Ameshindwa kujibu. Kwetu dini zimeletwa. Na waumini wengi wanafikiri kuwa dini zilishuka kama tulivyoletewa. Kwa mfano Yesu aliishi mashariki ya kati. Yeye na wanafunzi wake walifuata dini na mila za kiyahudi. Na baada ya Yesu kuondoka, wanafunzi wake walisambaa katika maeneo yaliokuwa na jumuia za kiyahudi. Na wanafunzi wake walikuwa ni waumini wa kiyahudi na walifuata desturi za kiyahudi. Hivyo ilichukua muda kwa Ukristo kujitenga kutoka kwenye uyahudi.
Pili kulikuwa na tofauti kati ya wanafunzi. Kuna wale waliokubali wasio wayahudi kuwa wafuasi na waliokataa.
Tatu katika miaka 300 ya mwanzo, ukristo ulikuwa sio dini rasmi ya dola. Hivyo waumini katika maeneo yao wajiendeshea mambo yao na walikuwa na vitabu vyao. Vitabu vingine vilikuwa vinafafana na vingine vinatofautiana.
Baada ya ukristu kuwa dini rasmi ya dola, juhudi zilianza kufanyika za kukubali baadhi ya vitabu na kukataa vingine. Na juhudi hizi hazikuwa za siku moja.
Nne kulikuwa waumini walioishi nje ya dola ya kirumi. Hawa walikuwa na uhuru wa kujifanyia mambo yao wenyewe. Kwa mfano Yemeni, Saudi Arabia na India zilikuwa na waumini ambao toka mwanzo walifuata mafundisho ya waalimu wao na sio kutoka Roma.
Hivyo ni utawala wa Kirumi uliojenga misingi ya ukatoliki tuujuao sasa. Na pale watu walipokuwa na uhuru, walijifanyia mambo yao kama wajuavyo wao. Luther, Kakobe, Lusekelo ni mfano wa matokeo ya uhuru huo. Japokuwa wengine wanatumia uhuru huo kujinufaisha wenyewe.