewe haijipi mamlaka mnayoipa ....hivyo ukiamua kubaki na kuamini kilichoandikwa tu si mbaya ila yapo mengi hayakuandikwa. Kanisa Katoliki ndio lililofanya juhudi za kukusanya vitabu na kuvichambua vipi viwe sehemu ya Biblia kwa muongozo wa Roho Mtakatifu .....kazi hiyo haikuishia hapo ...bado Roho Mtakatifu analiongoza hata sasa kama walivyopata maono ya kuhifadhi neno la Mungu....Biblia yenyewe inakiri kwenye 1Timothy 3:15 " This is the church of living God, which is the PILLAR and FOUNDATION of the TRUTH" .....Kanisa muongozo mkuu ni Roho Mtakatifu na Biblia ni sehemu ya msingi wa imani....
 
Kwani kina nani wanamuomba Mungu kupitia njia tofauti na Yesu.....?ebu tuambie na utuzdhibitishie hilo.....!nakusubiri.
 
Great kwa lipi...?kwa upotoshaji...?Upagani wa Roman Catholic ni upi haswa.....?Je unazungumzia vile vitabu 7 vya Deuterocanony....?kama ndio unajua historia yake....?katika safari yako ya usomaji ulishawahi kuvisoma vile vitabu...?kama bado nenda kavisome kama tayari vitabu vile vinapinga ya Mungu.....?na mwisho unajua historia ya hivyo vitabu yani kwann havipo kwenye biblia ya Wayahudi/Waprotestant.....?
 
Kwani kina nani wanamuomba Mungu kupitia njia tofauti na Yesu.....?ebu tuambie na utuzdhibitishie hilo.....!nakusubiri.
Kama na wewe unaomba kupitia Yesu Kristo basi uko sawasawa na Biblia na hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo Biblia inasema Yn.14:6
Nadhani tusipindishe, Yako uliyoeleza nakubaliana nawe..Kwamba Kanisa linaongozwa na Roho Mtakatifu...Nakubaliana nawe kabisa..Lakini unaposema Biblia ni sehemu ya msingi wa imani...hapo tutataofautiana..Kwanini, Kwasababu Biblia siyo sehemu...hapana!! Ndiyo haswa Msingi kamili wa Imani ya Kikristo na Roho Mtakatifu anapokuelekeza kufanya anakuelekeza ufuate kilichoandikwa kwenye Biblia..na ndiyo Maana Maandiko yanasema wazi kuwa asiwepo mtu wa kuondoa hata yodi moja ya neno Katika Biblia ili ule Msingi usiyumbishwe na matakwa ya watu..na hii tunaishuhudia hata sasa kuoona waalimu, manabii, wachungaji wanapotosha kilichoandikwa kwenye Biblia na kuaminisha watu kuwa ndivyo ilivyo, Mifano ni mingi, tunaweza kupata forum nyingine kueleza.
 
Great...kwamba ameelezea vizuri...hebu elezea hivyo vitabu umevieleweje na vinatoa tafsiri gani..?
 
Nadhani tuiangalie Biblia inasemaje..
inasemaje kuhusu nini..??

Theology isikufunge maana hiyo siyo Maandiko,
Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...

We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
 
Wewe umeniuliza nini na mimi nimekujibu nini..? Nimekujibu ulichoniuliza....
Basi tusigombane katika haya, nadhani forum hii ni kwa ajili ya kueleweshana ili kujenga uelewa mzuri zaidi, inawezekana mmoja akawa na uelewa zaidi au mdogo lakini mwisho wa siku ataelewa naye..ukichukia unaweza ukatunyima hata yale mazuri ambayo bado hujayasema hapa, naamini hivyo.
 
inasemaje kuhusu nini..??

Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...

We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
Ndugu una uhakika gani kama mimi siijui theology au credentials zangu unazijua? Naona tusimamie Biblia inavyosema na wengine wapate kuelewa, usiwe na hasira, rudi kwenye nafasi yako vizuri, elezea nasi tutakusoma na kukuelewa, Kule kwenye jokes forum wala hutaweza kuniona maana siyo eneo langu. asante
 
Kama na wewe unaomba kupitia Yesu Kristo basi uko sawasawa na Biblia na hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo Biblia inasema Yn.14:6
Kuna mtu alikataa...? Umeshawahi kuona jinsi sala za Katoliki zinavyoishia...?? Umeshawahi sikia maneno yanatamkwa mwishoni...??


Nadhani tusipindishe,
Nani anapindisha...??


..Lakini unaposema Biblia ni sehemu ya msingi wa imani
Sasa unadhani bila biblia huyo Yesu ungemjuaje...??
...hapo tutataofautiana..
Kwanini tutofautiane.. ??

Martin Luther sio aliondoa yodi moja ila aliondoa vitabu 7 vya Agano la Kale...
 
inasemaje kuhusu nini..??

Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...

We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
Midhaha tena! Jokes..why so?...Nadhani si vizuri kumtafsiri mtu ambaye hujui credentials zake..kama hukubaliani na nilichosema wala haikuzuii kuacha na kusema unachokiamini.
 
Haijalishi ni Martin Luther au Yeyote yule ambaye kwa kujua au kutokujua aliondoa hata yodi moja, Biblia inasema Ole wake!
Na ndiyo maana ukisoma Torah ya Wayahudi (Books of Moses)...utagundua vitu vingi vinakinzana na hizi tafsiri za Kisasa...Kuna watu watahukumiwa kwa kuondoa maneno kadha kwenye Biblia na haijalishi ni wewe au Luther au Roman authorities...Issue hapa Biblia ibaki kuwa Msingi wa yote. Yako mengi tunaweza kuyaongea lakini niishie hapo.
 
Hii suppport yako kwa huyo jamaa inamashaka matupu...Wote nyie mna ombwe la historia sahihi..
Inawezekana, Maana Biblia ni pana na historia yake ni ndefu..ila itabaki kuwa Msingi wa yote maadamu Roho Mtakatifu yupo wa kutuongoza.Miaka iliyodumu ni mingi kuliko miaka yangu, Kwahiyo uelewa wangu unaweza kuwa na kikomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…