MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

mi naomba msaada katika amri za kumi za Mungu kutoka kwa katoliki. amri ya tisa na ya kumi zinafanana kikatazo. amri kuhusu sanam haipo
 
Kulikomboa kanisa gani...? Lutheran Church limebaki Africa tuu....Ujerumani ni kama limekufa tayari, Sweden watu hata hajui kanisa nini..


Hayo maono, ndiyo yalipelekea yeye kupunguza vitabu 7 vya Agano la kale..?
Vita iliyopo ya kiroho ya kuupinga ukweli na watu wasielewe nini hasa uhalisia wa nene ni kubwa sana. Hali ya kanisa ni mbaya sana sana maana hata baada ya Luther wakati wake kupita, waliompokea baada yake nako walifanikiwa kidogo maana upinzani ni mkali mno. Kinachofanywa ni kusiliba watu wasiijue kweli ambayo kwayo ingewaweka huru. Hata huku africa ni muda tu unasubiriwa u will tell me. Makanisa mengi hayahubiri kweli waganga wa kienyeji na wapiga ramli wamejazana wakitumia majina feki ya Mungu na mwanae.
 
Vita iliyopo ya kiroho ya kuupinga ukweli na watu wasielewe nini hasa uhalisia wa nene ni kubwa sana. Hali ya kanisa ni mbaya sana sana maana hata baada ya Luther
Hiyo ni laana ndugu....Mbona Kanisa Katoliki linashamiri...huoni kuwa dhambi ya uasi inazidi inazidi kuwamaliza
 
Mada yako ina mapungufu mengi. Jipange kabla ya kutoa mada. Hapa unachoongelea wala hakiko wazi.
 
Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe
Martin Luther hakuwahi kuwa Askofu. Moja ya sababu zilizomfanya ajitenge ni pale alipoukosa Uaskofu alioutarajia kwa hamu kubwa kwa sababu alikuwa anapendwa na waamini wengi wa mji huo.
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Soma maandiko vizuri wakati Yesu anajiandaa kupaa aliwapa Muongozo wanafunzi wake soma Luka 24: 49 ina sema hivi" Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, lakini kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu. Msisitizo wake ni ujio wa roho mtakatifu na kuthibisha hilo ukisoma matendo ya mitume. Siku ya pentecoste mitume walivyojazwa nguvu ya roho wa Mungu aliyewapa ujasiri na nguvu mpya na kuwatoa hofu mioyoni mwao. Na ukisoma biblia yako hakuna hata sehemu moja watu wanaomba kupitia maria hayo ni mafundisho potofu.
 
Hiyo ni laana ndugu....Mbona Kanisa Katoliki linashamiri...huoni kuwa dhambi ya uasi inazidi inazidi kuwamaliza
Namuomba Mungu akupe macho ya kiroho. Ukisoma kitabu cha ufunuo wa yohana hutahoji utaogopa sana kinachotokea
 
Aisee umeandika blaa blaa nyingi mno ambazo haziko backed hata na mstari mmoja wa Biblia.Hiyo sio issue sana hata hivyo.Issue ya msingi hapa ni kwamba kanisa la Roma limeacha the main doctrine of the Bible na kuingiza mapokeo mengi yasiyo na msingi wa Biblia,na hivyo kuichafua imani ya kweli ya Kikristo.Let me be clear about this. Unapoingiza mapokeo au mawazo ya watu kwenye imani,it's wrong,kwa kuwa huwezi kuwa na uhakika mawazo hayo yanatoka wapi.Kwenye mambo ya kiimani hata hivyo,we know most likely the ideas would be coming from the Devil kwa kuwa nia yake siku zote ni kuiharibu imani ya kweli. Ndio maana ni muhimu kutegemea mafundisho ya biblia tu na kuachana kabisa na mapokeo.Martin Luther realized that truth and decided not to be cheated anymore.
 
Labda nikupe taarifa kama ulikuwa hujui maana ya mapokeo...

Biblia pia ni mapokeo kama ulikuwa hujui..
Hili fungu linawahusu Marko 7:6-9. Yesu akinukuu kitabu cha Isaya anasema. "Isaya alitabiri vema juu yenu...watu hawa hunishemu kwa midomo yao bali mioyo yao iko mabali nami....ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kufuata mapokeo?" Kama Biblia ni mapokeo, Yesu asingekemea kufuata mapokeo badala ya neno la Mungu.
 
Hakuna New Catholic ....Karistimatiki unaijua wewe? Karibu Emaus Centre Ubungo kila jumamosi na jumapili kuanzia saa nane ujue kazi ya Karistimatiki ndani ya Kanisa ....tena mwaka huu Pope amewaalika Wanakaristimatiki kusherekea nao miaka 50 ya kuanzishwa kwake (Grand Jubilee) siku ya Pentekoste .....
 
Martin Luther hakuwahi kuwa Askofu. Moja ya sababu zilizomfanya ajitenge ni pale alipoukosa Uaskofu alioutarajia kwa hamu kubwa kwa sababu alikuwa anapendwa na waamini wengi wa mji huo.
Halafu Mbona hawazungumzii Ile ya Martin Luther kumvua Kilemba Sister na Kumfanya Mke.. mpaka Leo Lutheran Maaskofu wanaoa wa Sababu Muasisi wao Alioa na Kuasi Kanisa Katoliki lililokataza Kuoa
 
Hata Zamani Waisraeli Waliomba Kupitia Mungu Siyo Yesu.. Sasa Huoni kwa Akili yako Hata Ww Una Mafundisho Potofu?

Ukifuatilia Kwa Makini UtajionaMjinga
 
Nataka jibu ile back ground pic ile sura ni ya nani...??
 
New catholic(More spiritual I think).....Karsmatiki
Nyinyi watu, mnajifanya mnalijua kanisa Katoliki kumbe mnaingia chaka...

What is new Catholic . ?

Karsmarik ni chama cha Kitume kama vilivyo vyama vingine vya kitume ndani ya Kanisa
 
Hapo ndo huwa sielewagi kabisa msimamo wa catholic ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…