Jambo la muhimu kutambua ni kuwa Biblia iliandikwa na watu waliipewa ufunuo na Mungu na pia walivuviwa na Roho Mtakatifu ili katika mazingira yao wakati huo waandike kwa usahihi kile walichofunuliwa na Mungu ili kiweze kufaa kwa mafundisho. Andiko nililonukuu kutoka kwa Paulo linathibitisha hilo. Kwa akili ndogo ti, je hapo Mtume Paulo alikuwa anazungumzia maandiko yapi? Ni wazi kuwa kumekuwapo utaratibu wa kuhifadhi maandiko ya Mungu kwa utaratibu ulioongozwa na Roho Mtakatifu. Kuanzia Mwanzo, Mungu aliongoza uhifadhi wa maandiko hata Yesu alipokuja alinukuu Maandiko ya wakati huo, Mitume pia walinukuu Biblia hiyo hiyo.Tangu awali sio kila kitu kilichofanywa na manabii au wafalme wa Israeli kiliandikwa kwenye Biblia, ukisoma vitabu vya wafalme wa Israel utaona hilo jambo limesemwa. Hata wakati wa agano jipya, utaratibu ulitumika huo huo. Yaani Mungu anawafunulia na kuwavuvia waandishi ili kuandika kile kilichokuwa cha msingi kwa wokovu wetu. Hili limefanyika kabla ya kanisa kuungana na upagani wa kirumi ambao walianza kupotosha maandiko chini ya kanisa la roman catholic. Na ndio maana Wakristo waaminifu waliihifadhi Biblia halisi tuliyonayo leo. Cha ajabu kanisa la roma linajipa mamlaka ya kuandika Biblia jambo ambalo si kweli. Kanisa la roma halitaki kukiri kuwa Biblia ilikuwepo tangu enzi za manabii na zaburi, Yesu aliitumia Biblia hiyo ikiwa na agano la kale. Kanisa la mitume likaendekeza kazi hiyo na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, vitabu 27 vya agano jipya vikachaguliwa kukamilisha Biblia ya vitabu 66. Kumbuka hii ni kazi ya Mungu, mtu yeyote asijisifu. Na yote yaliyo katika Biblia hii, yafaa kwa mafundisho na kwa wokovu wa mwanadamu.