Ndugu yangu...''tunanyweshana detto na dawa ya mbu makanisani kwetu?....wapi hiyo umenishuhudia, kwanini usitumie hii forum kufundisha na kuelewesha bila kushambulia kwa maneno makali namna hii. Detto imekuwa juice? Maandiko yanasema usitukane wengine, Nina imani unaamini ulichokiandika hakiendani na Biblia unayoiamini...inasemaje kuhusu nini..??
Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...
We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
Akasome historia upyaHii mada wenyewe wakiiona hapata tosha
Ameelezea vzuri kvp....?Nimeuliza upagani Roman Catholic ni upi haswa haswa naomba kueleweshwa apo ndg....?Vitabu vile vina mafundisho mazuri mno binafsi nilikuwa mpinzani kama wewe lkn baada ya kuvisoma nikagundua kuwa waliovingiza na na kuwa miongoni mwa vitabu ktk biblia takatifu hawakukosea,tusiwe wapinzani tuu na sisi tufuatilie,baadae nikitoka ofisini nitajaribu kukudavulia japo kdogo.Great...kwamba ameelezea vizuri...hebu elezea hivyo vitabu umevieleweje na vinatoa tafsiri gani..?
Ameshindwa kujibu. Kwetu dini zimeletwa. Na waumini wengi wanafikiri kuwa dini zilishuka kama tulivyoletewa. Kwa mfano Yesu aliishi mashariki ya kati. Yeye na wanafunzi wake walifuata dini na mila za kiyahudi. Na baada ya Yesu kuondoka, wanafunzi wake walisambaa katika maeneo yaliokuwa na jumuia za kiyahudi. Na wanafunzi wake walikuwa ni waumini wa kiyahudi na walifuata desturi za kiyahudi. Hivyo ilichukua muda kwa Ukristo kujitenga kutoka kwenye uyahudi.Umemuuliza maswali magumu sana sidhani kama atajaribu hata kukujibu.Hawa vijana wa seminari wamezoea kukaririshwa rozari tu.
Umemuuliza maswali magumu sana sidhani kama atajaribu hata kukujibu.Hawa vijana wa seminari wamezoea kukaririshwa rozari tu.
Ubani ulikuwa utatumika kuondoa harufu mbaya. Kwa mfano mtu akij@mb@Anaekimbia kathoric nakuludi alikuwa kakimbizwa na mapepo nasasa kapona ana amua kudi.. Lkn ninawaambia ubani hauwezi kutoa pepo maana hata yesu hakuutumia ubani .. Ubani ulitumiwa na waumini wakipindihicho ambao walikua sii wakiristo nakama walikuwa sii wakiristo inaamana walikuwa wapagani walikua na dini zao ambazo yesu alizishutumu sana hadi alifikia kuwaambi enyi wanafiki.. Ninani elie walaani.. Kamahizodini. yesu angezikubali asingeweza kuzifumua kiasi hicho
Miaka ya zamani kulikuwa hakuna printing machines. Na miaka ya mwanzo kilikuwa hakuna seminari. Hivyo watu walikuwa wanajitengenezea kopi kwa kuandika kwa mkono. Na wengine walitumia watumwa wao kufanya kazi ya kukopi.Haijalishi ni Martin Luther au Yeyote yule ambaye kwa kujua au kutokujua aliondoa hata yodi moja, Biblia inasema Ole wake!
Na ndiyo maana ukisoma Torah ya Wayahudi (Books of Moses)...utagundua vitu vingi vinakinzana na hizi tafsiri za Kisasa...Kuna watu watahukumiwa kwa kuondoa maneno kadha kwenye Biblia na haijalishi ni wewe au Luther au Roman authorities...Issue hapa Biblia ibaki kuwa Msingi wa yote. Yako mengi tunaweza kuyaongea lakini niishie hapo.
Sawa,na baadaye tutaona ndugu mmoja anaitwa 'Mark Shea..a popular Catholic writer and Speaker' alivyoeleza juu ya 5 myths about 7 Books...nadhani tutafika kwenye uelewa mpana...ila yule ndugu mwingine naona anaanza kutukana na kusema maneno magumu..kwamba Walokole wananyweshwa detto na dawa ya mbu...nadhani anakosea kushambulia badala ya kueleza anachokiamini...kuhusu deuterocanonical books (Second canon...or set of seven books) na kwamba kwanini viliondolewa na kwanini havipo katika Hebrew Bible au Protestants na kwanini Cathoric Church wanavikubali tangu council of trent and florence...Ameelezea vzuri kvp....?Nimeuliza upagani Roman Catholic ni upi haswa haswa naomba kueleweshwa apo ndg....?Vitabu vile vina mafundisho mazuri mno binafsi nilikuwa mpinzani kama wewe lkn baada ya kuvisoma nikagundua kuwa waliovingiza na na kuwa miongoni mwa vitabu ktk biblia takatifu hawakukosea,tusiwe wapinzani tuu na sisi tufuatilie,baadae nikitoka ofisini nitajaribu kukudavulia japo kdogo.
Kanisa la kwanza walikuwa na Biblia? Akina Paulo walikuwa wanahubiri na Biblia? Paulo alisoma Biblia gani kupata uwezo wa kuhubiri hadi wakati mwingine kumkosoa Petro aliyekuwa mwanafunzi kabisa wa Yesu? Kanisa ndio liliamua kukusanya vitabu na kuviweka pamoja kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Pia ni Kanisa lililoamua kuwa Biblia ni sehemu ya msingi wa imani. Mababu wa Kanisa la mwanzo hawakuwa na Biblia na walipiga injili watu wakaamini ....Kama na wewe unaomba kupitia Yesu Kristo basi uko sawasawa na Biblia na hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo Biblia inasema Yn.14:6
Nadhani tusipindishe, Yako uliyoeleza nakubaliana nawe..Kwamba Kanisa linaongozwa na Roho Mtakatifu...Nakubaliana nawe kabisa..Lakini unaposema Biblia ni sehemu ya msingi wa imani...hapo tutataofautiana..Kwanini, Kwasababu Biblia siyo sehemu...hapana!! Ndiyo haswa Msingi kamili wa Imani ya Kikristo na Roho Mtakatifu anapokuelekeza kufanya anakuelekeza ufuate kilichoandikwa kwenye Biblia..na ndiyo Maana Maandiko yanasema wazi kuwa asiwepo mtu wa kuondoa hata yodi moja ya neno Katika Biblia ili ule Msingi usiyumbishwe na matakwa ya watu..na hii tunaishuhudia hata sasa kuoona waalimu, manabii, wachungaji wanapotosha kilichoandikwa kwenye Biblia na kuaminisha watu kuwa ndivyo ilivyo, Mifano ni mingi, tunaweza kupata forum nyingine kueleza.
Swali zuri sana,Miaka ya zamani kulikuwa hakuna printing machines. Na miaka ya mwanzo kilikuwa hakuna seminari. Hivyo watu walikuwa wanajitengenezea kopi kwa kuandika kwa mkono. Na wengine walitumia watumwa wao kufanya kazi ya kukopi.
Hivyo kama mtumwa alipitiwa usingizi na kuacha yodi, naye atapewa adhabu?
Vilevile vitabu vya agano jipya vipo kwenye kigiriki lugha ambayo Yesu hakuitumia. Hivyo kuna maneno na maana zilizopotea kwenye kutafsiri. Je kutakuwa na adhabu hapo?
Upagani na Roman Catholic ni vitu viwili tofauti...ni vyema kukaa kimya au kutokushare jambo kama hujui kuliko kulopoka na ukaathiri mood ya watu...Nimeomba kudhibitishiwa upagani wa Roman Catholic jamani.......?Nawakarisha zakumu,ndaga,fst,Kitaja na mengine wenye fikra hizo kama kina The bold na Niffa
Zakumi...asanteAmeshindwa kujibu. Kwetu dini zimeletwa. Na waumini wengi wanafikiri kuwa dini zilishuka kama tulivyoletewa. Kwa mfano Yesu aliishi mashariki ya kati. Yeye na wanafunzi wake walifuata dini na mila za kiyahudi. Na baada ya Yesu kuondoka, wanafunzi wake walisambaa katika maeneo yaliokuwa na jumuia za kiyahudi. Na wanafunzi wake walikuwa ni waumini wa kiyahudi na walifuata desturi za kiyahudi. Hivyo ilichukua muda kwa Ukristo kujitenga kutoka kwenye uyahudi.
Pili kulikuwa na tofauti kati ya wanafunzi. Kuna wale waliokubali wasio wayahudi kuwa wafuasi na waliokataa.
Tatu katika miaka 300 ya mwanzo, ukristo ulikuwa sio dini rasmi ya dola. Hivyo waumini katika maeneo yao wajiendeshea mambo yao na walikuwa na vitabu vyao. Vitabu vingine vilikuwa vinafafana na vingine vinatofautiana.
Baada ya ukristu kuwa dini rasmi ya dola, juhudi zilianza kufanyika za kukubali baadhi ya vitabu na kukataa vingine. Na juhudi hizi hazikuwa za siku moja.
Nne kulikuwa waumini walioishi nje ya dola ya kirumi. Hawa walikuwa na uhuru wa kujifanyia mambo yao wenyewe. Kwa mfano Yemeni, Saudi Arabia na India zilikuwa na waumini ambao toka mwanzo walifuata mafundisho ya waalimu wao na sio kutoka Roma.
Hivyo ni utawala wa Kirumi uliojenga misingi ya ukatoliki tuujuao sasa. Na pale watu walipokuwa na uhuru, walijifanyia mambo yao kama wajuavyo wao. Luther, Kakobe, Lusekelo ni mfano wa matokeo ya uhuru huo. Japokuwa wengine wanatumia uhuru huo kujinufaisha wenyewe.
Ndio Biblia inasema hivyo. Lakini ukiondoa tablets zenye amri kumi na barua za Paulo, sehemu zingine zilishuka kwa masimulizi ya mdomo. Na ilichukua muda kwa masimulizi hayo kuwekwa kwenye maandiko.Swali zuri sana,
Biblia yenyewe inasema ukiondoa hata yodi moja ni Ole..! Biblia inasema waandishi wote walikuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu tunaamini kilichokuwa kimeandikwa na Musa kwa mfano (Torah books) kilitoka kwa Mungu kabisa, issue inakuja waliokuja kucopy au wanaotafsiri kutoka ile lugha aliyoitumia Musa kuja lugha zetu..je wanafanya kama vile Roho Mtakatifu anavyotaka au alivyotaka iwe.....hapo ndipo penye shida....maana wapo waliotafsiri kwa matakwa yao.. na ndiyo Maana unaona kunakuwa na utofauti fulani si tu wa vitabu kuondolewa bali maneno yanavyotafsiriwa mfano King James Version, NIV, American Bible, Good news Bible..nk ukivisoma utaona ninachokieleza hapa... sasa ikiwa kuna yeyote kati ya hao waliocopy au kutafsiri kwa lugha zetu atakayeondoa hata yodi moja ni Ole kwake...
Kanisa la kwanza walikuwa na Biblia? Akina Paulo walikuwa wanahubiri na Biblia? Paulo alisoma Biblia gani kupata uwezo wa kuhubiri hadi wakati mwingine kumkosoa Petro aliyekuwa mwanafunzi kabisa wa Yesu? Kanisa ndio liliamua kukusanya vitabu na kuviweka pamoja kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Pia ni Kanisa lililoamua kuwa Biblia ni sehemu ya msingi wa imani. Mababu wa Kanisa la mwanzo hawakuwa na Biblia na walipiga injili watu wakaamini ....
Wewe unafikiri wale waumini walionyweshwa detto na wachungaji wao ulikuwa unadhani walifanya hivyo kwa kutumia kitabu gani...? Si ni biblia hii hii..? Shida kubwa wsliyokuwa nayo hawana elimu Mungu na Biblia .(Theology)Ndugu yangu...''tunanyweshana detto na dawa ya mbu makanisani kwetu?....wapi hiyo umenishuhudia, kwanini usitumie hii forum kufundisha na kuelewesha bila kushambulia kwa maneno makali namna hii. Detto imekuwa juice? Maandiko yanasema usitukane wengine, Nina imani unaamini ulichokiandika hakiendani na Biblia unayoiamini...
Sasa tujikite kwenye mada....Infact People don't talk much about the deuterocanonical books these days...na wanajua kwanini hawasemi...Nadhani hii forum itawafanya
Ndaga nashindwa kujua nikuweke kwenye kundi gani kwa kuniambia kama nashindwa tofautisha Ukatoliki na upagani......?Rejea post ya Kitaja,Upagani na Roman Catholic ni vitu viwili tofauti...ni vyema kukaa kimya au kutokushare jambo kama hujui kuliko kulopoka na ukaathiri mood ya watu...
Upagani ni hali ya mtu kutokutambua na kuamini uwepo wa Mungu (Jehovah) kuwa ni Mungu wa Kuabudiwa na Kumtii kwa amri zake na sheria zake sawasawa na Biblia na kwamba yeye ndiye Muumbaji wa kila kitu na anaishi tena hafananishwi na mtu yeyote au kitu chochote hapa duniani au mbinguni au kuzimu.. huyo ndiye mpagani..
Roman Catholic ni Kusanyiko la watu wanaomini Mungu yupo huwezi wafananisha na wapagani..hapana..hiyo ndiyo tafsiri yangu.
Asante
Ni sawa kabisa, na hawa Wakristo ndio waliofanya kazi ya kukusanya pamoja maadiko ya agano jipya wakiunganisha na yale ya agano la kale,kisha ikapatikana Biblia moja.Inashangaza Roman Catholic Church wanapojipa madaraka ya kuwa wao ndio waandishi wa Biblia ilihali kanisa la roma limeanzishwa rasmi katikati ya karne ya 3 na 4. Kipiindi hicho mitume wote wakiwa wamekufa. Mfalme wa kirumi Constantino ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza muungano baina ya dola na kanisa mnamo mwaka 313 AD na kukomesha nateso kwa wakristo.Mwaka 380 AD ndipo Mfalme Theodosius alipoifanya dola ya kirumi kuwa ya kidini yaani "religious state".Lengo la muungano huu sio kuwa walikuwa wanamkubali Kristo na kutaka kuwa wafuasi wake,bali walitaka kuifanya dola ya kirumi iwe na nguvu zaidi kwa kutumia kofia ya dini.Wakaiita Roman Catholic Church yaani kanisa la kirumi la mahali popote.Catholic simply meant " everywhere". Na Papa wa kwanza alianza mwaka 538 AD baada ya kusimikwa rasmi na Mfalme Justinian.Hivyo papa akapewa madaraka ya kidini na kiserikali. Yaliyootokea baada ya hapo ni kupindisha mafundisho ya Neno la Mungu na mateso na mauaji kwa Wakristo waliompinga papa na mafundisho potofu.Nitaeleza vizuri wakati mwingine nikijaliwa katika thread nyingine.Leo ngoja niishie hapa.Usitukane..We mjibu hoja yake ili kujenga uelewa nadhani ndiyo msingi wa forum hii!
Yesu alipokufa aliliacha Kanisa lisilo na jina, na pale Yerusalemu, Mitume walikuwa na kawaida ya kukutana na Kusali hata baada ya mtawanyiko alipokufa Stefano, wengi walitawanyika kwenda Asia ya Kati, Wengine wakaenda hadi Antiokia (uturuki ya sasa) na huko baada ya wengi Kuiamini Injili ya Yesu Kristo wakaamua kujiita Wakristo..Kwa hiyo Neno ukristo lilianza kuitwa mahali hapo (Mdo:11:26..)
Kwahiyo hakuna mahali ambapo Biblia inatuambia aliacha Kanisa la Catholic, au Sabato, au Lutheran au Pentecoste, au Assemblies of God au lolote unalolifahamu....Ukifahamu hilo tunaweza kuendelea zaidi ya hapo...Karibu